SoC04 Kubadili muundo wa utawala ili kuondoa utitili wa viongozi wa umma wasiokuwa na tija katika kutatua shida za wananchi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Pendragon24

Member
Aug 8, 2018
39
66
Pamoja na ukuaji wa teknolojia lakini nchi yetu bado inakabiriwa na changamoto kubwa ya ufanisi inayosababishwa na ongezeko la kasi la viongozi na watumishi katika ofisi za umma ambao hawana tija yeyote katika kuleta ufanisi kwa wananchi ila wanaongeza mianya ya rushwa, urasimu, gharama, uvivu na uzembe kwa baadhi ya watumishi ndani ya serikali hivyo kupelekea wananchi kuchukua muda mrefu katika kutafuta suluhisho sahihi la matatizo yao shida ambayo ilitakiwa ishughulikiwe na idara moja itazungushwa kwenye idara zaidi ya mbili hivyo kupelekea jambo lililotakiwa kukamilika kwa siku moja, kwa muundo huu wa sasa jambo hilo litatumia siku tatu na zaidi.

Japo tunafahamu kwamba hatuwezi kumaliza changamoto zote za wananchi kwa siku moja lakini hali ya kujirudia rudia kwa changamoto zile zile katika maeneo mengi kila siku na kukosa mpango sahihi wa kitaifa wa kutatua changamoto zinazoweza kutatulika ndio tatizo kubwa zaidi linalosababishwa na muundo wa utawala ambao umebeba utitili wa watumishi wa umma bila kuwa na tija yeyote kwa wananchi.

Wapo viongozi wa umma ambao kwa maslai yao binafsi wameshindwa kutatua changamoto za wananchi kwa usahihi ingawa sera, kanuni, sheria na miongozo ya namna ya kutatua changamoto hizo ipo badala yake watumishi wa umma wamekuwa ndio chanzo kikubwa cha kuzalisha na kuendeleza migogoro mingi iliyopo kati ya wananchi. katika nyakati tofauti tumeshuhudia migogoro na mifarakano baina ya watumishi ndani ya wizara, halmashauri na hata mikoani.

Kutokana na utitili wa watumishi wa umma katika muundo wa utawala kuongeza urasimu katika kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi kwa haraka, wananchi wengi wamekuwa wakisubiri ziara na ujio wa viongozi wa kitaifa kama vile waziri mkuu au Raisi ili waeleze changamoto zao wakati waziri husika yupo,mkuu wa mkoa yupo,katibu tawala yupo mkuu wa wilaya yupo mkurugenzi na maafisa wa serikali za mitaa na kata wapo. sasa kama hali ndivyo hivi ilivyo kuna haja gani ya kuwa na utitili wa viongozi hawa wote katika muundo wa utawala?

CHINUA ACHEBE alisema The trouble with Nigeria is poor Leadership, lakini hapa kwetu shida si tu uongozi pekee lakini hata muundo wa utawala ambao unatumika ni changamoto kubwa kwa sababu muundo huo umetengeneza uzembe,ukiukwaji wa haki za binadamu, rushwa, uchawa, gharama kubwa na kupunguza ufanisi katika kutatua matatizo ya wananchi kwa usahihi.

Muundo wa utawala wa watumishi wa umma unapelekea mapato mengi yanayokusanywa na serikali kwenda kugharamia uendeshaji wa shuguli za ofisi za serikali kuliko kuwekeza katika kuboresha zaidi huduma za maendeleo kwa wananchi. Haiwekezani kilimo kinachangia asilimia 26.5 katika pato la taifa lakini ushuru wa mazao,pembejeo pamoja na zana nyingine za kilimo bado ni janga kubwa kwa wakulima.
source Masoud kipanya

Ndio maana serikali inawatwika wananchi mizigo mikubwa ya kodi, makato, ushuru, adhabu kali na malipo mengine katika huduma za jamii kwa lengo la kukusanya mapato ya kutoshea kuhudumia shughuli za ofisi za serikali zilizokithiri utitili wa watumishi wasiyo na tija yeyote kwa wananchi. Ndio maana pamoja na utitili wa watumishi katika muundo wa utawala wa mamlaka ya bandari Tanzania TPA pamoja na mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi UDART wameshindwa kuleta ufanisi kwa wananchi badala yake kutafuta wawekezaji.


Kama suluhisho la haraka halitapatikana katika kupunguza utitili wa viongozi wa umma kwa miaka 25 ijayo kuna uwezekano mkubwa wa ongezeko la umasikini na uhuru wa watu kumezwa kiuchumi na utitili wa watumishi wa umma waliopo kuanzia ngazi ya kitongoji mpaka serikali kuu wanaoishi kifahari kwa kodi za wananchi ambazo zilitakiwa kuboresha huduma za jamii.​

Picture02.jpeg

TANZANIA TUITAKAYO ni ya muundo mpya wa utawala utakaokuwa na viongozi wachache watakaosaidiwa na mifumo ya kidigitali katika kuwahudumia wananchi. Hizi ni baadhi tu ya njia za namna ya kubadili muundo wa utawala,​
  • Nafasi za kisiasa katika serikali za mtaa na mabaraza ya kata kama hazina mamlaka kamili ya kutatua shida za wananchi kwa kukwepa lawama kama vile mwenyekiti wa mtaa na madiwani wa viti maalumu zinapaswa kuondolewa.​
  • Kuhamasisha vituo jumuishi vya kutoa huduma kwa jamii ngazi ya tarafa vitakavyosaidiwa na mifumo ya kiteknolojia hasa katika miji na majiji.​
  • Kuunganishwa kwa kata kuanzia tatu na zaidi kulingana na eneo husika ili kupata diwani mmoja atakayewakilisha kata hizo au pawepo na diwani wa tarafa.​
  • Majimbo ya uchaguzi yenye changamoto chache hasa yale yaliyopo kwenye majiji na miji yaunganishwe ili kupunguza idadi ya viti na utitili wa wabunge wasio na tija.​
  • Kupunguza idadi ya wabunge wa viti maalumu na wale wa kuteuliwa ambao hawawajibiki kutatua shida za wananchi moja kwa moja.​
  • Kuondoa utitili wa nafasi za kuteuliwa katika ngazi ya mkoa na wilaya na kuunganisha baadhi ya Idara zake ambazo majukumu yake ni machache na hayawagusi wananchi moja kwa moja.​
  • Kuondoa nafasi za naibu mawaziri na naibu katibu mkuu kwani majukumu yalipo sasa mawaziri na makatibu wakudumu (permanet secretary) wanamudu ipasavyo hii itapunguza hata mifarakano iliyopo wizarani.​
  • Kuunganisha wizara ambazo zina majukumu machache kama vile wizara ya madini, wizara ya maendeleo ya jamii, muungano na mazingira.wizara ya utamaduni,Sanaa na michezo​
  • Kuondoa vyeo vya kubuni ambavyo havipo kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi kama vile waziri wa nchi,ofisi ya Raisi, ikulu (kazi maalumu) na naibu waziri mkuu.​
  • Kuunganisha baadhi ya wizara ambazo haziendi kuhudumia shida za wananchi moja kwa moja kama vile wizara ya fedha pamoja na wizara ya mipango na uwekezaji, wizara ya katiba na sheria pamoja na wizara ya utumishi na utawala bora.​
  • Kuunganisha wizara iliyopo chini ya ofisi ya makamu wa raisi na wizara iliyopo ofisi ya waziri mkuu hata baadhi ya wizara zilizopo chini ya ofisi ya Raisi zenye majukumu machache.​
  • Kubadili uakilishi wa mabalozi badala ya kila nchi sasa tuwe na uwakilishi wa mabalozi kwa kanda kama vile ECOWAS, SADC, EAC, EU,Asia na nchi za Amerika ya kusini kutegemea na kanda husika ilivyo.​
Mwisho TANZANIA TUITAKAYO ni ya muundo wa utawala wenye kuleta tija kwa watu ambao utatambulika ndani ya katiba, sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya nchi ili kila kiongozi wa umma aufuate huo sio kutengeneza nafasi na vyeo vya ajabu ajabu ili kuweka ndugu na marafiki katika ofisi za umma.​
 
Kutokana na utitili wa watumishi wa umma katika muundo wa utawala kuongeza urasimu katika kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi kwa haraka, wananchi wengi wamekuwa wakisubiri ziara na ujio wa viongozi wa kitaifa kama vile waziri mkuu au Raisi ili waeleze changamoto zao wakati waziri husika yupo,mkuu wa mkoa yupo,katibu tawala yupo mkuu wa wilaya yupo mkurugenzi na maafisa wa serikali za mitaa na kata wapo. sasa kama hali ndivyo hivi ilivyo kuna haja gani ya kuwa na utitili wa viongozi hawa wote katika muundo wa utawala?
Ilipaswa kama litatatuliwa jambo ambalo lilikuwa ndani ya uwezo wa kiongozi aliyepo na hakuwajibika, basi awajibishwe.

Na huyo mwananchi anayevizia kiongozi wa serikali ndio awasilishe shida kama alipaswa kuipeleka kwenye taratibu zilizopo naye awajibishwe🏃.!!

uhudumia shughuli za ofisi za serikali zilizokithiri utitili wa watumishi wasiyo na tija yeyote kwa wananchi.
Umerudia mara kadhaa kuwa hawana tija, hawana tija, ni kama unajumuisha sana (overgeneralization) mengine ya ufanisi na urasimu na rushwa yanaweza kujipenyeza na kiasi maana penye wengi pana mengi lakini bro ndio bila tija kabisa? Yeyote kabsaa!??

Tunahitaji mifumo na watu pia. Tukiwekeza kwenye ubora wa hivyo vyote nadhani tutatoboa tu
 
Back
Top Bottom