Kuadhimisha Siku Ya Saratani Duniani [4 Februari 2016]

Je Upo Tayari kuja kufanya uchunguzi wa Saratani ya;

  • 1. Tezi Dume

    Votes: 0 0.0%
  • 2. Saratani ya Koo

    Votes: 0 0.0%
  • 3. Saratani ya Shingo ya Kizazi

    Votes: 0 0.0%
  • 4. Saratani ya Matiti

    Votes: 0 0.0%
  • 5. Saratani nyenginezo

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    0

Orcitz

Member
Aug 28, 2015
8
5
Siku ya Saratani huadhimishwa duniani kote tarehe 4 Februari ya kila mwaka katika taratibu ambazo huunganisha azma ya dunia nzima katika kupambana na tatizo linalokua la ugonjwa wa saratani. Siku hii ya Saratani imeendelea kuwa siku muhimu kwetu sote, ikiadhimishwa miaka mitano baada ya utiwaji saini azimio la umoja wa mataifa la mwaka 2011 lililohusu kusaidia upatikanaji wa kinga na kuzuia ukuaji wa magonjwa yasiyo ambukiza (NCD’s) ikwemo ugonjwa wa Saratani.

Kauli mbiu ya siku ya Saratani Duniani kwa mwaka 2016 ni “Tunaweza, Ninaweza. Binafsi au Sote kwa Pamoja tunavyoweza kutekeleza wajibu wetu wa kupunguza janga la Saratani Duniani.”. Hii ina maana kuwa, kama watu binafsi, mashirika wakishirikiana Pamoja na Serikali kusaidia jitihada za kupambana na Saratani, tutaweza kutibu, kuponya na kupunguza idadi ya vifo vya Saratani kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2025.

Katika kuadhimisha siku ya Saratani Duniani hapo Tarehe 4 Februari 2016, Taasisi ya Saratani Ocean Road itafanya yafuatayo;

1. Kufanya uchunguzi wa Saratani kwa wananchi watakaojitokeza kwenye kliniki za uchunguzi hospitalini hapo. Uchunguzi utakaofanyika ni wa
Saratani ya Tezi Dume kwa wanaume, Saratani ya Shingo ya Kizazi na Saratani ya matiti kwa wanawake; na saratani ya ngozi kwa wanaoishi na Albinism. Uchunguzi huu utafanyika bure bila ya malipo yoyote

2. Kuandaa Warsha na waandishi wa habari kuhusu madhara ya Tumbaku na njia za kupambana na matumizi ya Tumbaku.

Karibuni

Cancer 1.png



cancer 2.png
 
Saratani, a deadly and most neglected Disease. I wonder when people will wake up
 
Back
Top Bottom