Kwanza kabisa nitoe pongezi zangu za dhati kwa namna ya kipekee ambavyo mmekuwa mkifanya kazi zenu, ni jambo jema sababu katika miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia mapinduzi makubwa katika kupashana habari mbalimbali.
Pili nitoe malalamiko yangu juu ya kitendo cha serikali/Bunge kuminya uhuru na haki ya mtanzania kupata habari kwa mujibu wa katiba ya JMT ibara 18. Tuna kila sababu ya kulaani vitendo viovu kama hivi sababu tunashindwa kujua wawakilishi wetu wanafanya nini ndani ya Bunge.
Lakini wakati jitihada zinaendelea za kutafuta ufumbuzi wa hili suala, ningeshauri yafuatayo;-
1. Fanyeni mkutano wa pamoja kama uliofanyika jana Mwanza lakini huu uwe na agenda moja ya kujadili sababu za usitishwaji wa kurusha Bunge live
2. Mualikeni Waziri mwenye dhamana ya habari awe sehemu ya huu mkutano
3.Elezeni takwa la wananchi na wakishindwa kuwasikiliza, kubalianeni kutorusha habari yoyote ya rais, waziri na mbunge wa chama tawala. Kataa kabisa ili wafanye mambo yao gizani, through this watafeel wananchi tunachokifeel na hii iwe ni makubaliano ya wote.
4. Mwandikieni Rias Barua ya kutoridhishwa na uongozi safari hii hasa katika uhuru wa habari na haki ya Mtanzania.
Naomba Kuwasilisha.