Joseverest
JF-Expert Member
- Sep 25, 2013
- 53,261
- 72,431
Tunaoumia ni sisi mashabiki halafu wao wanachukulia vitu easy tu! Sisi kama mashabiki na wanachama hai tuna haki ya kuhoji, hatutaki siasa na porojoKama vipi mashabiki tuandamane! Haiwezekani mpaka sasa timu na mashabiki tunatumia nembo ya mdhamini wa zamani, yaani sportpesa!
Hii ni hujuma ya wazi kabisa kwa mdhamini wetu mpya Mbet!
Na mimi binafsi naona kuna uzembe umetokea hawataki kuweka wazi (wataaibika) na ndio maana wanajificha kwenye kichaka cha ''SABABU ZILIZO NJE YA UWEZO WETU'' na Mdhamini.... Kipindi chote hicho walikuwa hawajui kuwa mkataba na Sportpesa unaisha msimu huu, juzi hapa wakapata aibu ile ya kubandua logo ya mdhamini wa zamani wakaweka mdhamini mpya juu kwa juu (hii tunaita kukosa weledi)
Tukubali tu pale kuna kiongozi fulani hajawajibika ipasavyo au anatufanyia hujuma au kuna mgongano wa kimaslahi na kusababisha UZEMBE na sintofahamu hii kwa mashabiki hadi leo...(YAPASWA ALAUMIWE naawajibishwe kwa onyo)
Wenzetu majirani wao wamewahi na kesho kwenye JAMBO LAO wanakinukisha sisi tunabaki mtaani macho kodo tunaringishiwa na mtani.
Sisi kama mashabiki lialia wa Lunyasi mnyama tunaomba uzembe huu usijirudie...
Kutoka tawi la Mpira na Maendeleo - Fire Upanga Magharibi