Kosa ni la nani?

Kosa ni la nani?

chikara

New Member
Joined
Mar 30, 2015
Posts
4
Reaction score
1
Mdau wa MMU,

Ni imani yangu umeyaanza vyema mapumziko marefu ya mwishoni mwa wiki.

Ninakuja kwenu kuomba ushauri kwa tatizo linalo nikabili. Mnamo wiki iliyopita niliamua kwenda kutembea mazingira ya nje ya nyumbani kwangu na kupigiwa simu na dada mmoja ambae tunafanya kazi kampuni za mtu moja lakini katika ofisi tofauti.

Nami bila hiyana nikamweleza mahali nilipo nae hakuchelewa akaja. Tulibadilishana mawazo ya kazi kwani mimi na yeye sote tu waendeshaji wakuu wa makampuni mawili tofauti yenye mmiliki mmoja.Baada ya muda mfupi wa maongezi ya kikazi, akanieleza hajafurahia mazingira tuliyokaa,nami kama kijana rijali nikatambua nia yake. Nikamchombeza kidogo na kumwomba mhudumu wa ile hotel tupate private room.

Nilimpa haki yake na kisha akanieleza mahusiano yake na mtu wangu wa karibu kifamilia nami nikamhakikishia kuwa sitomweleza huyo ndugu yangu wa karibu,nikamsihi na yeye pia anitunzie hiyo aibu kwani sikuwahi kumtongoza au kuwa na mahusiano ya karibu zaidi ya kiuendaji tu.

Nikajua labda aliwaza siku nying na aliona huo ni muda mwafaka kwa yeye kunitunuku dhahabu yake. Lakini J3 nimepata simu toka kwa jamaa yangu akiomba tuonane ingawa hatujaweza onana, ameamua kuniweka wazi kuwa huyo ni mtu wake hivyo nisimfatilie na tayari ameelezwa juu ya mimi kumfuatilia huyo binti.

Nilichukuwa uamuzi wa kumpigia nimweleze masikitiko yangu huku nikimkumbusha yale tuliyokubaliana,lakini baada ya muda mfupi nikapata ujumbe toka kwa mpenzi wake ukieleza tena juu ya mahusiano yao na jinsi alivyomuuliza na kuelezwa.

Nimebaki najiuliza je huyu mwanamke ni kipi alichokuwa akikitafuta kwangu? Hadi mda huu anaendelea kunisumbua juu ya kuomba nisikatishe mahusiano nae na yuko tayari kukutana nami muda wowotenikimhitaji.
Nimeumia sana,sikutegemea kufanya kitu cha namna hii maishani mwangu.
 
Kwa vile tayari anamtu wake istoshe huyo mtu wake ni nduguyo,nadhan hakuna namna zaidi ya ku move on...waache wao waendelee na mapenzi yao kwa heshima ya huyo ndugu yako
 
Katika mazingira hayo usikubali tena kukutana nae maeneo ya siri lasivyo fumanizi linakuhusu
 
Kuna njama anakuandalia.

Kuwa makini
 
Duh kweli umeuma mpaka umeamua kujiunga na JF ili utueleze hii shida yako. Anyway alichofanya huyo demu ni kuhakikisha yeye hashtukiwi at your expense lakini yawezekana kweli anakuhitaji ila anampoteza maboya nduguyo, cha muhimu ushajua nduguyo anakula hapohapo wewe mpotezee kwenye mambo ya faragha
 
Huyo mpotezee,utakua unatafuta uadui na huyo jamaa yako.mkwepe kadiri uwezavyo mkuu
 
Mdau wa MMU,

Ni imani yangu umeyaanza vyema mapumziko marefu ya mwishoni mwa wiki.

Ninakuja kwenu kuomba ushauri kwa tatizo linalo nikabili. Mnamo wiki iliyopita niliamua kwenda kutembea mazingira ya nje ya nyumbani kwangu na kupigiwa simu na dada mmoja ambae tunafanya kazi kampuni za mtu moja lakini katika ofisi tofauti.

Nami bila hiyana nikamweleza mahali nilipo nae hakuchelewa akaja. Tulibadilishana mawazo ya kazi kwani mimi na yeye sote tu waendeshaji wakuu wa makampuni mawili tofauti yenye mmiliki mmoja.Baada ya muda mfupi wa maongezi ya kikazi, akanieleza hajafurahia mazingira tuliyokaa,nami kama kijana rijali nikatambua nia yake. Nikamchombeza kidogo na kumwomba mhudumu wa ile hotel tupate private room.

Nilimpa haki yake na kisha akanieleza mahusiano yake na mtu wangu wa karibu kifamilia nami nikamhakikishia kuwa sitomweleza huyo ndugu yangu wa karibu,nikamsihi na yeye pia anitunzie hiyo aibu kwani sikuwahi kumtongoza au kuwa na mahusiano ya karibu zaidi ya kiuendaji tu.

Nikajua labda aliwaza siku nying na aliona huo ni muda mwafaka kwa yeye kunitunuku dhahabu yake. Lakini J3 nimepata simu toka kwa jamaa yangu akiomba tuonane ingawa hatujaweza onana, ameamua kuniweka wazi kuwa huyo ni mtu wake hivyo nisimfatilie na tayari ameelezwa juu ya mimi kumfuatilia huyo binti.

Nilichukuwa uamuzi wa kumpigia nimweleze masikitiko yangu huku nikimkumbusha yale tuliyokubaliana,lakini baada ya muda mfupi nikapata ujumbe toka kwa mpenzi wake ukieleza tena juu ya mahusiano yao na jinsi alivyomuuliza na kuelezwa.

Nimebaki najiuliza je huyu mwanamke ni kipi alichokuwa akikitafuta kwangu? Hadi mda huu anaendelea kunisumbua juu ya kuomba nisikatishe mahusiano nae na yuko tayari kukutana nami muda wowotenikimhitaji.
Nimeumia sana,sikutegemea kufanya kitu cha namna hii maishani mwangu.

Achana nae huyo...jali kazi za mwajiri wako!
 
Back
Top Bottom