Ndugu wana Jamii
Chuo cha ufundi Arusha kilipata mamlaka ya kujitawala chenyewe kupitia tangazo la Serikali la Machi, 2007. Chuo cha Ufundi Arusha kiko chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Kwa mamlaka Chuo kiliyopewa, kilipelekea Chuo kupata Mkuu mpya wa kuendesha shughuli za Chuo. Hivyo mwezi Septemba, 2009 Chuo kilipata Mkuu mpya wa Chuo. Mkuu huyu wa Chuo anaitwa Eng. Dr. Richard J. Masika. Kitaaluma ni mtaalamu wa fani/mambo ya ujenzi hasa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji. Mkuu huyu alitokea Dar es salaam. Alikuwa akifanya kazi Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam (DIT) kama mkurugenzi wa mafunzo, (Director of Studies). Tangu Mkuu huyu afike chuoni kufanya kazi, Chuo kimejikuta kikiendeshwa katika hali ya ajabu na isiyofuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kisheria.Mshahara wa Mkuu wa Chuo
Mkuu wa Chuo ana cheo cha Senior Lecturer. Cheo hiki kina ngazi ya mshahara PHTS 13-14. Kwa kudhania kwamba mkuu wa chuo ameandika machapisho kadhaa jambo ambalo halina uhakika, ichukuliwe kuwa anayo sifa hiyo na hivyo akawa PHTS 14. Kwa ngazi hito Mkuu wa Chuo alipaswa kulipwa Tsh 3,903,400/= kulingana na muundo wa mishahara ya Taasisi zilizoko chini ya Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa mwaka wa fedha 2011/12. Kinyume chake Mkuu wa chuo alilipwa Tsh. 4,303,400/= ngazi ya PHTS 16 ambayo ni ngazi ya Profesa kamili (Full Professor) katika kipindi hicho cha mwaka wa fedha 2011/12. Mshahara huu wa ziada umeanza kulipwa tangu 2010, kulingana na barua ya maombi ya marekebisho ya 29/02/2010.Ufisadi wa Fedha za Mafunzo ViwandaniKutokana na taarifa za uhakika kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Chuo cha Ufundi Arusha kilipewa fedha ya Mafunzo viwandani jumla ya Tsh 559,860,000/=. Fedha hizi zilitengwa kwenye Kijifungu 220800 kasma 220807 Tsh. 505,680,000 na Kijifungu 221000 kasma 221002 Tsh. 54, 180,000/=. Fedha hizi zilikusudiwa kuwalipa wanafunzi 903 kwenda mafunzo viwandani pamoja na waalimu 95 kwenda kuwakagua viwandani katika kipindi cha Mwezi wa Mei na Juni 2013. Matumizi ya fedha hizi hayakwenda kulingana na maombi ya fedha husika. Kulingana na idadi ya wanafunzi na waalimu waliolipwa haikulingana na kiasi kilichoombwa. Haijulikani kiasi cha fedha zaidi ya Tsh 35,000,000 ziko wapi au zilifanya nini na kwanini. Uwakilishi wa Wanataaluma kwenye Bidi ya ChuoSheria iliyoanzisha Chuo cha Ufundi Arusha ya Machi 2007 inatamka wazi kuwa kutakuwa na mwakilishi wa wanataaluma kwenye Bodi ya Chuo. Sheria hii ni sawa kabisa na sheria za Vyuo vingine vya elimu ya juu. Tofauti na inavyotakiwa kisheria na kinyume na uzoefu kwenye vyuo vingine, kwenye Bodi ya Chuo kuna Makamu wa Mkuu wa Chuo. Hakuna anayejua ni sheria gani, kigezo gani au ni hekima gani inamwongoza Mkuu wa Chuo kumweka Msaidizi wake kwenye Bodi tofauti na inavyotakiwa kisheria. Haijulikani pia kwamba ni mpaka nini kitokee ndipo Mkuu wa Chuo ajue kuwa anahitajika kuongoza kwa kufuata sheria na utawala bora? Je Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha yuko juu ya Sheria?Matumizi mabaya ya madarakaKutokana na kukosa uwakilishi kwa watumishi na hasa wanataaluma kwenye vyombo mbalimbali vya maamuzi chuoni hasa kwenye Bodi ya Chuo, Mkuu wa Chuo anatumia mwanya huo kutumia fedha za Chuo Vibaya. Amekuwa akitumia mwanya huo kuajiri watumishi anaotaka, anatoa kadharasi za upendeleo kwa mkandarasi mmoja wa nyumbani kwao kupitia Bodi ya Zabuni ambayo wajumbe wake ni wakuu wa Idara ambao wameteuliwa na Mkuu wa Chuo. Anatumia anavyojisikia fedha za uzalishaji mali zinazowekwa kwenye akaunti iliyoko katika benki ya CRDB.