Kubenea na kisa cha uwili mtakatifu

Kubenea na kisa cha uwili mtakatifu

Maramla

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2014
Posts
588
Reaction score
648
Katika makala ya mwisho jana nilionesha jinsi nadharia ya fremu (framing theory) inavyoweza kutusaidia kuwajua "WATU WASIOJULIKANA" katika kuwatambua waliomdhuru mwanasheria wetu mahiri Tundu Lissu.

Katika kudadavua kauli, maandiko na hata maneno ya baadhi ya watu wa mwanzo kuzungumza sakata hili tukaibua wahusika wengine muhimu "WATU WASIOTAKA KUJULIKANA."

Sasa fuatilia kisa cha uwili mtakatifu: Jana nimelisoma gazeti la MwanaHalisi la Mbunge wa Chadema, Saed Kubenea na kubaini yafuatayo kuhusu "WATU WASIOTAKA KUJULIKANA" kwa mujibu wa nadharia ya fremu.

1.Ni wazi kwa stori ya Kubenea kuwa kuna watu "WASIOTAKA KUJULIKANA" wapo katika mji wa Ontore Njorobi (almaarufu Nairobi) ambao ingawa walitakiwa kumtazamia kwa karibu mpendwa wetu Lissu wanaonekana wanafanyakazi nyingine yenye lengo mahsusi.

Tuwaache kwanza. Sasa ukitumia nadharia ya fremu utakuta habari kuu ya MwanaHalisi ya jana inamnukuu Mhe. Lissu kwa kina eti akisisitiza anawajua waliomshambulia na.hivi na vile.

Lissu inafahamika yuko ICU baada ya oparesheni kadhaa na taarifa ya Mwenyekiti Mbowe ya juzi imethibitisha hilo.Hapa ama Kubenea ni muongo au "WATU WASIOTAKA KUJULIKANA" ndio wanamletea uongo;

2.Ukisoma habari kuu ya jana ya MwanaHalisi utakuta mahojiano ya kina kati ya gazeti hilo la Kubenea na dereva wa Lissu akieleza mengi lakini kubwa akikanusha kuhusu "WATU WASIOJULIKANA."

Yeye anasema anawajua watu waliokuwa wakiwafuatilia siku nyingi na hata siku ya tukio aliwaona kuanzia walipoanza safari Bungeni kisha gari lao moja likaishia getini lingine likawafuata hadi ndani. Kwa fremu hii dhana ya "WATU WASIOJULIKANA" inaanguka rasmi. Lissu na dereva wake wanawajua wahusika.

Kwamba dereva huyu ndiye Tanzania Daima la jana pia lililomweleza kwa kichwa cha habari cha kishambenga mno kuwa "Dereva Mnayemtaka Yuko Nairobi" na Mbowe naye akashadidia kuwa dereva huyo yuko Nairobi akipatiwa matibabu ya kisaikolojia. Huyu ndiye dereva ambaye Mbowe anasema hawezi kuhojiwa na Polisi kwa sababu mgonjwa tena wa kisaikolojia lakini Kubenea kamhoji tani yake na kuchapisha mahojiano naye.

Hapa tena ama Kubenea ni muongo au "WATU WASIOTAKA KUJULIKANA" wanamletea uongo.

3. Katikati ya stori hiyo kuna para dereva wa Lissu anapoeleza jinsi alivyowachenga "WATU WASIOJULIKANA" akiwa anatoka Dar lakini Kubenea anahoji utata wa kauli hiyo ya dereva wa Lissu akionekana kushangaa kuwa kama dereva wa Lissu aliingia njia ya porini kwa nini waliokuwa wakimfukuzia hawakumfuata kummaliza huko huko?

"Utata" anaandika Kubenea akihoji maelezo ya dereva wa Lissu.Kwa nini kubenea anahoji maneno ya dereva wa Lissu ana chochote tofauti anachokijua labda kutoka kwa "WATU WASIOTAKA KUJULIKANA?"

Sasa kesho mida kama hii tulia tuli hapo ulipo katika kufaidika na nadharia ya fremu.

Nitakuletea kisa kimoja muhimu cha "WATU WASIOTAKA KUJULIKANA."

Usikose

By political Jurist, UDOM.
 
Kubenea naye amezidi kidomodomo, kuna kipindi aliandika ati Ben Saanane amepatikana kumbe ujinga mtupu.
Nadhani atulie sasa.
PRAY FOR TUNDU LISU

Kwa Hisani Ya Watu Wa Mbeya!
 
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom