Krismas mbaya kwa Kikwete

Sijawahi ona Mashehe wakikemea serikali ya Kikwete kazi yao ni kusifia tu au wao wanaona maisha ni mswano tu.
 
wakuu... mimi nadhani madai kama ya katiba ni haki kwa kila asasi kuwa na matakwa nayo kwani hutimiza yale malengo ya wananchi.... hivyo madhehebu kama ya dini yakidai katiba sio kuingiza dini katika siasa.... hata wanasiasa kupitia vyama vyao wanajukumu la kudai katiba... hivyo tuwe makini tunaposema au kuhoji matamko ya viongozi wa dini kudai katiba mpya.... hata wafungwa nao wanahaki ya kudai katiba hii
 
Hivi na padre Slaa naye kasemaje? watalia sana maana padre mwenzao kashindwa, na yeyote atakayeletwa na kanisa au msikiti atashindwa maana nchi hii haina dini.
 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) Zakaria Kakobe alisema tathmini zilizofanywa baada ya uchaguzi mkuu hazikuwa za haki.
Kakobe alisema tathmini hizo zililenga kumjenga mgombea wa chama tawala ambaye anadai hakustahili kupewa haki hiyo.

Akaongeza:"Chanzo cha machafuko ni inapofikia mtu amepewa haki isiyokuwa yake na yule anayestahili haki hiyo akanyimwa,".

"Jamii inatakiwa kuondokana na fikra potofu za chama kimoja kushika hatama ya uongozi, huo ni ukale, na hiki ni kizazi kingine," alisema Kakobe.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Katoliki, Mwashamu Kadinali Pengo,
Alisema yeyote anayehubiri amani, lazima kwanza awe na amani moyoni mwake na suala la kuleta ama kulinda amani ni jukumu la kila mtu na haiwezi kuletwa na viongozi au mataifa makubwa kama ambavyo baadhi ya watu wanafikiria.

"Amani haiji kwa mabavu bali kwa paji la Mwenyenzi Mungu, amani haitegemei wenye mamlaka bali ni kila mmoja wetu bila kujali mali zetu, ilimradi tumtumikie bwana na kutenda mema.


Chanzo: Gazeti la Mwananchi.[/QUOTE]

Maaskofu inabidi waendelee kuisema vizuri uongozi wa nchi hii hasa kipindi hiki, kuna dalili mbaya sana ya UDINI katika nchi hii, hasa kuanzia kipindi cha awamu ya nne. Serikali ya awamu hii inajifanya ya kiitelijensia zaidi wakati hakuna lolote la maana zaidi ya UDINI tunaoushuhudia sasa...
Kikwete na serikali yako badilini mwelekeo tuijenge nchi..
merry x-mass😛arty:
 
ni kweli mkuu, lakini lazima ujue kuwa kumtukana mtu si lazima unchagulie tusi, maana yake ni kuwa wao wameshafikisha ujumbe, mtoto wa samaki ni samaki pia wala hawezi kuwa tumbiri
 

Kwa urais wa kuchakachua jk hatakuja apate amani kamwe. Atasemwa mpaka siku ya mwisho.
 
Wasaidizi kama hawafanyi kazi kama inavyotakiwa anaweza kabisa kuwafukuza. Tangu aingie madarakani 2005 ni wasaidizi wangapi ambao amewafukuza kufuatia malalamiko mbali mbali kutoka kwa Watanzania? Alishawahi kutamka kelele za mpangaji........
 
Wala simlaumu jk. Wengine mlimchagua, na alioochakachua matokeo mkamuunga mkono. Alipoambiwa aende kwenye mdahalo wa wagombea akakataa, nyie hamkushtuka kwamba Hana hata uwezo wa kujenga hoja na mtoto wa darasa la ratu. Hajui hata kuwasha komputa nyie mko bize mtandaoni mnamjadili. Kila siku hutoa mifano kwamba anatazama tv, kwa sababu inamruhusu akae kizembe na kuchekacheka.

Endelea jk, kula bata na kupiga misele. Wapambe wako wakipeleka nchi machafukoni haikuhusu. After all, wao ndio wamekuweka madarakani wakijua huna uwezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…