Kuchakachuliwa kwa matokeo ya usaili uhamiaji.

Kuchakachuliwa kwa matokeo ya usaili uhamiaji.

moforoo

New Member
Joined
Nov 26, 2013
Posts
4
Reaction score
29
Hivi karibuni Makao Makuu ya Uhamiaji walifanya usailli wa watumishi wapya, Konstebo na Koplo. Baadhi ya waliochaguliwa hawakufanya usaili baada ya kuonekana kukosa sifa na kuwa na vyeti feki lakini wamechomekwa baada ya kila kichwa kutoa milioni 2 na waliochomekwa ni zaidi ya watu 10. Kibaya zaidi ni kwamba wenye sifa wametolewa na kuchomekwa wenye uwezo kifedha jambo ambalo limeleta manung'uniko makubwa na baadhi kutaka kumuona waziri wa mambo ya ndani
Kutokana na vipimo vya afya baadhi ya waliochomekwa wameonekana hawafai na wengine kukimbia kupima, wale waliochujwa kwa afya wanadai warudishiwe fedha yao kwakuwa hawakujulishwa kabla. Tunaziomba mamlaka husika zifuatilie suala hili kama walivyo fanya polisi na kutoa majibu hadharani. Ni mimi muathirika wa usaili
 
duh hii nchi sjui tunakoelekea
 
Back
Top Bottom