Kova achunguzwe, gorofa analojenga Ilala pesa alipata wapi?

Warangi huwa ni wabahili sana. Sioni ajabu kujenga ghorofa.
Ila nakumbuka aliyekuwa mbunge wa Kondoa Mustafa Nyang'anyi naye aliwahi kuulizwa bungeni miaka ya 80s kuwa yeye kama waziri mshahara wake ni elfu 40, pesa za kujenga nyumba kama ikulu alipata wapi? Nakumbuka swali hili liliulizwa bungeni na Christopher Nandonde.
 
Kwa hiyo unahalalisha ufisadi sio kwa kuwa hata humu wamo?? Hii nchi machizi mko wengi sana. Kwa mshahara wa polisi jinsi ulivyo Kova hajafikisha hata mshahara wa 2M, leo utudanganye anakopesheka kwa 500M unatuona wajinga eeeh. Tunaelewa ili ukopesheke lazima uwe na collaterals na uwezo wa kulipa sio tu kila mtu anakopesheka na kwa bongo cheo cha kova hakimfanyi apate mkopo zaidi ya hutu tumikopo tudogo twa up to 20M. Ingekuwa nchi hii inafuatA utawala wa sheria tungemchunguza Kova na kuangalia kodi anazolipa TRA kwa mwaka na kuhusisha na kipato chake na jengo. Kila kipato halali kinatakiwa kuendana na kodi halali. But CCM hawafanyi hivyo kulinda mfumo fisadi wanaonufaika nao

Hapo nilipo-bold nakupa like maana hutu tumikopo twa up to 20m ndio nilikuwa namaanisha ukitushika unaanzisha business in future utakuwa na hela za kufanya mambo makubwa ila wewe umeangalia zaidi kuchukua mkopo kwenda kujenga nyumba utarudishaje sasa?maana siku zote tunaambiwa mikopo tuchukue tufanyie biashara kwa sie watu wa kawaida. Kuhusu kufanya uchunguzi hiyo ni sawa tu kama vile awamu ya kwanza ya uongozi ilivyokuwa inafanya kuwana viongozi na wananchi wa kawaida japokuwa kuna ambao walionewa lakini mwisho wa siku taifa lilikuwa linanidhamu mtu akijenga nyumba au kununua gari au Tv lazima aonyeshe source of fund
 
huyu kamanda wa Polisi wa kanda Maalum Dsm naye ni fisadi tu. Anaporomosha gorofa pale Ilala makutano ya Pangani na Morogoro Streets karibu na Mahakama ya Mwanzo.

Tetesi zilizowahi kuzagaa ni kwamba alipata pesa nyingi akiwa Mbeya alipokuwa akiruhusu mihadarati kupitishwa na hata kutuma askari kusindikiza au kupokea magari yaliyobeba sheheni hiyo.

Hilo gorofa inasemekana ni la shemeji yake, wengine wanasema ni swahiba tu aitwaye Issa, au maarufu Mister Kep. Wote hawa kwao Kondoa.

Hivyo ili aendelee kula matunda juu ya migongo ya Watanzania masikini, serikali inamuach tu, kwani analipa fadhila kwa kufunika madudu mengi tu ya wakubwa hapa jijini, zikiwemo kashfa zao za ngono, za traffic accidents na hata za mauaji.

Nyingine ni kama hii ya sasa ya Dr Ulimboka -- ni lazime aitetee serikali na timu ya uchunguzi aliosema ameunda kuchunguza itakuwa ni ya magumashi tu.

Haijakaa vizuri, kama ni chuki binafsi vile! Kwani wewe inakuhusu nini ghorofa lake!! Au hata kama sio lake.... Au tupatie details za uhakika badala ya kubahatisha...
 
Kama anajenga nchini humu safi tu simwekezaji wa ndani bwana.Anatakiwa hata akistaafu awe amekaa vizuri bwana sio wa kuchekwa mtaani
 
Warangi huwa ni wabahili sana. Sioni ajabu kujenga ghorofa.
Ila nakumbuka aliyekuwa mbunge wa Kondoa Mustafa Nyang'anyi naye aliwahi kuulizwa bungeni miaka ya 80s kuwa yeye kama waziri mshahara wake ni elfu 40, pesa za kujenga nyumba kama ikulu alipata wapi? Nakumbuka swali hili liliulizwa bungeni na Christopher Nandonde.
Eee kumbe umekula chumvi nyingi.
 
Siasa za Tanzania nazo zimekuwa uchwara sana siku hizi...ni mastorii tu.
 
Kama anathubutu kuwaagiza askari wake kufanya umafia hawezi kosa hela ya kujenga ghorofa maana biashara haramu yoyote inamalipo makubwa sana!
 
Hivi kwanini watu wenye tittle serikalini wakifanya kitu huwa tuna link na ufisadi? ni kweli kuna ambao kweli ni mafisadi lakini kuna ambao sio. Tatizo tumekuwa nchi ya kijamaa muda mrefu na tumesahau kwamba siku hizi mtu unaweza chukua mkopo pia na kufanya biashara huku unafanya kazi. Kama ni suala la ufisadi hata humu JF jamaa wakishuka na kufanyia uchunguzi utakuta mafisadi ni wengi, hata kama umejenga chumba na sebule kwa milioni 6 lakini wakilinganisha na kipato chako na muda uliokaa kazini unaweza kuwa ni fisadi. Ufisadi sio kwa viongozi tu hata huku uswahilini. Mtoa mada nadhani bado ana fikra kwamba unapokuwa mfanyakazi unatakiwa huishi maisha flani hivi.

abdormality yoyote ile huleta doubt na hivo watu hupenda kujua zaidi kuhusu hiyo kitu.mtu unalipwa mfano hata milioni moja tuseme with no time unajenga ghorofa ya bilioni this is not normal
 
Kama anajenga nchini humu safi tu simwekezaji wa ndani bwana.Anatakiwa hata akistaafu awe amekaa vizuri bwana sio wa kuchekwa mtaani

Watanzania wanaofanya kazi serikalini ni kama watu wanaolima shamba moja. ikwa wote mnalima sawa lakin iwachache wanaonekana wamejaza vihenge vya mazao yaleyale mnayolima huku wengine hawana hata kikapu unadhani tafsiri yake ni nini? hili si dogo walinacho hawajali sana usawa lakini wanyonge hulipenda neno holi.
 
abdormality yoyote ile huleta doubt na hivo watu hupenda kujua zaidi kuhusu hiyo kitu.mtu unalipwa mfano hata milioni moja tuseme with no time unajenga ghorofa ya bilioni this is not normal

Ni kweli mdau ila matatizo yote yametokana na system kutofanya kazi, huwezi amini mtu Janury 2012 unaweza ukawa na kipato cha kawaida lakini ikifika December 2012 mambo yako yapo juu lakini system inaona sawa, hii nadhani kwa kuwa hata hao waliopo kwenye systems ni wachakachuaji wa uchumi wa nchi na ukisema sana unaambiwa lete ushaidi kwanini kwa mambo kama haya serikali isifanye kazi badala ya kuwaambia watu walete ushahidi
 
Yaani Kova ana ghorofa....!!!!!!????? Si alikuwa maskini tu wakati anahamishiwa Dar...!!!???? Leteni ukweli wa picha.... na anaweza kuhojiwa...!!!! katoa wapi PESA????
 
Yaani Kova ana ghorofa....!!!!!!????? Si alikuwa maskini tu wakati anahamishiwa Dar...!!!???? Leteni ukweli wa picha.... na anaweza kuhojiwa...!!!! katoa wapi PESA????

Ni kweli Mkuu, kuna gorofa lilikuwa linajengwa kwa kasi pale Ilala karibu na Mahakama, mtaa Morogoro (Morogoro Street) na gumzo kubwa eneo hilo ni kwamba gorofa hilo la Kova ingawa anamtumia shemeji wake kutoka Kondoa. Huyu ni mfanyabiashara al;iyepewa tenda na CCM ku-import Tshirt na kofia za CCM wakati wa kampeni mwaka juzi. Nimemsahau jina lake.
 
hivi kwanini watu wenye tittle serikalini wakifanya kitu huwa tuna link na ufisadi? Ni kweli kuna ambao kweli ni mafisadi lakini kuna ambao sio. Tatizo tumekuwa nchi ya kijamaa muda mrefu na tumesahau kwamba siku hizi mtu unaweza chukua mkopo pia na kufanya biashara huku unafanya kazi. Kama ni suala la ufisadi hata humu jf jamaa wakishuka na kufanyia uchunguzi utakuta mafisadi ni wengi, hata kama umejenga chumba na sebule kwa milioni 6 lakini wakilinganisha na kipato chako na muda uliokaa kazini unaweza kuwa ni fisadi. Ufisadi sio kwa viongozi tu hata huku uswahilini. Mtoa mada nadhani bado ana fikra kwamba unapokuwa mfanyakazi unatakiwa huishi maisha flani
hivi.
wewe haikosi ni assistant supretendent of police. Sasa huoni kauli kumuhami kova ni kama una conflict of interest?
 
Hivi kwanini watu wenye tittle serikalini wakifanya kitu huwa tuna link na ufisadi? ni kweli kuna ambao kweli ni mafisadi lakini kuna ambao sio. Tatizo tumekuwa nchi ya kijamaa muda mrefu na tumesahau kwamba siku hizi mtu unaweza chukua mkopo pia na kufanya biashara huku unafanya kazi. Kama ni suala la ufisadi hata humu JF jamaa wakishuka na kufanyia uchunguzi utakuta mafisadi ni wengi, hata kama umejenga chumba na sebule kwa milioni 6 lakini wakilinganisha na kipato chako na muda uliokaa kazini unaweza kuwa ni fisadi. Ufisadi sio kwa viongozi tu hata huku uswahilini. Mtoa mada nadhani bado ana fikra kwamba unapokuwa mfanyakazi unatakiwa huishi maisha flani hivi.
Mkuu usijidanganye hata nchi ya kibepari kama USA au UK ukifanya kitu beyond your capabilities lazima uchunguzwe labda una dill na drugs au nini!!! Kwa hiyo kwa Tanzania lazima tuulize maswali na yapate majibu vinginevyo huo ndio ufisadi!!!!

kwa nini asitajirike, majambazi wamekamatwa na kukutwa na pesa mil 10 kama ushaidi, zilizoibiwa ni ml150, nyingine huenda wapi?, tumekamata kilo 5 za heroin kumbe mbebaji alikuwa na 20, nyingine huenda wapi! kama sio KINO. nakwa t. kwa tumbo
 
Ni kweli mdau ila matatizo yote yametokana na system kutofanya kazi, huwezi amini mtu Janury 2012 unaweza ukawa na kipato cha kawaida lakini ikifika December 2012 mambo yako yapo juu lakini system inaona sawa, hii nadhani kwa kuwa hata hao waliopo kwenye systems ni wachakachuaji wa uchumi wa nchi na ukisema sana unaambiwa lete ushaidi kwanini kwa mambo kama haya serikali isifanye kazi badala ya kuwaambia watu walete ushahidi
Mkuu unafikiri nini kama watu waliambiwa walete fedha za wizi za EPA wasamehewe na hajaambiwa walileta kiasi gani na ninani walirudisha???? Kusamehewa kwa sheria ipi ambayo mwizi arudishe mali alizo iba asamehewe???? Nch ya ajabu sana hii (WAGAGAGIGIKOKO REP)!!

Mkuu usijidanganye hata nchi ya kibepari kama USA au UK ukifanya kitu beyond your capabilities lazima uchunguzwe labda una dill na drugs au nini!!! Kwa hiyo kwa Tanzania lazima tuulize maswali na yapate majibu vinginevyo huo ndio ufisadi!!!!

Ni kweli mdau hapa nilikuwa too general kuna mwana JF mmoja nilimjibu nilikuwa namaanisha nini
 
Back
Top Bottom