Kuchelewa kwa fedha za field IFM

Kuchelewa kwa fedha za field IFM

Joined
Apr 30, 2013
Posts
93
Reaction score
19
Ndugu wana jukwaa chuo chetu cha usimamizi wa fedha (IFM) kimeamua kututesa bila sababu ya msingi kwani tuliahidiwa kuingiziwa fedha za field baada ya uhakiki kumalizika ila cha kushangaza mpaka dakika hii uhakiki umekamilika ila hakuna mwanafunzi yoyote aliyeingiziwa fedha za kujikimu.

Fedha chuo kimekabidhiwa kutoka hazina ila hawataki kutuwekea mpaka tusaini wakati Mama Ndalichako alituhakikishia fedha za kujikimu zitaingia kwenye akaunti za wanafunzi na kusainiwa pindi chuo kitakapofunguliwa.

Swali la kujiuliza wao wanataka wanafunzi wasaini fedha ndio waingiziwe, hawajui kama wanafunzi wapo likizo na tunaishi mikoa tofauti kwanini wakiuke Maagizo ya mama Ndalichako mbona vyuo vingine wameingiziwa?

Tumechoka na unyanyasaji unaoendelea IFM
 
KIU education wanamaliza field kesho na hawajawai Kupewa hata 100/=...heshima kwao kwa uvumilivu
 
Mlipoambiwa mtaisoma namba mlidhani nini? Na bado huo ni mwanzo tu
 
Mkuu ni kweli pesa zimeshafika vyuoni, bt wanaleta ukiritimba mpaka Watu wasaini wakati wengine wapo mikoani, nimeshangaa leo nimepigiwa simu nikasaini na mwisho wa kusaini ni j5 ambaye hatasaini hapati kitu... Huu ni unyanyasaji wa hali ya juu
 
Mkuu ni kweli pesa zimeshafika vyuoni, bt wanaleta ukiritimba mpaka Watu wasaini wakati wengine wapo mikoani, nimeshangaa leo nimepigiwa simu nikasaini na mwisho wa kusaini ni j5 ambaye hatasaini hapati kitu... Huu ni unyanyasaji wa hali ya juu
Duuuh hii nchi bhana
 
kwa habar nilizopata waliosaini wameshaingiziwa sasa tuliohuku vijijini mnatusaidiaje jamani hali ni ngumu tunakufaa na njaa simtuekee hizo fedha
 
Back
Top Bottom