Kosa kubwa Serikali inafanya kuhusu Magomeni Kota!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Nimemsikia Waziri wa Ardhi akisema kwamba Serikali imemaliza mgogoro uliokuwepo kati ya wakazi wa eneo la Magomeni Kota na TAMISEMI na sasa Serikali imeamua kwamba itajenga Nyumba na kuwauzia wakazi asilia wa eneo hilo kwa bei nafuu, mpaka hapo sina tatizo na pia nauunga mkono!

Ila tatizo langu liko kwenye matumizi ya ardhi, kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi Serikali inatarajiwa kujenga Nyumba 644 eneo hilo na watakazouziwa zitakuwa na vyumba vitatu, sasa kwangu mimi haya ni matumizi mabaya sana ya ardhi ikizingatiwa mahali kama Magomeni ambapo ni mjini kabisa na kunaweza kuvutia watu wengi kuishi hapo kwa sababu ya ukaribu wake na mjini yaani eneo la kazi, kwa nini Serikali wasijenge Maghorofa kama yale ya fire Kariakoo au Mwenge Jeshini?

Ukijenga Maghorofa ya Msajili una uwezo wa kuchukuwa watu wengi zaidi na kwenye eneo dogo na eneo linalobakia kutumiwa kwenye matumizi mengine kama viwanja vya kuchezea vya watoto au hata Shule na Hospitali, lkn kujenga nyumba moja moja huko kwa maoni yangu ni kuharibu hilo eneo, kwani Dar tayari tuna uhaba wa Ardhi na Mji wetu karibia unaunga na Bagamoyo na Kibaha na haipaswi kuwa hivyo kwa maana Bagamoyo au Kibaha ni Mkoa mwingine hivyo haipaswi kuungana!

Ningeishauri Serikali ichukuwe Ramani ya Michenzani, Zanzibar ambapo wamejenga hayo Maghorofa ya gharama nafuu na ya watu wa kawaida!

michenzani.jpg

88065695.jpg

michenzani2.jpg

Zanzibar+200.jpg

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemaliza mgogoro wa makazi wa Magomeni Kota uliodumu kwa kipindi kirefu.

Hayo yamesbainishwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi wakati akiongea na Kamati ya Mgogoro wa Makazi ya Magomeni Kota mbele ya waandishi wa habari.

“Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefuta hati na mikataba yote inayohusiana na ardhi ya yaliyokuwa makazi ya Magomeni Kota, Dar es Salaam”,alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Lukuvi Rais ameondoa umiliki wa eneo hilo toka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kumilikisha Serikali Kuu ambayo ndiyo itakayosimamia ujenzi wa nyumba 644 ambazo zitauzwa kwa bei nafuu kwa waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota.

“Tutajenga nyumba 644 na kuwauzia kwa bei ya jengo na siyo ya ardhi ili kuwapeni unafuu katika kununua,”alisema Lukuvi huku akishangiliwa na baadhi ya wakazi wa Magomeni.

Aidha, Lukuvi amesema kuwa anampongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kumaliza mgogoro huu ambao umedumu kwa muda mrefu na kuongeza kuwa ameagiza timu ya wataalamu wa Wizara kupima na kuchora michoro kwa ajili ya ujenzi.

Lukuvi amesema katika eneo hilo zitajengwa nyumba za heshima ambazo kila moja itakuwa na vyumba vitatu ili kukidhi mahitaji ya kifamilia kwani watu hawa wamekaa kwa miaka takribani 50 hadi wameshapata wajukuu. Ameongeza kuwa kila mmiliki wa nyumba hiyo atapewa hati yake hata kama nyumba hiyo itakuwa kwenye ghorofa.

Lukuvi amesema kuwa Rais ameagiza maeneo kama ya Magomeni Kota katika mikoa ishirini ya Tanzania Bara nayo yatakuwa katika mfumo huo wa Magomeni. Kwa mujibu wa Lukuvi wazee ambao wanakaa kwenye nyumba kama hizo sehemu nyingine wasiondolewe kwani hao walikuwa watumishi wa umma hivyo Rais amesema wasibughudhiwe.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Mgogoro wa Makazi Magomeni Kota, George Abel ameshukur Mhe Rais Magufuli na Wazir Lukuvi kwa kutatua mgogoro huo ambao anadai umewasumbua sana.

Ameahidi kutoa ushirikiana kwa Serikali pindi suala la ujenzi litakapokuwa linaendelea ili kuhakikishaujenzi unaenda haraka.

Naye Wakili ambaye alikuwa akiendesha kesi hiyo kabla ya Mhe. Rais kuingilia kati, Mhe. Twaha Tasilima ameonyesha kuridhishwa na utendaji wa Rais Magufuli.

“Rais Dkt Magufuli na Mhe. Waziri Lukuvi ni watu wa vitendo na si maneno na kweli wanawajali wanyonge, nawashukuru sana,”alisema Tasilima.

Uamuzi wa kurudisha eneo hilo kwenye Serikali Kuu umetolewa na Rais Magufuli tarehe 10/7/ 2016
 
Ile eneo si waweke bustani nzuri tu ..kila eneo kujenga tu?...waite Magomeni Water Park, iwe na fountains za maji na maua mazuri mjini utapendeza...

Hapana kuweka bustani eneo lote siyo wazo zuri kwa maana ni eneo kubwa sana ila kuna uwezekano wa kujenga Maghorofa na pia kubakiza eneo la bustani ya kutosha tu, ukiweka mablock kama yale ya Mwenge au fire inatosha kabisa na kupata sehemu ya bustani pia!
 
Acha kuikosoa serikali wewe sema Yes tu,wataalamu wameshafanya upembuzi yakinifu na return kwa mauzo hayo
 
Inafanya Kazi ya kuchekesha wasio na upeo wakati nchi inaharibikà NA wenye akili wameshaonya tayari,tangu lini serikali ikajengea watu badala ya kuwafidia?wanatumia sheria gani ya Ardhi au yoyote ile? Na kama lilikuwa eneo la tamisemi je serikali kuu Imewafidia halmashauri?
 
Mpaka hapo Serikali iko sawa kabisa kwenye kuwapa kipaumbele cha kwanza wakazi asilia wa hilo eneo, nafikiri labda haujaelewa haiwajengei bali inajenga Nyumba bora zaidi na za hadhi klk hizi zilizopo na kuwauzia kwa bei nafuu.

Watu wa hilo eneo wana haki pia ya kuishi hapo kama wanapenda na Serikali ina jukumu la kuwalinda kama ilivyo na jukumu na kulinda raia wote wanyonge wasinyanyaswe na wenye uwezo zaidi yao, ila tatizo kwa maoni yangu lipo kwenye matumizi ya hilo eneo kujenga nyumba moja moja ni matumizi mabaya ya ardhi!
 
Hapana kuweka bustani eneo lote siyo wazo zuri kwa maana ni eneo kubwa sana ila kuna uwezekano wa kujenge Maghorofa na pia kubakiza eneo la bustani ya kutosha tu, ukiweka mablock kama yale ya Mwenge au fire inatosha kabisa na kupata sehemu ya bustani pia!
Nyamazaaaaaa! Unaweza kuwa na akili nyingi kumzidi Rais wewe? Watu wengine mpogoje lakini? Serikali imesema itajenga tujumba tudogo tudogo ili kila raia ajitawale kwake full stop!!
 
Nimemsikia Waziri wa Ardhi akisema kwamba Serikali imemaliza mgogoro uliokuwepo kati ya wakazi wa eneo la Magomeni Kota na TAMISEMI na sasa Serikali imeamua kwamba itajenga Nyumba na kuwauzia wakazi asilia wa eneo hilo kwa bei nafuu, mpaka hapo sina tatizo na pia nauunga mkono!

Ila tatizo langu liko kwenye matumizi ya ardhi, kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi Serikali inatarajiwa kujenga Nyumba 644 eneo hilo na watakazouziwa zitakuwa na vyumba vitatu, sasa kwangu mimi haya ni matumizi mabaya sana ya ardhi ikizingatiwa mahali kama Magomeni ambapo ni mjini kabisa na kunaweza kuvutia watu wengi kuishi hapo jkwa sababu ya ukaribu wake na mjini yaani eneo la kazi, kwa nini Serikali wasijenge Maghorofa kama yale ya fire Kariakoo au Mwenge Jeshini?

Ukijenga Maghorofa ya Msajili una uwezo wa kuchukuwa watu wengi zaidi na kwenye eneo dogo na eneo linalobakia kutumiwa kwenye matumizi mengine kama viwanja vya kuchezea vya watoto au hata Shule na Hospitali, lkn kujenga nyumba moja moja huko kwa maoni yangu ni kuharibu hilo eneo, kwani Dar tayari tuna uhaba wa Ardhi na Mji wetu karibia unaunga na Bagamoyo na Kibaha na haipaswi kuwa hivyo kwa maana Bagamoyo au Kibaha ni Mkoa mwingine hivyo haipaswi kuungana!
pamoja na kujitoa Akili kwenye mambo ya msingi Leo kwa Mara ya kwanza ninakuunga mkono hoja yako.
 
Lengo lao kuu ni kupora mamlaka ya usimamizi wa ardhi kutoka serikali za.... na tawala za mikoa ili kujaribu kuondoa uwezekano wa Mstahiki Meya wa kinondoni kuchapa kazi iliyowashinda ccm kwa miongo kadhaa.

Wana roho mmmbaya kama sura ya waziri wa udongo.
 
Ile eneo si waweke bustani nzuri tu ..kila eneo kujenga tu?...waite Magomeni Water Park, iwe na fountains za maji na maua mazuri mjini utapendeza...

....unapenda maua umekua nyuki!
 
Ile eneo si waweke bustani nzuri tu ..kila eneo kujenga tu?...waite Magomeni Water Park, iwe na fountains za maji na maua mazuri mjini utapendeza...
uko sawa utatofautiana na wengi wasiojua maana ya urban breathing hill wazo LA kitaaluma zaidi na faida yake nikubwa Mara dufu kiuchumi na kijamii
 
Nimemsikia Waziri wa Ardhi akisema kwamba Serikali imemaliza mgogoro uliokuwepo kati ya wakazi wa eneo la Magomeni Kota na TAMISEMI na sasa Serikali imeamua kwamba itajenga Nyumba na kuwauzia wakazi asilia wa eneo hilo kwa bei nafuu, mpaka hapo sina tatizo na pia nauunga mkono!

Ila tatizo langu liko kwenye matumizi ya ardhi, kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi Serikali inatarajiwa kujenga Nyumba 644 eneo hilo na watakazouziwa zitakuwa na vyumba vitatu, sasa kwangu mimi haya ni matumizi mabaya sana ya ardhi ikizingatiwa mahali kama Magomeni ambapo ni mjini kabisa na kunaweza kuvutia watu wengi kuishi hapo kwa sababu ya ukaribu wake na mjini yaani eneo la kazi, kwa nini Serikali wasijenge Maghorofa kama yale ya fire Kariakoo au Mwenge Jeshini?

Ukijenga Maghorofa ya Msajili una uwezo wa kuchukuwa watu wengi zaidi na kwenye eneo dogo na eneo linalobakia kutumiwa kwenye matumizi mengine kama viwanja vya kuchezea vya watoto au hata Shule na Hospitali, lkn kujenga nyumba moja moja huko kwa maoni yangu ni kuharibu hilo eneo, kwani Dar tayari tuna uhaba wa Ardhi na Mji wetu karibia unaunga na Bagamoyo na Kibaha na haipaswi kuwa hivyo kwa maana Bagamoyo au Kibaha ni Mkoa mwingine hivyo haipaswi kuungana!
Kuna sehemu ametaja atajenga nyumba mojamoja? Kuwa na nyumba 600+ si lazima ikawa nyumba moja moja yanaweza kuwa magorofa na ikatoa nyumba hzo...wewe ulivyoona kasema nyumba 600+ ukaconclude kwamba anamaanisha ni lazima ajenge nyumba za chini...subiri mipango uone..wasi wasi wangu uwezo wa hao watu kununua hzo nyumba.
 
Nimemsikia Waziri wa Ardhi akisema kwamba Serikali imemaliza mgogoro uliokuwepo kati ya wakazi wa eneo la Magomeni Kota na TAMISEMI na sasa Serikali imeamua kwamba itajenga Nyumba na kuwauzia wakazi asilia wa eneo hilo kwa bei nafuu, mpaka hapo sina tatizo na pia nauunga mkono!

Ila tatizo langu liko kwenye matumizi ya ardhi, kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi Serikali inatarajiwa kujenga Nyumba 644 eneo hilo na watakazouziwa zitakuwa na vyumba vitatu, sasa kwangu mimi haya ni matumizi mabaya sana ya ardhi ikizingatiwa mahali kama Magomeni ambapo ni mjini kabisa na kunaweza kuvutia watu wengi kuishi hapo kwa sababu ya ukaribu wake na mjini yaani eneo la kazi, kwa nini Serikali wasijenge Maghorofa kama yale ya fire Kariakoo au Mwenge Jeshini?

Ukijenga Maghorofa ya Msajili una uwezo wa kuchukuwa watu wengi zaidi na kwenye eneo dogo na eneo linalobakia kutumiwa kwenye matumizi mengine kama viwanja vya kuchezea vya watoto au hata Shule na Hospitali, lkn kujenga nyumba moja moja huko kwa maoni yangu ni kuharibu hilo eneo, kwani Dar tayari tuna uhaba wa Ardhi na Mji wetu karibia unaunga na Bagamoyo na Kibaha na haipaswi kuwa hivyo kwa maana Bagamoyo au Kibaha ni Mkoa mwingine hivyo haipaswi kuungana!
haya maamuzi ni ya visasi,na hizo nyumba za vyumba vitatu hao maskini zitawashinda bei si chini ya milioni 40
 
Hukufuatilia kwa makini taarifa ya Mhe. Waziri, kwani unachokipendekeza ndio hicho alichosema waziri.
 
Kuna sehemu ametaja atajenga nyumba mojamoja? Kuwa na nyumba 600 si lazima ikawa nyumba moja moja yanaweza kuwa magorofa na ikayoa nyumba hzo...wewe ulivyoona kasema nyumba 600+ ukaconclude kwamba anamaanisha ni lazima ajenge nyumba za chini...subiri mipango uone..

Imeandikwa watajengewa ,,nyumba za vyumba vitatu" na kuuziwa, hiyo maana yake nini? na unawezaje kujenga Maghorofa zaidi ya 600 kwenye hilo eneo?
 
Back
Top Bottom