Korea Kaskazini yasema iko tayari kuzungumza na rais Trump

Malcolm X5

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
1,637
2,747
_96038888_3.jpg

Korea Kaskazini imesema kuwa itafanya mazungumzo na Marekani iwapo mazigira yataruhusu ,kulingana na vyombo vya habari vya Korea Kusini.

Mjumbe mwandamizi wa Korea Kaskazini amesema kuwa mazungumzo na serikali ya rais Trump yanawezekana kufuatia mkutano na waliokuwa maafisa wa serikali ya Marekani nchini Norway.

Awali mwezi huu rais wa Marekani Donald Trump alisema itakuwa heshima kubwa kukutana na rais Kim Jong un.

Matamshi yake yanajiri kufuatia ongezeko la hali ya wasiwasi kuhusu mipango ya Korea Kaskazini ya kinyuklia pamoja na ile ya utengezaji wa makombora ya masafa marefu.

Choe Son Hui ambaye ni afisa katika wizara ya maswala ya kigeni kuhusu maswala ya Marekani kaskazini alitoa matamshi hayo wakati alipokuwa akirudi Pyongyang baada ya mkutano mjini Oslo.

Source :BBC Swahili
 
haya wale wachambuzi wa kwenye makochi wa JF eti oooh vita ipoo, sisi team Korea, mna dhani vita ya nyuklia ni mchezo, wenye nyuklia wenyewe wana ogopa kupigana. Kadri Nyuklia zinavo kuwa nyingi, mambo mengi yatamalizwa kwa amani.
 
Kwani sisi ndo tulikuwa tunataka wapigane au wao wenyewe ndo walikuwa wanataka kupigana?sie mashabiki tu.waamuzi wa mwisho ni wao.
 
Sema marekani kaogopa.si amepeleka mpaka meli za kivita.kaishia sauzi.au umesahau

ndio nnao sema uchambuzi wa kwenye makochi huo, Manowari ya kivita ikienda kwenye bahari ya N.K ni vita!!?
hakuna vita na hakuna taifa linalo taka kupigana mtasubiri sana
 
Marekani ana shida sana kwa walala hoi wenye stress zao, akiimba mambo yaishe kidemokrasia, utasikia "kaukimbia mziki kaogopa" akishambulia akisababisha demage, utasikia "mbona hakupigana peke yake, angeenda peke yake angeona" hahaha! Bora haya mambo yaishe kwa amani ili wabongo wachane mikeka yao.
 
ndio nnao sema uchambuzi wa kwenye makochi huo, Manowari ya kivita ikienda kwenye bahari ya N.K ni vita!!?
hakuna vita na hakuna taifa linalo taka kupigana mtasubiri sana
Naona haukuwepo duniani.wakati mmarekani alipokuwa anatia mikwara ya kumpika kaskazini.akaambuwa rusha hata mchanga.mmarekani akaogopa.
 
Naona haukuwepo duniani.wakati mmarekani alipokuwa anatia mikwara ya kumpika kaskazini.akaambuwa rusha hata mchanga.mmarekani akaogopa.
ndio shida ilipo hapo ila elewa tu mtu mwenye nyukilia hapigwi na ustegemee ata pigwa, hakuna asiye jua madhara ya nyuklia
 
Trump aliposema tu anataka akutane na kim kama hali itaruhusu nikajua hamna vita..

Nadhani kim nae sasa ndo amejibu baada ya kuona hashambuliwi kwa wiki karibu tatu nzima,

marekani atakuonea tu kama uko mnyonge mnyonge
 
Back
Top Bottom