Kitope
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 236
- 58
Heshima kwa wote wakuu!, Katika kuhangiaka kwangu na ukulima sasa nimeamua moja katika mapande niliyonayo nifanye ni sehemu ya kuweka kajibanda cha watoto na wajukuu panapomajaaliwa. Kitu kimoja sina elimu nacho. naomba kwa mwenye ufahamu wa ndani anieleweshe. Kubalisha shamba kuwa plot ya kujenga ni hatua ngapi na ni zipi nipite ili kesho na keshokutwa nisije kuambia nimejenga barabarani au niambiwe niwapishe nakupoteza vijisenti hivi vya halali??. na je gharama zake kwa makadirio ni zipi?? natanguliza shukrani za dhati. Facts :- shamba lipo kigamboni, ukubwa eka sita na nusu. Ninayoyajua!!! :- kwa mujibu wa watu wanasema ita mabingwa wanapima wana weka mawe na unalipia mawe! mawe kiasi gani?? Naombeni wanaweni kwa mwenye ujuzi na hili anijuze hatua kwa hatua ya mwanzo mpaka Building permit na makadirio yake. Nashukuru sana.