Yote aliyafanya ni part of the game,hivyo hivyo hata kwenye Utawala wa demokrasia watu wanauwawa sana na watawala kwa kutumia kigezo hicho hicho cha demkrasia utofauti ni kuwa huyu anakuua huku anacheka na huyu anakuua akiwa amenuna.
KUABUDU MTU NA MATOKEO YAKE!
FEBRUARI 25, 1956, Katibu Mkuu wa Chama cha Komunisti, Nikita Krushchev, alitoa hotuba maarufu iliyoitwa “The Personality Cult and Its Consequences” – “Kuabudu Mtu na Matokeo Yake". Pia huitwa “Hotuba ya Siri.”
Ukumbi wa Great Kremlin, Moscow, Urusi, ukiwa na jopo la wajumbe 1,500 kutoka nchi za Umoja wa Sovieti, pamoja na mamia ya wageni waalikwa, walinyamaza kimya kwa saa 4 (dakika 240), wakimsikiliza Krushchev akitema nyongo.
Sio tu kwamba wajumbe na wageni waalikwa walinyamaza, bali pia walishindwa hata kugeuza shingo kutazamana wao kwa wao. Wote macho yao yalikuwa pima kumtazama Krushchev, kwa hofu kubwa. Krushchev aliamua kuvaa mabomu kuusema ukweli ulioogopwa na wengi.
Krushchev alitoa hotuba hiyo ikiwa ni miaka mitatu kasoro siku tisa tangu kifo cha aliyekuwa Mtawala wa Sovieti, Joseph Stalin kilichotokea Machi 5, 1953. Tangu kufa kwa Stalin, hakuna lolote baya lililotamkwa kuhusu kiongozi huyo ndani ya Sovieti.
Viongozi waliofuata baada ya Stalin, walipitia kipindi kigumu kwa kila walichofanya. Maana walipimwa kwa utendaji wa Stalin. Ndani ya Urusi na Sovieti yote, Stalin alitukuzwa mithili ya Mungu mtu.
Tangu kufa kwa Stalin, Komunisti hawakuwa wamefanya Mkutano Mkuu mpaka Februari 14, 1956. Mkutano huo ulichukua siku 11. Ndipo wakati wa hotuba yake ya kufunga mkutano, Krushchev akaamua kuwaambia watendaji wakuu wa chama na Serikali za Sovieti unyama wote uliofanywa na Stalin.
Krushchev alisema, Stalin aliua watu wengi, wapinzani wake, watiifu wa chama pamoja na kutekeleza unyama mwingine wa kila aina, na hayo ni matokeo ya kumtukuza mno na kumwabudu kama Mungu.
Baada ya hapo, Krushchev alimtangaza Stalin kama mtu mwovu. Kumbukumbu mbalimbali za Stalin zilianza kuondolewa. Stalin alipokufa mwili wake haukuzikwa, ulihifadhiwa jirani na Kiongozi wa zamani Sovieti na Chama cha Komunisti, Vladimir Lenin, ndani ya jumba la Makumbusho la Lenin.
Mwaka 1961, katika kuhakikisha kumbukumbu za Stalin zinafutwa na haadhimishwi, mwili wake uliondolewa kwenye Jumba la Makumbusho la Lenin, ukazikwa makaburi ya Kremlin Wall kama mtu wa kawaida. Lenin ndiye pekee mwili wake umetunzwa mpaka leo.
SOMO: Madikteta huwa na sumu ya ajabu sana kwa umma. Hutokea kupendwa na kuabudiwa licha ya kufanya unyama mwingi. Kuna wanaomuenzi Mobutu Sese Seko, wapo wanaosema Idi Amin alikuwa kiongozi mzuri. Hata Adolf Hitler anaenziwa. Katika utawala wake, Stalin anahusishwa moja kwa moja na vifo vya watu wanaofikia 20 milioni.
Ndimi Luqman MALOTO
Nitajie 10 tu uje kuchukua mbuzi wa IDD! Jinga weweYohana wa Chattle ndye Dictator pekee kwa Africa aliyeua watu wengi na kupora mali nyingi sana!
Tuwekee uthibitisho wa watu aliowaua na mali alizopora.Yohana wa Chattle ndye Dictator pekee kwa Africa aliyeua watu wengi na kupora mali nyingi sana!
Wewe ndio umemuelewa mleta mada 🤣 🤣 🤣Sasa unataka kutuambia nini kuhusu Stalin na Bongo yetu??---- nani alikuwa Stalin wa Bongo??
Maneno yako kama usingetumia neno dikteta upo sahihi !! Paragraph ya kwanza na ya pili ni sahihi ila paragraph ya tatu kidogo nimeona ina ukakasi !! Watu wa tabaka la chini siku zote humpenda kiongozi anayewajali na vigezo wanavyovitumia huwa wanavijua wenyewe kwamba ni kwa sababu gani wamempenda !! Masuala ya kusema anauwa watu au anateka watu au amewabana wapinzani Mara nyingi kwao huwa sio issue kubwa sana !! Wao huwa wanajali vitu vinavyowahusu wao direct sio indirect !!Niliona mahala wanasema madikteta hueshimiwa kwasababu hujiweka karibu na tabaka la watu wa chini wakati wa utawala wao.
Naamini wengi wao hufanya hivyo wakiamini tawala zilizowatangulia hazikuwa zikiwajali watu hao. Mfano wa hili utaupata hapa kwetu wakati wa awamu ya nne namna wachache walivyokuwa wakifaidi keki ya taifa.
Japo yule wa kwetu aliitwa "uchwara" kumaanisha kwamba hakuwa dikteta kamili kama walivyokuwa kina Iddi Amin na wengine, huyu wetu alilenga kuwamaliza wale tu aliowaona wanamsumbua kwenye utawala wake, zaidi wakiwa wapinzani.
Magufuli tumeishafuta historia yakeKUABUDU MTU NA MATOKEO YAKE!