Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,557
- 8,672
Leo nimesikiliza hotuba ya Rais Magufuli akiongea mbele ya Rais Zuma kafanya kosa kubwa sana ambalo pengine linatokana na kutoijuwa vema historia ya ukombozi kusini mwa Africa , au kutojua historia ya TANU .
Mwalimu Nyerere alisema "..Tanzania haiwezi kuwa huru kama nchi zingine za Africa Zitakuwa kwenye ukoloni ",toka hapo miaka ya uhuru sera yetu ya nje ilikuwa kusimamia ukombozi wa mwafrica .., na katika hili alisimamia yeye mwenyewe moja kwa moja akisaidiwa mwanzo kwa karibu na OSCAR NATHANIEL KAMBONA na baadaye na RADHID KAWAWA kabla ya kuundwa rasmi kwa kamati ya Ukombozi na Mtendaji Mkuu kuwa BRIG GEN HASHIM MBITA .
Tumejitolea sana hilo kweli lakini toka mwanzo Mwalimu alikataa kabisa kuweka kigezo cha kulipwa pesa , MWALIMU"S DOCTRINE AND HUMANITY IN LIBERATION ...hata viongozi wengi waliofuatia hakuna hata mmoja akiwemo MWINYI ambaye alipokea nchi katika mazingira magumu sana baada ya mwalimu kuwekewa vikwazo na IMF na WB wakizikataa sera zake za Ujamaa NA Kujitegemea .
Mwalimu alimkabidhi Mwinyi akijuwa hilo ,alumueleza " naelewa hawa watu hawanitaki mimi kwa ajili ya misimamo yangu , namimi sintaweza kujeuka nyuma" ,ila aliahidi kumshauri na ndiye specifically alimshauri alegeze masharti ikiwemo kukubali biashara huria ...ambapo yeye angekubali ingekuwa fedheha na ushindi kwa wazungu
Miaka mitano ya Mwinyi aliendelea na mapambano Majeshi yetu yakiwa Msumbiji na mengine yalikuwa yanasimamia Uganda hadi mwaka 1986, kama kuna wakati tungejeuka na kuanza kuwadai tuliowasaidia ulikuwa huo kama tulistahimili iweje tuje kujivua nguo leo ...
TANZANIA imebaki na hiyo heshima na hata kama tunaona hawajali lakini haiondoi ukweli kuwa tunayo kura ya turufu kwa ukanda huu"sphere of infuence" watanzania hatuhitaji kulipwa na hizi nchi bali tunahitaji kufanya nazo BAISHARA basi!! tusijivue nguo uzeeni ....
Unajua ni kama kumsomesha mtu alafu unaanza kumdai kwa kuwa ana kazi na watoto wako hawana kazi .....busara ni kukaa kimya na Mungu atakupa kwa ziada ..maana ukianza kukumbusha ni kama MASIMANGO...
Hivi hata kama watatulipa ....vipi kuhusu DAMU za askari wetu waliokufa kwenye mapambano...na familia zao wao wanastahili kulipwa nini ???? kuna ma agent TISS na wa jeshi walikuwa wakiingia na wapigania uhuru hadi SOUTH AFRICA wapo waliokamatwa ...na hata miili yao isionekane na wala ndugu zao hawajui wako wapi kutokana na nature ya usiri wa kazi hizo wakati huo ......watadai nini???
Viongozi walikuwapo enzi ya Mwalimu haya yakifanyika wapo ,ni vema wakamshauri Rais kuwa hata kwa mila za kiafrica Wema huwa haukumbushwi...bali muungwana ukimtendea akabaki na deni atabaki kulipa tu ..kwa kuwa atabakia na ile kauli " sijui nikulipe nini "....isije siku tukakutana na viongozi wasio wastaarabu huko wakatuambia " watanzania tuwalipe shilingi ngapi kwa kutusaidia ukombozi na kutoa maisha yenu?"
Misingi yetu ilikuwa ya UTU na UHURU NA HESHIMA WA MWAFRICA KAMA TUMEUPATA BASI TUFANYE KAZI KWA BIDII