Kuanzisha na kusimamia Biashara ya kupanga na kuboresha ndani ya Nyumba

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Kupangilia nyumba (hoteli, benki, loji, resoti, shule, chuo, majengo ya biashara na kadhalika) ni moja ya biashara zinazolipa kiasi kikubwa cha faida katika miji mikubwa.

Kupamba nyumba ni moja ya aina ya ukarabati usio wa lazima
kuufanya, lakini huongeza thamani kama ilivyo kwenye bustani ya
nyumbani. Kupamba nyumba ni moja ya njia ya kuongeza kiasi cha
kodi ya pango la nyumba yako kwa sababu huongeza thamani ya
nyumba unayopangisha.

Kupamba nyumba ni moja ya eneo ambalo watu hubobea ili kuingiza kipato cha kila mwezi. Wewe pia unaweza
kubobea katika eneo hili na ukajiongezea kipato maradufu.

Kuboresha nyumba ni hatua muhimu sana katika nyakati zifuatazo;-

✓ Kabla ya kuipangisha nyumba yako.

✓ Kabla ya kutangaza kuuza nyumba yako.

✓ Kabla ya kuombea mkopo wa majengo kwa ajili ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

✓ Kabla ya kulipia bima ya majengo.

Upambaji wa nyumba husaidia mambo yafuatayo;-

Moja; kuongeza ubora wa nyumba ya mteja wako. Anayeishi kwenye
nyumba iliyopambwa huonekana bora hata katika muonekano wake
kwa sababu ya ndani ya nyumba anayoishi ina mvuto.

Mbili; huongeza hamasa ya kufanya kazi katika nyumba au chumba kikichopambwa. Ukiwa na ofisi iliyopambwa utaweza kufanya kazi
kwa muda mrefu kuliko kama ingekuwa unafanya kazi kwenye ofisi
chafu, yenye mpangilio mbaya na harufu mbaya.

Tatu; huongeza ubora wa huduma au uuzaji wa bidhaa mbalimbali. Hasa
kama chumba au nyumba inatumika kwa ajili ya kufanyia biashara za
huduma au biashara za huduma.

Changamoto Kuboresha Nyumba

Moja; hugharimu pesa. Ili kupamba nyumba yako ya kupangisha huhitaji
kutoa pesa kutoka kwenye vyanzo vingine vya kipato chake. Hivyo utahitaji kiasi cha mteja fedha ili kuweza kupamba nyumba yako. Na
utahitaji kuandaa bajeti ya kupamba nyumba yako kila baada ya miezi
kadhaa.

Mbili; inaweza kuifanya nyumba ikose wateja au uchelewe kupata wanunuzi wa nyumba uliyopamba. Hii hutokea sana endapo nyumba umeipamba kupitiliza na kutumia matilio ya gharama kubwa.

Jinsi Ya Kuanza Kupamba Nyumba.

Unaweza kuunganisha huduma za kupamba nyumba na huduma za
kutengeneza na kupanda bustani katika nyumba za wateja wako.

Unaweza kuanza kwa kuchagua moja ya njia zifuatazo;-

(a) Kuanza bila kuwa na kampuni la kupamba nyumba.

Njia hii hufaa zaidi kwa makundi yafuatayo ya wafanyabishara;-

✓ Watu ambao wana kiasi kidogo cha mteja fedha kwa ajili
ya huduma za upambaji wa nyumba au bustani za maua kwenye
nyumba.

✓ Watu ambao ndio wanaanza kazi za kupamba nyumba na hawana
mtandao wa watu wenye uzoefu kwenye kazi za upambaji nyumba.

✓ Watu ambao wana muda wa kutosha kufanya kazi za upambaji
nyumba wakiwemo waajiriwa katika taasisi binafsi na taasisi za
umma.

✓ Watu ambao hawana uhakika juu ya ubunifu wao. Hii ni kwa
sababu kazi hii huhitaji ubunifu mkubwa sana.

(b) Kuanza kwa kumiliki kampuni ya upambaji wa nyumba na bustani za maua kwenye nyumba.

Njia ya aina hii inawafaa kwa watu ambao wana sifa zifuatazo;-

✓ Watu ambao wapo tayari kusimamia waajiriwa. Kazi hii itahitaji
uwe na wanatimu wabunifu na nadhifu.

✓ Mtu ambaye ana mtaji fedha kwa ajili ya kuanzisha, kusimamia na
kukuza biashara ya huduma ya upambaji wa nyumba.

✓ Mtu ambaye ana maarifa na uzoefu kuhusu upambaji wa nyumba.

Au mtu ambaye ameajiri mtu mwenye uzoefu na maarifa sahihi
kuhusu upambaji wa nyumba.

Sio lazima utengeneze pesa kwa kutumia njia hii. Kuna njia nyingine
nyingi za kutengeneza pesa kwenye ardhi na nyumba.

Njia nyingine ambazo unaweza kutengeneza pesa kwenye ardhi na
nyumba ni kama ifuatavyo;-

✓ Kumiliki, kukarabati na kupangisha nyumba. Kupangisha nyumba
ni moja ya njia ya kufikia uhuru wa kifedha kupitia ardhi na nyumba.
Wengi wa wawekezaji ambao wamefikia uhuru wa kifedha
waliwekeza kiasi kikubwa cha mtaji fedha wao kwenye majengo ya
kupangisha.

✓ Kununua, kukarabati na kuuza nyumba ndani ya mwaka mmoja.

✓ Kununua nyumba na kisha kuuza nyumba kwa kupangisha nyumba
hiyo.

✓ Kuwekeza kwenye ardhi na nyumba kwa kuingia ubia.

✓ Kufanya kazi ya uwakala au udalali wa ardhi na nyumba. Hii ni kazi ambayo inahitaji uvumilivu na uaminifu ili kupata mafanikio makubwa sana.

Kwa miaka ya hivi karibuni, ukiwa ni dalali au wakala wa ardhi na
nyumba na hutumii mitandao ya kijamii kuwafikia wateja.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mawasiliano; +255 752 413 711
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom