Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,580
- 18,157
Duru Za Kimataifa: Pyongyang-Korea ya Kaskazini
Masaa machache yaliyopita Taifa la Korea ya Kaskazini limefanya majaribio mapya ya Makombora ya Masafa mafupi(Short Range Missiles) .
Jana nchi wanachama wa UN Security Council walipiga kura ya pamoja na kupitisha azimio la vikwazo vikali baada ya Urusi juzi kuchelewesha kura hiyo kwa kutaka kwanza wasome rasimu ya Azimio baada ya Kikao cha Obama na Rais Xi Jinping wa China hivyo Urusi wakataka kuona kama Maoni yao kwenye Rasimu yapo sawa kabla ya hatua ya upigaji Kura.
Jana niliandika mahali muda mfupi baada ya kusoma azimio namba 2270(2016) la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa(UNSC Resolution 2270) juu ya kuiwekea vikwazo vikali zaidi(Tough Sanctions) Korea ya Kaskazini kuwa hawa watu sio rational actor kwenye siasa za kimataifa kama Irani ya sasa na nikasema reaction ya Rais wao Kim Jong-Un inaweza kuwa ya kijeuri zaidi.
Ndivyo ilivyotokea masaa machache yaliyopita.Hapa ni sawa na kutuma ujumbe wa jeuri kwa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuonyesha hasira dhidi ya Azimio namba 2270(2016) lililolenga kuhakikisha inabanwa kurudi kwenye meza ya mazungumzo(Negotiation Table) badala yake wamejibu kwa Millitary Action .Ukaidi!
Vikwazo vinahusisha kuzuia wataalamu wa kijeshi wa Korea ya kaskazini kutoa huduma za kijeshi kama walivyofanya kufundisha jeshi la polisi la Uganda Recently,Mabenki na Taasisi za Fedha marufuku kufanya kazi na Korea ya Kaskazini,Marufuku kukodishia au kuiuzia ndege Korea ya Kaskazini,Makampuni 12 na watu 16 wamekuwa blacklisted ambao ni washirika na serikali ya Kim Jong-Un,Biashara ya mafuta na Korea marufuku,Hakuna kununua malighafi ya Chuma kutoka Korea ,Meli zote zikaguliwe na pia bidhaa za anasa kwenda Korea Marufuku na hata Magari(Trucks) ambayo yanaweza kugeuzwa kuwa magari ya kijeshi marufuku kuiuzia Korea
Je,China mshirika wa karibu atakubali kutimiza wajibu wake kutekeleza azimio dhidi ya North Korea?
Pamoja na kuwa naona kila Dalili ya Korea ya Kaskazini kuendeleza majaribio,lakini katika sheria za kimataifa jaribio lao la masaa machache yaliyopita sioni kama limekiuka sheria za kimataifa kama lile la Mwezi January maana lilivunjilia mbali Mkataba wa kudhibiti Makombora ya Masafa Marefu na ya Hatari (Anti-Ballistic Missiles Treaty)
Wakati Iran ilipowekewa Vikwazo,Tanzania ilituhumiwa kuwa meli zenye bendera yake zilitumika kukwepa Vikwazo dhidi ya Iran
Safari hii Tannzania inahitaji kuwa makini zaidi kwani Korea ya Kaskazini ni Bingwa wa Kukwepa Vikwazo.
Tayari Balozi wa Kudumu wa Marekani Umoja Wa Mataifa Samantha Power ameshatoa angalizo kuwa Korea ni Mabingwa wa Sanctions EVasion.
Aluta Continua,Victory Ascerta....