Wakuu wa mambo ya IT nisaidieni. Ninahisi kuna mtu anafuatilia malipo ninayofanya kupitia M-PESA,kila nifanyapo malipo kwa jamaa yangu fulani kuna mtu mwingine ananipigia simu.Hawa watu wawili ninayemtumia na huyo anayenipigia hawana mawasiliano kabisa ila ni washindani kibiashara nami ni mteja wao.
Wakuu naomba msaada,je kuna uwezekano wa kwamba simu yangu inadukuliwa na huyu mwingine na kwa vipi?
Je,,nichukue hatua gani na nianzie wapi?