Kosa kubwa walilofanya DC Comics

Kosa kubwa walilofanya DC Comics

UNCLE THREE

Member
Joined
Jul 20, 2021
Posts
25
Reaction score
88
Dc Comics na Marvel ni washindani wakubwa katika vibonzo au comics lakini pia katika kutengeneza Filamu na hata vikaragosi au cartolns pia.

MARVEL wamewaacha mbali DC katika filamu hasa katika miaka ya karibuni na kilichowafany Marvel awe anawasumbua DC ni maamuzi aliyechukua Mkurugenzi wa Marvel Kevin Feige mwaka 2008.

Mwaka 2008 Kevin Feige aliamua Marvel waanzishe ulimwengu wao wa filamu nia ni kuwa matukio yanatotokea katika filamu yaingiliane au yawe yana muendelezo katika filamu nyingine na akaanza na filamu ya Iron Man.

Kuanzisha ulimwengu wa kisinema sio kazi ndogo kumbuka hadi sasa Marvel ana filamu na series zaidi ya 30 Ambazo kwa namna moja au nyingine zinaingiliana , hii ina maana kila director akipewa dili la kuongoza filamu ya Marvel lazima ataambiwa hata kama ana mawazo yake ajitahidi kutunza kile alichokikuta.

DC COMICS wapo vizur sana katika shows za cartoons au animated tv shows lakini Marvel kawajibu na anaimation ya What if ? Ambayo imefanya vizuri pia.

DC pia alikuwa ananyanyaswa kwenye filamu hivyo akelekeza nguvu kwenye series kama the flash na arrow lakini Marvel naye Miaka ya karibuni kahamia pia katika series kwa kuachia series kama Loki, Wanda na nyinginezo.

Hii ina maana kila sehemu ambapo Dc anataka apumue marvel anaelekeza mashambulizi huko huko.

Hii haina maana kwamba filamu za DC hazipendwi au hawapati faida ? La hasha Dc bado ni kampuni kubwa lakini anaweza akawa kazidiwa hatua kadhaa na Marvel hasa katika kipindi cha miaka 10 au mitano iliyopita.

Lakini je Dc wamekosea wapi ? Na inakuwaje Filamu za Avengers zinapendwa zaidi kuliko filamu kama Justice league?

Wengi wanasema moja ya kosa kubwa la DC ni filamu zao kuwa serious sana kiasi kwamba masihara yanakosekana kabisa hadi zinakuwa zinaboa.

Lakini kumbuka wahusika wengi wa DC ni watu serious , mtu kama Batman filamu yake haiwezi kuwa kama Deadpool, huwez msikia Batman kakamata kibaka mitaa ya Gotham afu akaanza kumtania au kumpa vijembe kama anavyofanya Spiderman akikamata wezi wake mitaa ya Queens.

Dc Nao walihisi kuwa serious ni kosa kwao na wakaamua kuanza masihara kidogo ndio mana filamu kama Shazam na Aqua man zimekuwa zina masihara na u-serious umepungua tofauti na kama tulivyowazoea.

Filamu 3 za Batman maarufu kama the Batman trilogy zilizoongozwa na director Christopher Nolan zilikuwa serious sana na ingawa zilikuwa ni filamu za ma-superheroes lakini zina uhalisia mkubwa sana na zilifanya vizuri sana hasa the Dark knight iliyomtambulisha vilivyo adui Joker aliyechezwa kiustadi mkubwa na marehemu Heath Ledger.

Nahisi Dc baada ya kuona filamu za Nolan zimefanikiwa wakamua filamu zao nyingi ziwe za aina hiyo lakini wakashindwa kufanikisha hilo mfano halisi ni filamu ya Batman vs Superman ilifeli vibaya kwa kutaka kuwa serious mno matokeo yake ikawa kituko.

Lakini Dc sio kwamba hajafanikiwa kutoa filamu nzuri iliyokuwa serious la hasha..filamu ya JOKER Joker ilikuwa haina masihara mengi lakini ilifanya poa na kufanikiwa kuondoka hadi na oscar kwa mhusika mkuu jacquin Phoenix.

Dc ili kushindana na Marvel kuna muda walikuwa wanamendea ma-directors wa Marvel mfano James Gunn aliyefukuzwa na Marvel ingawa kwa sasa kasharudishwa tena kuendelea na filamu zake za Guardians of the Galaxy.

Dc walimchukua James Gunn na akawafanyia project mbili hadi sasa ambazo ni Suicide Squad mpya na series ya PEACEMAKER ambazo ukiziangalia utaona kabisa zina utofauti na projects nyingi za Marvel kwani ingawa ni filamu ambazo zina u-serious mwingi lakini zimezungukwa na masihara mengi pia.

Lakini hebu nisikuchoshe ngoja sasa nikuambie kosa kubwa la DC ni nini? Hasa hasa katika filamu ya the Justice league.

Ni hivi Marvel kabla hajaachia filamu ya AVENGERS part 1 alianza na filamu ya Iron man, the incredible hulk,captain America pamoja na thor .

Kwahiyo kabla ya kuangalia The Avengers watazamaji walikuwa wanamfahamu Iron man, black widow (mana black widow mara ya kwanza kaonekana kwenye Iron man), Thor, Loki ,Hulk pamoja na captain America.

MARVEL alianza kuwatengeneza na kuwatambulisha Superheroes wake kwenye Filamu zao binafsi kabla hajawakutanisha pamoja kwenye filamu ya AVENGERS.

Nia ilikuwa ni kuwatengenezea chemistry nzuri watazamaji na Superheroes hao ili wasishangae sana pale watakapowaona kwenye screen pamoja.

Ndio mana kwenye Avengers superhero aliyeongezeka ni Hawkeye pekee ila wengine wote tayari watazamaji tulikua tunawajua.

DC Katika filamu ya Justice League (ile ya kwanza kabla the snyder cut kuachiwa)
Walimtambulisha Aqua man , Flash, na Cyborg bila hata kuwapa filamu zao binafsi.

Aqua man alipewa filamu yake baada ya Justice league kutoka, The flash naye filamu yake haijatoka bado (ndio kuna series ya The flash lakini Barry Allen wa kwenye series na filamu ni watu wawili tofauti)
Cyborg na yeye filamu yake haieleweki itatoka lini mana hata mwigizaji Ray Fisher ambaye ndiye kavaa uhusika huo kashafukuzwa kazi na DC kutokana na mambo binafsi.

Hivyo kuwaleta Superheroes ambao hatujawahi kuwaona hapo kabla na kuwakutanisha kunakuwa hamna mashiko kama kuwatambulisha kwanza mmoja alafu baadae ndio kuwaleta pamoja wapambane kama walivyofanya Avengers.

Hebu fikiria Avengers infinity war ingekuwa imetoka bila baadhi ya filamu binafsi za masuperheroes kutoka unadhani ingekuwaje?

Yani unawaona tu Guardians of the galaxy wanaongea na Thor hata huwajui ni akina nani? Au mara Black panther huyo anatokea anasema twende wakanda na hata hujui Wakanda ni wapi?

DC Wanaweza kujitetea kuwa wanaamin kuww mashabiki wao wengi wanasoma comics inaweza ikawa kweli lakini je inakuwaje kwa wale ambao hawasomi hizo comics?

Mfano sisi watanzania wengi ni wavivu kusoma nani atakubali kusoma comic ya Justice league wakati kuna filam yake?

Na hilo ndio kosa kubwa la DC walitukutanishia Superheroes wengi kwa pamoja bila kututambulishia mmoja mmoja kwanza alafu baadae ndio wakatukusanyia wote kwenye screen.

Author:
Betuel Edson (Film Enthusiast)
 
Happy kwa Flash kusema hajatam ulishwa before sikweli hiyo series ya The Flash ni utambulisho tosha, alafu suala la Berry Alan kufukuzwa kazi halina mantiki kwenye Character kinachoangaliwa Character sio muigizaji character ya Flash, Cyborg nk itabaki palepale.
 
Kampun hiyo ya Marvel ina film nzur sana ingawa nying ni za kufikirika
 
Kosa kubwa ni moja tu
Dc hawana continuity

Hawana long term project planning Kama marvel

Second kitendo cha wao kutoa filamu nyingi bila mpangilio zikichezwa na characters tofauti mfano Batman trilogy na Superman trilogy Ina haribu chermistry

Mfano marvel Robert amecheza iron man zote pekee hatujasikia kuna iron man mwengine unless ....ndio wakaleta concept ya multiverse kwamba uhusika mmoja unaweza chezwa na watu tofauti

Ndio maana Spiderman no way home walileta concept ya multiverse kidogo iyo iko reasonable hata wakiwa wapo tofauti Tobey ,tom na Andrew .

Inshort dc Hawana plan wapowapo tu
 
Back
Top Bottom