Kuchaguliwa chuo moja kwa moja Diploma

Kuchaguliwa chuo moja kwa moja Diploma

Mwanakulipata

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2018
Posts
720
Reaction score
1,210
Habari, kuna mdogo wangu amemaliza form 4 mwaka jana, kwenye self form nilimuombea advance maana alibalance CBG pamoja na HKL, lakini akachaguliwa kusoma ACCOUNTANCY huko CBE mwanza campus, cha ajabu ni kwamba tumepiga simu chuoni kuulizia taratibu za Ada tumeambiwa ada yake ni +1M...

Sasa nachojiuliza inakuaje hawa wanaochaguliwa moja kwa moja (Directly entry) ada yao inakuwa sawa na hawa wanaoomba wenyewe (indirectly entry)??

Mimi nipo ATC arusha...ambapo ada kwa hawa madogo wa moja kwa moja ambao wapo under government sponsor ni 300K ambap chakula wanakula hapa hapa bure pamoja na malazi (Hostel) bure na hii sio tu hapa hata DIT pamoja na MUST..sijajua vyuo vingine.

Hii naona sio sawa otherwise kama wamepanga kupunguza wanafunzi kuendelea kusoma...maana mwanafunzi kutoka shule zetu hizi then umpeleke chuo bila ridhaa yake ingalikuwa alikuw anatak advance tena alipe hela nyingi pamoja na kula ajitegemee hii ni kukatisha ndoto za watu..

Tamisemi asanteni dogo atasoma ila kwa mbindee sana....

Regard, mwanakulipata
 
Angalieni kama mnamudu si akasome advance Private school
 
Back
Top Bottom