Tuanzie kwanza ana ufaulu gani huyo mwanao, pili alichagua combinations zipi kwenye mtiririko. Yani PCB ilikuwa ya ngapi na HKL ilikuwa ya ngapi. Pia tujue ana ufaulu gani kwenye hayo masomo matatu ya PCB.
Baada ya hapo utalinganisha na shule aliyosoma ufaulu wao ukoje, kama alisoma shule nzuri na ana ufaulu wa kawaida asiende PCB atazunguka na kurudi diploma. Kama shule ufaulu wa kawaida alijipambania kwa uwezo binafsi, anaweza pambana kwa nguvu kubwa A level na comb. hiyo.
HKL sio ya kusoma kama hana nia nayo, akishindwa options zote bora aende diploma, nusu ya nguvu ya kusoma PCB anaiweka uko anatoka na GPA ya 3.5+ na kwenda Degree kwa kuchelewa mwaka mmoja ila kwa uhakika.