Kubali kataa Ngeleja ndio rais 2015

Kubali kataa Ngeleja ndio rais 2015

Joined
Oct 9, 2014
Posts
95
Reaction score
13
BREAKING NEWS:NGELEJA AONGOZA TAFITI KWENYE MEDIA URAISI UPANDE WA VIJANA

Taarifa iliyotolewa Jana na jarida la kimataifa la habari (International Journal), zinaonesha Ngeleja Willium ambaye ni kijana mwenye miaka 47 anaongoza kwa 32% kwenye mbio za uraisi upande wa vijana nchini Tanzania, anayemkaribia Ngeleja ni ndg Emmanuel Nchimbi aliyewah kuwa Waziri wa mambo ya Ndani ya nchi mwenye 14% na January Makamba anafuatia katika nafasi ya tatu akiwa na 8%.

Hata hivyo jarida hilo lilionyesha kutokukubaliana na mawazo ya mmoja kati ya vijana waliotangaza nia ya uraisi kutokana na umri kutokukidhi vigezo , kijana huyo ni ndg Khamis Kigwangala ambaye ana umri wa miaka 38 tofauti na umri wa kuanzia kama kigezo kwa mgombea uraisi wa miaka 40... Jarida hili lilimtaja Ngeleja kuwa na nafasi kubwa ya kufika tatu bora ya wagombea uraisi kwa ujumla na hata pengine kuweza kuwa raisi wa jamhuri ya Muungano.

Jarida hilo lilitoa ufafanuzi kuhusu Waziri wa Ulinzi ndg Hussein Mwinyi kuhusishwa na uraisi na liliandika kuwa Hussein Mwinyi ana 40% za kuwa raisi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kakini sio raisi wa Muungano kwani ana upinzani mkubwa sana kutoka kwa mh.Willium Mganga Ngeleja.

SABABU WALIZOZITOA KAMA MSINGI WA MCHANGANUO HUU NI ZIFUATAZO:

1. Mh. Ngeleja atakumbukwa kama Nguzo ya msingi katika sekta ya nishati na madini katika awamu ya nne,. kwani mpaka tunafikia hapa kwa hali hii ya nishati ni kutokana na kazi kubwa aliyoifanya mh.Ngeleja katika kipindi chake cha utawala katika Wizara ya Nishati na madini kwa muda wa miaka 5 na miezi 8, ndiye aliyehakikisha swala la gesi ya mtwara kufikia hapa lilipo kutokana na ujenzi wa bomba lenye urefu wa km 500 kutoka mtwara ilipo gesi mpaka maeneo ya tabata jijini dar es salaam, Sera na sheria mpya ya nishati na Madini ya mwaka 2009 na mwaka 2010 ambayo inatumika mpaka sasa na serikali kitu ambacho kilizibiti mianya yote ya upotevu wa rasilimali madini na mengine mengi.

2. Kutokuhusika katika sakata la Escrow, najua wengi mtashangaa kwani mlishasikia kuwa mh.Ngeleja alipata mgawo wa mil 42 za kitanzania kutoka katika mgawo wa fedha za escrow lakini kwa uchunguzi mkubwa uliofanywa na jarida hili hata kwa kumuhoji CAG pamoja na kuipitia ripoti yake hata baada ya kukagua majina yaliopo katika bank statements za Bank-M na ile benki nyingine jina la Willium Mganga Ngeleja halikuonekana popote na ukweli ni kwamba hajashiriki kwa lolote lile katika sakata la escrow kitu kinachompa nguvu kubwa sana ndani ya chama na hata nje ya chama, swala hili linamsafishia njia kijana huyu na ni hatari kubwa sana katika Mbio za uraisi hapo mwakani, wenye kuona mbali watakubaliana na taarifa hii.

3. Mambo mengi aliyoyafanya ndani ya jimbo lake kwa muda wa miaka 9 mpaka sasa, ukilinganisha na vijana wengine waliotangaza nia mh. Ngeleja ni moja ya wabunge waliofanya mambo makubwa sana ndani ya jimbo lake na mpaka leo wapinzani wanaliogopa jimbo lile kwani hawatak hata kulisogelea kwa sababu hakuna cha kukosoa kazi ni kubwa sana iliyofanyika na ni dhahiri kuwa kijana huyu anafanya sana kazi pindi anapokabidhiwa.

4. Kukubalika sana kanda ya ziwa, mh.Ngeleja ni moja ya viongozi wanaokubalika sana kanda ya ziwa kulingana na uwezo wao kiutendaji na hata kuishi na kuzungumza na wananchi wa hali ya chini sana, ukifika kanda ya ziwa ukimtaja Willium Mganga Ngeleja iwe ni kwa viongozi wa dini zote nchini, kwa wanaopenda kunywa pombe, waimba kwaya na aina zote za nyimbo zenye kumsifu Mungu, vijana wa aina zote, wazee mababu kwa mabibi watakwambia mh. Ngeleja ndie simba wa kanda ya ziwa, ni mtu wa watu mwenye kusikiliza na kusaidia panapowezekana,, kwa hili uraisi 2015 kazi ni kubwa sana hakuna namna unaweza kuwashawishi watu wa kanda ya ziwa usipolipitisha jina la Ngeleja kwenye majina ya wagombea uraisi..

5. Kijana tegemeo anayeaminika na mh. Jakaya Mrisho Kikwete raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, itakumbukwa kuwa ndiye aliyekuwa Waziri wa nishati na madini na waziri mchapakazi aloyewah kutokea katika wizara ya nishati kitu kilichomfanya Jakaya Kikwete kumpenda na kumuamini sana, itakumbukwa mwaka 2012 mwezi May mh.Raisi alipokuwa nje ya nchi mh.Willium Ngeleja aliandika barua ya kujiuzulu kutoka wizara ya nishati kutokana na shinikizo la bunge pamoja na viongozi baadhi ndani ya chama, na mh. Ngeleja alifanya hivyo kama dhana na ya uwajibikaji popote pale duniani, Mh.Raisi alipopata taarifa ya kujiuzulu kwa Ngeleja alipokuwa nje ya nchi alimuomba sana kuutengua uamuzi wake na Ngeleja alisimamia hilo kwani anazitambua vizuri principle za uongozi za kiuwajibikaji katika kunusuru, Mh.Raisi aliumia sana na alikuwa hana namna na alikuja kuvunja baraza alipofika nchini na kuunda baraza jipya, hata hivyo juzi katika reshuffle ya tatu mh.Raisi alimuomba Ngeleja kurudi kwenye baraza la mawaziri akamsaidie katika wizara ya maliasili na utalii na mh.Ngeleja aligoma na kumwambia raisi kuwa ningependa kuwafanyia kazi watanzania kwa muda mrefu kazi ambayo itaonekana nikuombe uniwie radhi lakini tupo pamoja daima, kuukataa uwaziri wa Maliasili kwa mh.Ngeleja kulitosha kuonesha namna Ngeleja asivyokuwa na uchu wa madaraka na nia yake yakuliongoza taifa katika njia sahihii alipewa muda wa kutosha na mapenzi ya dhati na nchi yake..mapenzi haya ya mh.Raisi kwa Ngeleja ni silaha tosha inayomfanya Ngeleja kuwa na nguvu kubwa ya uraisi nyuma ya vijana wenzake wenye nia ya uraisi...

MWISHO
Kwa mchanganuo huo kutokana na jarida la kimataifa (International Journal) inaonyesha kuwa kwa ujumla mpaka sasa wagombea wote wenye nia ya uraisi wanamuogopa sana Ngeleja na wanadai kuwa kwake kimya ni hatari zaidi kwani wanashindwa kujua wapi waanzie kumchunguza na hata kumjadili, "Ngeleja ni tishio kubwa sana" alisikika akiongea mmoja ya watangaza nia mwenye nguvu pia ambaye ana Nywele nyekundu mchanganyiko na kijani"...

Nawasilisha
Wenu, mchambuzi wa siasa nchini
 
Hivi wapuuzi kumbe ni wengi sana hapa Tanzania?ilo jalida ni la wapi?kwa umaarufu upi apewe uraisi?acheni kuchezea maisha ya Watanzania na vikampeni vyenu uchwara.
 
Hivi tafiti ndo zinatupatia Mgombea Uraisi au ni SIFA za mtu huyo tunazozijua, kama sielewi. maana tafiti zimezidi na hatujui zina malengo gani.
 
Ngeleja atakumbukwa kwa kuulea mgawo wa umeme. Sasa anavuna chake toka kwenye fedha za IPTL. Akiwa Rais, hautakuwa mgao tena, itakuwa giza totoro kuanzia January hadi December. Viwanda vyote vitafungwa. GOD forbid!
 
sisi kina gogo la shamba kinachotushangaza ni kule kuona wagombea wa ccm wote ni kutoka Tanganyika, alafu kama huu utabiri wao ni kweli, watutabirie nani atashinda katika mechi ya mtani jembe kati ya Simba na Yanga
 
Haya mambo na tafiti mnazitoa wapi hebu kuweni na adabu msituletee tafiti za vyumbani bana tunaakili zetu subirini wakati ufike wakombe watangaze ndipo tuwapime vema sasa.
 
Siwezi soma upuuzi kama huu, haiwezi na haitatokea ngereja kuwa rais TZ
 
BREAKING NEWS:NGELEJA AONGOZA TAFITI KWENYE MEDIA URAISI UPANDE WA VIJANA

Taarifa iliyotolewa Jana na jarida la kimataifa la habari (International Journal), zinaonesha Ngeleja Willium ambaye ni kijana mwenye miaka 47 anaongoza kwa 32% kwenye mbio za uraisi upande wa vijana nchini Tanzania, anayemkaribia Ngeleja ni ndg Emmanuel Nchimbi aliyewah kuwa Waziri wa mambo ya Ndani ya nchi mwenye 14% na January Makamba anafuatia katika nafasi ya tatu akiwa na 8%.

Hata hivyo jarida hilo lilionyesha kutokukubaliana na mawazo ya mmoja kati ya vijana waliotangaza nia ya uraisi kutokana na umri kutokukidhi vigezo , kijana huyo ni ndg Khamis Kigwangala ambaye ana umri wa miaka 38 tofauti na umri wa kuanzia kama kigezo kwa mgombea uraisi wa miaka 40... Jarida hili lilimtaja Ngeleja kuwa na nafasi kubwa ya kufika tatu bora ya wagombea uraisi kwa ujumla na hata pengine kuweza kuwa raisi wa jamhuri ya Muungano.

Jarida hilo lilitoa ufafanuzi kuhusu Waziri wa Ulinzi ndg Hussein Mwinyi kuhusishwa na uraisi na liliandika kuwa Hussein Mwinyi ana 40% za kuwa raisi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kakini sio raisi wa Muungano kwani ana upinzani mkubwa sana kutoka kwa mh.Willium Mganga Ngeleja.

SABABU WALIZOZITOA KAMA MSINGI WA MCHANGANUO HUU NI ZIFUATAZO:

1. Mh. Ngeleja atakumbukwa kama Nguzo ya msingi katika sekta ya nishati na madini katika awamu ya nne,. kwani mpaka tunafikia hapa kwa hali hii ya nishati ni kutokana na kazi kubwa aliyoifanya mh.Ngeleja katika kipindi chake cha utawala katika Wizara ya Nishati na madini kwa muda wa miaka 5 na miezi 8, ndiye aliyehakikisha swala la gesi ya mtwara kufikia hapa lilipo kutokana na ujenzi wa bomba lenye urefu wa km 500 kutoka mtwara ilipo gesi mpaka maeneo ya tabata jijini dar es salaam, Sera na sheria mpya ya nishati na Madini ya mwaka 2009 na mwaka 2010 ambayo inatumika mpaka sasa na serikali kitu ambacho kilizibiti mianya yote ya upotevu wa rasilimali madini na mengine mengi.

2. Kutokuhusika katika sakata la Escrow, najua wengi mtashangaa kwani mlishasikia kuwa mh.Ngeleja alipata mgawo wa mil 42 za kitanzania kutoka katika mgawo wa fedha za escrow lakini kwa uchunguzi mkubwa uliofanywa na jarida hili hata kwa kumuhoji CAG pamoja na kuipitia ripoti yake hata baada ya kukagua majina yaliopo katika bank statements za Bank-M na ile benki nyingine jina la Willium Mganga Ngeleja halikuonekana popote na ukweli ni kwamba hajashiriki kwa lolote lile katika sakata la escrow kitu kinachompa nguvu kubwa sana ndani ya chama na hata nje ya chama, swala hili linamsafishia njia kijana huyu na ni hatari kubwa sana katika Mbio za uraisi hapo mwakani, wenye kuona mbali watakubaliana na taarifa hii.

3. Mambo mengi aliyoyafanya ndani ya jimbo lake kwa muda wa miaka 9 mpaka sasa, ukilinganisha na vijana wengine waliotangaza nia mh. Ngeleja ni moja ya wabunge waliofanya mambo makubwa sana ndani ya jimbo lake na mpaka leo wapinzani wanaliogopa jimbo lile kwani hawatak hata kulisogelea kwa sababu hakuna cha kukosoa kazi ni kubwa sana iliyofanyika na ni dhahiri kuwa kijana huyu anafanya sana kazi pindi anapokabidhiwa.

4. Kukubalika sana kanda ya ziwa, mh.Ngeleja ni moja ya viongozi wanaokubalika sana kanda ya ziwa kulingana na uwezo wao kiutendaji na hata kuishi na kuzungumza na wananchi wa hali ya chini sana, ukifika kanda ya ziwa ukimtaja Willium Mganga Ngeleja iwe ni kwa viongozi wa dini zote nchini, kwa wanaopenda kunywa pombe, waimba kwaya na aina zote za nyimbo zenye kumsifu Mungu, vijana wa aina zote, wazee mababu kwa mabibi watakwambia mh. Ngeleja ndie simba wa kanda ya ziwa, ni mtu wa watu mwenye kusikiliza na kusaidia panapowezekana,, kwa hili uraisi 2015 kazi ni kubwa sana hakuna namna unaweza kuwashawishi watu wa kanda ya ziwa usipolipitisha jina la Ngeleja kwenye majina ya wagombea uraisi..

5. Kijana tegemeo anayeaminika na mh. Jakaya Mrisho Kikwete raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, itakumbukwa kuwa ndiye aliyekuwa Waziri wa nishati na madini na waziri mchapakazi aloyewah kutokea katika wizara ya nishati kitu kilichomfanya Jakaya Kikwete kumpenda na kumuamini sana, itakumbukwa mwaka 2012 mwezi May mh.Raisi alipokuwa nje ya nchi mh.Willium Ngeleja aliandika barua ya kujiuzulu kutoka wizara ya nishati kutokana na shinikizo la bunge pamoja na viongozi baadhi ndani ya chama, na mh. Ngeleja alifanya hivyo kama dhana na ya uwajibikaji popote pale duniani, Mh.Raisi alipopata taarifa ya kujiuzulu kwa Ngeleja alipokuwa nje ya nchi alimuomba sana kuutengua uamuzi wake na Ngeleja alisimamia hilo kwani anazitambua vizuri principle za uongozi za kiuwajibikaji katika kunusuru, Mh.Raisi aliumia sana na alikuwa hana namna na alikuja kuvunja baraza alipofika nchini na kuunda baraza jipya, hata hivyo juzi katika reshuffle ya tatu mh.Raisi alimuomba Ngeleja kurudi kwenye baraza la mawaziri akamsaidie katika wizara ya maliasili na utalii na mh.Ngeleja aligoma na kumwambia raisi kuwa ningependa kuwafanyia kazi watanzania kwa muda mrefu kazi ambayo itaonekana nikuombe uniwie radhi lakini tupo pamoja daima, kuukataa uwaziri wa Maliasili kwa mh.Ngeleja kulitosha kuonesha namna Ngeleja asivyokuwa na uchu wa madaraka na nia yake yakuliongoza taifa katika njia sahihii alipewa muda wa kutosha na mapenzi ya dhati na nchi yake..mapenzi haya ya mh.Raisi kwa Ngeleja ni silaha tosha inayomfanya Ngeleja kuwa na nguvu kubwa ya uraisi nyuma ya vijana wenzake wenye nia ya uraisi...

MWISHO
Kwa mchanganuo huo kutokana na jarida la kimataifa (International Journal) inaonyesha kuwa kwa ujumla mpaka sasa wagombea wote wenye nia ya uraisi wanamuogopa sana Ngeleja na wanadai kuwa kwake kimya ni hatari zaidi kwani wanashindwa kujua wapi waanzie kumchunguza na hata kumjadili, "Ngeleja ni tishio kubwa sana" alisikika akiongea mmoja ya watangaza nia mwenye nguvu pia ambaye ana Nywele nyekundu mchanganyiko na kijani"...

Nawasilisha
Wenu, mchambuzi wa siasa nchini

This is shit Now!
Na wewe umeibuka na TWAWEZA yako. Haya tembea na uchafu wako.
 
Raisi wetu ajaye ni DR SLAA tuuu ccm wameshapoteza sifa za kugombea uraisi
 
......Mbavu zangu......!!! Uwiiiii, hili bonge la original comedy. Nimependa creativity yako, hii kwa comedy utauza sana, nakushauri kaiwekee hati miliki mapema asikupige bao mtu. Nimesoma kichwa cha habari tu, sijui ulichoandika ndani, NIKACHEKA sana, sana, yaani namaanisha cheka ile mbaya!!
 
alikataa uwaziri......................
alibembelezwa asijihuzuru..........................
kama ameweza kukueleza yote hayo wewe, kesho atawaeleza mambo ya tanzania wasiohusika!
 
Hizo n harakat za kumpaisha tu ngeleja, kiukweli mjani ya kijani hayaungwi kwenye chai
 
Back
Top Bottom