Kubeba mishikaki kwenye bodaboda itaisha lini?

mende 2014

JF-Expert Member
Apr 13, 2014
763
131
Jamaa huyu anafaa kutumbuliwa jipu maana anahatarisha maisha ya watu.
Vile vile abiria hao nao ni majipu maana kwa nini wakubali kubebwa hivyo?
20160307_043739.jpg
 
Kujaza abiria kwenye daladala kupita kiwango kwani kutaisha lini.
 
Hakutaisha kwa sababu askari wa usalama barabarani wameacha kutoa elimu ya usalama barabarani na kugeuka kuwa mawakala wa Serikali wa kukusanya mapato kwa njia ya faini. Kwa hiyo muda wote wanaomba mtumiaji wa chombo cha moto akosee ili wampige faini.
 
Traffic wakiacha kuomba rushwa tatizo litaisha maana watasimamia sheria.
 
kunamambo hayataisha,
......ila yanaeza pungua kwakiasi kikubwa
 
Niliona India sababu waendesha pikipiki kule ni wengi na wanapigwa faini bila kukoma...Askari wakapitisha kila bodaboda akikamatwa na kosa anakula viboko hapo hapo tena vya maana...Nadhan sheria hiyo ingekuja bongo ingekuwa muarobain
 
Hakutaisha kwa sababu askari wa usalama barabarani wameacha kutoa elimu ya usalama barabarani na kugeuka kuwa mawakala wa Serikali wa kukusanya mapato kwa njia ya faini. Kwa hiyo muda wote wanaomba mtumiaji wa chombo cha moto akosee ili wampige faini.

Askari wa barabarani si kazi Yao kutoa elimu. Elimu unapata kwenye TRAFIC SCHOOLS then unapewa leseni. Unapopewa leseni inamaana umesha jifunza trafic rules na driving technicals.
Ukifanya makosa ni haki huyo askari akakupa faini, lakini pia anaweza kuku hurumia na akakupa onyo.
 
Niliona India sababu waendesha pikipiki kule ni wengi na wanapigwa faini bila kukoma...Askari wakapitisha kila bodaboda akikamatwa na kosa anakula viboko hapo hapo tena vya maana...Nadhan sheria hiyo ingekuja bongo ingekuwa muarobain

Da hii kali sana, bora walete na huko Tanzania, maana watu wanalalamika eti askari wa barabarani wanakzi ya kukusana hela za faini badala ya kutoa elimu. sasa badala ya kutozwa faini bora wachapwe viboko.
 
Niliona India sababu waendesha pikipiki kule ni wengi na wanapigwa faini bila kukoma...Askari wakapitisha kila bodaboda akikamatwa na kosa anakula viboko hapo hapo tena vya maana...Nadhan sheria hiyo ingekuja bongo ingekuwa muarobain
Hahahahajaaaaaaaaaaa hii inaweza kumaliza tatizo maana wabongo ni wagumu kuelewa na kutekeleza kwa hiari.
 
Back
Top Bottom