Kubali au kataa, ila wachaga ndio Wanaotikisa Nchi japo wanakumbana na upinzani!

Kubali au kataa, ila wachaga ndio Wanaotikisa Nchi japo wanakumbana na upinzani!

Davidmmarista

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2024
Posts
2,266
Reaction score
4,427
Wadau wa JF, hope mko poa! Kama kawaida yetu hapa Jamiiforums, tunapenda kutafuta "mchawi" wa maendeleo, si ndio? Leo nataka tuzungumze kuhusu kabila moja ambalo linachangamsha hii nchi, linaibua mijadala, na kwa namna fulani, lipo kwenye radar ya wengi Wachaga! Kabla hujakunja ndita, shusha kipupwe cha maji kwanza. Leo tutajadiliana kwa hoja, tukitupa maneno ya "chuki binafsi" kwenye dustbin.

Wachaga ni Moto wa Kuotea Mbali
Bila hata kulazimisha, ukitembea kwenye miji mingi Tanzania, ukiona biashara inasonga mbele na mtu anapiga pesa bila wasiwasi, kuna uwezekano mkubwa kuwa ni Mchaga. Ukifika Kariakoo, unakuta yule jamaa mwenye duka la jumla analeta mzigo kila wiki, ukienda Sinza, bar na lounges nyingi zinaendeshwa na Wachaga, ukifika Arusha...sijui niseme nini, wenyewe ndo wanaipangilia hiyo mji.

Lakini si biashara tu, hata kwenye siasa na nafasi za uongozi kuna wachache wa kutoka Moshi lkn influence yao inaonekana. Kuna watu watasema Wachaga ni wachoyo, hawasaidii wenzao lakini ukikaa nao, utagundua kuwa ni watu wa mikakati na juhudi. Hawategemei kupewa msaada, wanajitengenezea fursa!

Kabila la Kufundisha Nchi Kustawi
Kama kuna sehemu unataka kujifunza biashara, basi peleka tour Moshi. Wana maduka, wana hoteli, wana mahoteli, wana real estate na wana kila aina ya biashara unayoweza kuimagine. Moshi ni moja ya miji midogo inayoingiza pesa ndefu nchini. Wamehakikisha watoto wao wanapata elimu nzuri na wako tayari kumlipia mwanao ada kwa mkopo (ila utalipa kila senti bila excuse!).
Unaweza kusema "ah, mbona kila kabila lina wafanyabiashara wake?" Ndio, ila je, ni kabila gani limewahi kufanikisha mabadiliko ya biashara nchi nzima? Wachaga wamefanikiwa kuinfluence watu wa makabila mengine kuacha utegemezi na kuanza kujishughulisha. Ndio maana ukiona biashara inakuwa mtaani, usishangae kusikia msemo maarufu wa kimtaa: "Huyu lazima ana damu ya Kichaga!"

Wanaface Opposition?

Hili nalo halikwepeki! Wachaga wamefanikiwa sana kiasi kwamba kuna watu wanaona wanameza kila kitu. Serikali nayo mara nyingine imekuwa ikiweka vigingi visivyoeleweka mikopo haitoki kirahisi kwao, urasimu kwenye biashara upo, na hata kwenye siasa, sio rahisi kwao kupenya kwa urahisi kwenye nafasi kubwa.

Pia kuna dhana kuwa Wachaga wanajiona juu sana. Ukweli ni kwamba wao wanaamini katika self-reliance (kujitegemea). Ukikaa na Wachaga wachache tu, watakuambia wazi kwamba "mtu hajengwi, anajijenga!" Sasa kwa wale waliokuzwa kwa mentality ya "serikali inisaidie", hii inawauma sana.

Ukweli ni kwamba, whether you love them or hate them, Wachaga wameleta muamko mkubwa nchini. Wamebadili mindset ya watu kuhusu biashara, uwekezaji na maisha kwa ujumla. Kama kuna jambo ambalo kila Mtanzania anaweza kujifunza kutoka kwa Wachaga ni kuwa; Mchaka mchaka ndio mpango mzima, na hela hailali!

Kwa hiyo wadau wa JF, kubali au kataa lkn ni wazi kuwa Wachaga ni nguvu kubwa kwenye maendeleo ya Tanzania.
 
Nauza anti- jealous tablets 😹

Nimependa huu uzi
20250315_231126.jpg
 
Moshi hakuna mashamba wala sehemu kubwa za ufugaji, hivyo biashara, ndiyo njia pekee yakutoa ndiyo maana tunakuwa serous sana na biashara au kazi inayotuingizia kipato.

Nina Pub maeneo fluni hapa mjini zaidi ya ya miaka 10 Sasa...kunà watu wamefungua jirani yangu zinakufa, mpaka wengine wamejenga chuki kubwa sana
 
Back
Top Bottom