Korodani bandia kutengeneza shahawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Korodani bandia kutengeneza shahawa?

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Mar 26, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Wanasayansi nchini Marekani wako mbioni kutengeneza korodani bandia (artificial testicle) zitakazokuwa zikitengeneza shahawa ili kusaidia wanaume wenye matatizo ya uzazi.
  [​IMG]
  Timu ya wanasayansi katika jimbo la San Fransisco nchini Marekani chini ya Dk Paul Turek wamepewa ruhusa ya kuendelea na utafiti huu baada ya kuahidiwa kupewa pesa za kutosha kutekeleza mradi huu.  Kwa muda mrefu, wanasayansi wamejaribu kutengeneza seli za shahawa (Sperm Cells) bila mafanikio kwa vile wamefanikiwa kutengeneza robo tatu tu ya mchakato wa kupata shahawa kamili. Hii inatokana na mazingira maalum yanayopatikana katika korodani kuhitajika kukamilisha utengenezaji wa shahawa hizo. Mazingira hayo ya uhalisia ni tofauti na mazingira yoyote yale ya nje katika utengenezaji shahawa.

  Korodani hizo zitakuwa katika umbo la duara (cylindrical shape) na zitakuwa na urefu wa inchi kadhaa na hazitahitaji kupachikwa kwenye mwili wa binadamu. Aidha kifaa hiki kitakuwa tofauti na korodani nyingine bandia ambazo huwekewa wanaume waliokosa korodani moja kutokana na sababu mbalimbali.Kwa kawaida korodani za namna hii huwa hazitengenezi shahawa kwa vile hujazwa maji maalum ya saline solution ili kutumika kama mapambo.

  Ili kufanikisha hili, wanasayansi hao itabidi kubuni utaalamu wa kutengeneza chembechembe za shahawa na wamepanga kutumia seli za asili (human embryonic stem cells) zilizoongezewa jena (genes) ili kuzifanya kuwa seli zinazoweza kuzaa chembechembe za shahawa na hivyo kutumika katika njia za kutungisha mimba kwenye maabara zinazojulikana kama In Vitro Fertilization (IVF).[​IMG]

  Wakati tafiti zimeonesha ya kwamba inawezekana kutibu panya dume mwenye matatizo ya uzazi kutoka katika seli zao za asili yaani embryonic stem cells, kwa binadamu tafiti hizi zimeshindwa kuzaa matunda yoyote yale mpaka sasa.

  Kyle Orwig, Profesa wa masuala ya uzazi na magonjwa ya wanawake (Obstetrics and Gynecology) na sayansi ya uzazi (Reproductive Sciences) anasema “Ni mradi wa matumaini sana lakini nina wasiwasi kama utafanikiwa, ukifanikiwa itakuwa ni mafanikio makubwa sana katika sayansi ya tiba ya uzazi.” Kwa kawaida, shahawa hutengenezwa na kuhifadhiwa katika korodani za mwanaume.

  Matatizo ya kushindwa kutungisha mimba kwa wanaume hutokana na hitilafu katika mfumo wa uzalishaji shahawa kwenye korodani unaosababishwa na magonjwa ya cystic fibrosis, matatizo ya jena (genetic defects), korodani ambazo hazijashuka katika sehemu sahihi (undescended testis), madhara katika korodani kama ajali na saratani ya kwenye korodani.

  Kwa habari na matukio ya kila siku tembelea www.ughaibuni.com
   
 2. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Dear MziziMkavu!
  I'm very sceptical with this topic! kwanza tuanze kuangalia jinsi mbegu za jinsia ya kiume zinavyotengenezwa. hapa naandika kwa kifupi as I told you before katika topic ya mama mjamzito kuvimba miguu kuwa kuandika kiswahili ktk sayansi ni vigumu sana: but hapa chini nitaandika kwa ufupi:
  Spermatogenesis ni utaratibu ambao mbegu (seli (chembe, ) ya jinsia ya kiume, au gametes) hutengezwa. Hii hutokea kwa makende ya kijana, kuanzia wakati wa kubalehe na kuendelea mpaka mwisho wa ya maisha yake.

  Spermatogenesis (hutengenezwaji wa chembe hizi) huanza mara moja wakati wa chembe au seli changa (spermatogonia) kukomaa na kukua kuwa spermatocyte . Seli hii hujigawa katika hatua ya kwanza itwayos meiosis I na kufanya spermatocytes mbili. Baada ya meiosis ya II, hutengenezwa haploid spermatids nne. Hizi spermatids nne hukua na kuwa manii (sperm)zilizo komaa. katika kipindi hiki kutakakuwa na chromosomes 23.
  Na ili huu mtiriliko wote utokee, inabidi kuwe na vichochezi (hormones) mablimbali na mzaingira ya kufaaa.
  3 yrs ago Chuo cha Norrkoping, Sweden, kitengo cha biomedicine walidai wanaweza fanya, two months later wakasema haiwezekani. na sioni sababu yoyote ya kuspend katika reseach hiyo waka Intracytoplasmic sperm injection(ICSI) inaweza tumica.
  unadai kordani hizo hazitapachikwa katika mwili wa mwanaume,je zitaregulate vipi temp. na mbegu zitakuwa vipi? niaandikie kidogo Idea zako then tunaweza ongea zaidi!
  nimependa topic yako::
  [h=3][/h]
   
Loading...