Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,441
- 40,534
Watanzania wameichoka CCM lakini kosa kubwa la wapinzani ni kuonesha kwamba wao ndiyo wanapambana na CCM badala ya kuwafanya watanzania wote wapambane na CCM, matokeo yake watanzania wanadhani kwamba wanaoshindwa siku zote ni wapinzani na wala wao hawahusiki.
CCM huwa inaonesha kwamba yenyewe inawakilisha matakwa mapana ya watanzania wakati wapinzani wao wanakuwa wako bize kuwaambia watanzania kwamba CCM ni mbaya na wao ni watu wema.
Watanzania wameaminishwa na wapinzani kwamba CCM ni wachafu, na hilo wamelikubali, kwa sasa ukisema kwamba CCM kuna mafisadi, watanzania hawashangai. Kwa kitendo cha wapinzani kuonekana ni wasafi, CCM wakisema wapinzani wana mafisadi watanzania wanastuka na kuchukia! Na hapo mara zote Kosa wanalolifanya wapinzani ni kushindwa kulinda utakatifu wao kinadharia!
Uchafu wote unaoumbuliwa hivi sasa na Magufuli unatokana na uendeshaji serikali uliokuwa unafanywa na Marais waliotangulia ambao wote wanatokana na CCM. Lakini leo hata kama "wanaotumbuliwa majipu" wanaonewa na watawala, wapinzani wakijaribu kuwatetea itaonekana kama wanakwenda kinyume na Uasili wao, yaani usafi. Na ni lazima wananchi watawachukia.
Kosa la wapinzani ni kujiweka kwenye nafasi ya kudumu ya kuikosoa CCM badala ya kuwa kwenye nafasi ya waendesha serikali watarajiwa. Nilikwenda kwenye Kampeni ya mgombea Ubunge mmoja wa UKAWA nikamsikia akisema "nichagueni ili niende kubweka dhidi ya serikali ya CCM" nikajisemea huyu naye kweli anaamini kwamba UKAWA itashinda na kushika dola?
Wapinzani geuzeni vita dhidi ya CCM isiwe kati yenu na CCM bali kati ya wananchi na CCM.
cc: "list of 46"