Kubadilishwa kwa sarafu ni namna mojawapo ya kuzirejesha fedha hizo kwenye mzunguko

ng'adi lawi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
2,956
1,114
Hivi sasa wafanyabiashara wakubwa wameacha kuagiza bidhaa wakiangalia kwanza hali ya uchumu itakuwaje chini ya serikali ya rais JPM.
Hii ina maana kuwa kuna fedha nyingi sana majumbani mwa watu hao.

Mimi siyo mchumi lakini nadhani kubadilishwa kwa sarafu ni namna mojawapo ya kuzirejesha fedha hizo kwenye mzunguko na pia kurekebisha sheria ya BOT ili kuthibiti matumizi ya fedha taslimu kwenye biashara.
Hivi sasa mtu unaweza kuchukua hata tzs 1bn fedha taslimu kutoka benki kwenye masanduku na masandarusi!!!!!!!!!!
Ni wakati muafaka kukataza kuchukua fedha taslimu kutoka benki na kulazimisha hundi zote zipitie kwenye akaunti za wateja au kuweka kiwango cha juu kwa mtu yeyote kuchukua fedha taslimu kutoka benki.
 
Sijaelewa kama unatuarifu kuwa sarafu ipo mbioni kubadilishwa au unatoa ushauri sarafu ibadilishwe pamoja na sheria ya BOT?

Tafadhali rudi uliweke sawa.
 
Sijaelewa kama unatuarifu kuwa sarafu ipo mbioni kubadilishwa au unatoa ushauri sarafu ibadilishwe pamoja na sheria ya BOT?

Tafadhali rudi uliweke sawa.

Ni mawazo yangu na ninaomba wachumi waje hapa kwa maoni ya kitaalamu.
 
Ili sarafu ibadilishwe lazima kuwe na kitu kinachoitwa overnight inflation,kama ilivyo dollar ya zimbabwe sasa.co kukurupuka tu kama ambavyo wewe umekurupuka kuleta hii thread hapa.
 
Ili sarafu ibadilishwe lazima kuwe na kitu kinachoitwa overnight inflation,kama ilivyo dollar ya zimbabwe sasa.co kukurupuka tu kama ambavyo wewe umekurupuka kuleta hii thread hapa.

Wewe ndiwe umekurupuka. Kuna sababu ya zaidi ya inflation ili sarafu ibadilishwe. Ninachozungumza ni kubadilisha sura ya sarafu. Kwa mfano kama fedha bandia zikiwa nyingi kwenye mzunguko, kama ikionekana kuna haja ya uboreshaji ili zidumu zaidi. Kwa maoni yangu ili fedha zinazohodhiwa majumbani zirudi kwenye mzunguko BOT wafanye marekebisho ya sheria ili wafanyabiashara wakubwa wote wafanye miamala yote mikubwa kupitia mabenki.
 
Awamu ya kwanza na Pili walikuwa na kawaida ya kubadili shilingi kila mara ilisaidia kuwaumbua wale wote wanaoficha mapesa kwenye Mahandaki majumbani mwao.
 
Back
Top Bottom