Korea ya kaskazini yasema itawahi kuishambulia marekani kwa nyuklia

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,784
20,154
Serikali ya Korea Kaskazini imemuonya Rais mpya wa Marekani, Donald Trump kuhusu siasa zake za kiuhasama na kusema kwamba ikiwa nchi hiyo itapanga kuishambulia, Pyongyang itakuwa ya kwanza kuanzisha mashambulizi.
Gazeti la Rodong Sinmun la chama tawala cha Korea Kaskazini limeandika kuwa, nchi hiyo itaendelea kuimarisha uwezo wake wa silaha za nyuklia na nguvu zake za kiulinzi. Gazeti hilo limefafanua kuwa, Pyongyang inakutambua kuingia madarakani rais huyo mpya huko Marekani kuwa kumeifanya hali ya mambo kimataifa kuwa mbaya zaidi na kwamba ili kukabiliana na hali hiyo haina njia nyingine ghairi ya kuimarisha uwezo wake wa kiulinzi na silaha za nyuklia.
Kadhalika ripoti hiyo imesisitiza kuwa, Korea Kaskazini kama moja ya nchi zenye uwezo wa nyuklia duniani, inafanya juhudi za kuimarisha usalama na kwamba itaendeleza siasa hizo.
Gazeti hilo limekosoa vikali maneva ya kijeshi ya kila mwaka yanayofanywa kwa pamona na Marekani na Korea Kusini ambayo mwaka huu yamepangwa kufanyika mwezi Machi na kusisitiza kuwa, mazoezi hayo yamelitia hatarini eneo zima la Peninsula ya Korea.
Wakati huo huo televisheni ya taifa ya Korea Kaskazini imeripoti kuwa, kwa kutegemea uwezo wake wa silaha za nyuklia, nchi hiyo imejiandaa kuingia katika vita vya kila aina na Marekani
 
MWENYE ENZI MUNGU ILINDE DUNIA YANGU MILELE YOTE AMEN RA
 
Angekuwa mjanja angelipua kimya kimya sasa hayo makelele anatishia tu
 
Back
Top Bottom