Ku refill catrage za Hp printer LaserJet M1132 MFP

Ngosi

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2011
Posts
391
Reaction score
191
Habari wanajamvi
Naomba kujua ni wino upi ni bora ku refill catrage maana awali ilikua ni ki refill unakuwa fresh ila baada ya kununua catrage mpya na ilipo isha niki refill ina faint sana yaani uki print maandishi yanaonekana kwa mbaali. Wino naotumia ni Kiyo wa kopo dogo gram 60
Msaada tafadhali
 
nunua ule wa pakti ya1kg na pengine umekosea kurefill mfano ukiacha uchafu lazima drum ipunguze ufanisi.
 
Ahsante!
Nitakupa feedback
 
nunua ule wa pakti ya1kg na pengine umekosea kurefill mfano ukiacha uchafu lazima drum ipunguze ufanisi.

Mkuu wino unapatikanaje? Na je kuRefill 85A, 80A, 75A. Wino unaotumika ni mmoja au wino unayofautiana?
 
kwa kurefill wino inayotumika kwenye 85A hauna tofauti na hizo zingne tena hata ile cartridge ya Canon ndogo hutumia wino huo huo. Kinachotakiwa ni usafi wa drum ukihakikisha unafungua na kumwaga wino mchafu uliobaki kabla ya kuweka mwingne mpya na zingatia usiishike shike drum au kuifuta kwa kitambaa kigumu husababisha michubuko yenye kupelekea kupunguza ufanisi wake
 
namna ya kuupata wino nenda pale kkoo mtaa wa uhuru karibu na msikiti kuna duka la wasomali flani hivi au nenda mbele utakuta mtaa mwingne unaotokea barabara ya mnazi mmoja nenda kushoto km unaifuata barabara ya mnazi mmoja kuna maduka mengi ya stationery uliza 85A na km unataka wa bei poa unasema naomba 85A namba mbili watakuelewa unamaanisha nn. Eidha kwa wino wa kurefill sema nataka Kiyo ndogo
 
Nauza toner na ink(toner kwa ajili ya laserjet na ink kwa ajili ya inkjet au deskjet au vilevile officejet), Toner za HP Tshs. 15,000/= wino una ujazo wa grams 140.
Kama huwezi kujaza nitakujazia kwa Tshs. 20,000/=
 
Nauza toner na ink(toner kwa ajili ya laserjet na ink kwa ajili ya inkjet au deskjet au vilevile officejet), Toner za HP Tshs. 15,000/= wino una ujazo wa grams 140.
Kama huwezi kujaza nitakujazia kwa Tshs. 20,000/=
Mkuu una Toner za printer aina ya Brother HL 2040?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…