Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,525
- 22,465
Korea Kaskazini jumatatu asubuhi (kwa saa za Korea) imefanikiwa kurusha kombora la masafa marefu lililobeba mtambo wa satellite kutokea kituo cha Sohae nchini humo.
Nchi hiyo ambayo ilitoa taarifa kwa umoja wa mataifa kupitia taasisi ya masuala ya bahari IMO imesema kombora hilo lilikuwa limebeba mtambo wa satellite.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akihutubia baraza la kijeshi mjini Pyongyang.
Updates:
Viongozi wa Korea Kaskazini wamebadilisha tarehe ya kurusha kombora la masafa marefu ambapo wamesema itakuwa ni kati ya tarehe 7 na 14 na si kati ya 6 na 25 kama walivyosema mwanzo.
Taarifa mabalimbali zinadai Korea Kaskazini wanataka kufanya tukio hilo sambamba na mpambano wa soka la nchini Marekani wa Super Bowl linalofanyika siku Jumamosi Usiku saa tano unusu usiku kati ya timu za Carolina Panthers na Denver Broncos.
Mechi ya Super Bowl inatarajiwa kufanyika kisu ya Jumapili nchini Marekani.
Hapo awali nchi ya Korea Kaskazini ilitoa taarifa kwa vyombo vya umoja wa mataifa ikosema ilikuwa inajianda kurusha angani kombora la masafa marefu siku yoyote kuanzia jumamosi usiku.
Inasadikiwa kuwa siku hasa ya kufanya shughuli hio ingekuwa ni Jumapili ambayo kwa Korea Kaskazini itakuwa ni jumatatu.
Nchi hiyo itafanya tukio hilo kinyume na maonyo ya kutoka nchi za Korea Kusini na jumuiya ya Ulaya na Marekani kwamba majaribio ya makombora yamepigwa marufuku na umoja wa mataifa.
Wiki ilopita nchi ya Korea Kusini ambayo ni adui na Korea Kaskazini walitoa taarifa za kijasusi kuonyesha kwamba Korea Kaskazini wangefanya majaribio ya kurusha kombora la masafa marefu lakini nchi hiyo haikufanya hivyo.
Lakini Korea Kaskazini imejitetea kwamba inafanya majaribio ya makombora hayo ili kutaka kuweka chombo cha mawasiliano satellite kwenye njia ya Orbit na kukanusha kwamba inafanya majaribio ya teknolojia mpya ya makombora yaani "ballistic missile technology".
Korea Kaskazini haitajatoa taarifa ya mabadiliko yoyote kwenye utaratibu wa tukio hilo na njia na chombo cha kurushia kombora pamoja na eneo linalotumika kurushia kombora hilo vinabakia kuwa kama vilivyopangwa.
Nchi hiyo iliitoa taarifa kwa taasisi ya masuala ya majini yaani International Maritime Organisation siku ya Jumanne na ingerusha kombora hilo kati ya terehe 8 na 25 mwezi huu wa February lakini hawakusema chochote juu ya mabadiliko yoyote.
Hatua hii kubwa na ya hatari zaidi inakuja baada ya nchi hiyo kufanya jaribio la nne la silaha ya nyuklia mwishoni mwa mwaka jana na wataalam wanahisi kwamba jitihada za nchi hiyo kuweka bomu la nyuklia kwenye kichwa cha kombora la silaha hiyo zimefikia ukingoni.
Taarifa ya Korea Kaskazini kwenda IMO kuonyesha nia ya kurusha kombora la masafa marefu- Picha inatoka shirika la habari la Ufaransa AFP.
Mwaka 2012 Korea Kaskazini wamewahi kurusha kombora walilodai lilikwenda satellite kwenye Orbit na baadae kufanya majaribio ya milipuko ya mabomu mbalimbali mwaka 2006, mwaka 2009, na mwaka 2013.
Taarifa zingine za kijasusi zinasema kwamba nchi hiyo huenda ikarusha kombora hilo siku ya tarehe 16 mwezi huu ambayo ni siku alozaliwa baba wa kiongozi wa nchi hiyo hayati Kim Jong II.
Lakini pia taarifa hizo zinasema kwamba picha za satellite zinaonyesha kituo cha kurushia kombora hilo kiko tayari kwa kombora hilo au Rocket likiwa limefunguka na kuonekana limekwishjazwa mafuta.
Nchi ya Japan tayari wamechukua hatua za dharura zikiwemo za kuweka mitambo ya kuzuia makombora mjini Tokyo na eno la kisiwa cha kusini cha Okinawa ili kutungua mabaki yoyote ya kombora hilo ambayo yatatishia kutua ndani la eneo la kisiwa kizima cha nchi ya Japan.
Korea Kusini na Marekani wao wanajianda kwa kuweka mitambo maalum ya kufuatilia kombora hilo litakaporushwa angani kwa kutumia ndege za kijasusi zenye rada na vyombo vya kuvunjia mabaki ya kombora viitwavyo Aegis-equipped Destroyers.
Pia Korea Kusini imejianda kutumia mtambo wake wa kutungulia makombora uitwao Patriot ambao unaweza kusaka kombora ndani ya maili 9 au kilomita 15 na kutungua kombora hilo.
Korea Kusini Yaweka No-Fly zone kwenye anga lake.
Korea Kusini imetangaza kufunga anga lake upande wa kusini magharibi kuepusha kuvunjwa kwa ndege zake. Pia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Incheon utafungwa kuanzia kuanzia terehe 7 kwa siku 18.
Dunia inangoja tukio hili ambapo saa inaonekana Korea Kaskazini hawana wa kumdhibiti.
Vyanzo vya habari: AFP, Reuters, CNN, Daily Mail, Xinhua, taasisi za utafiti duniani na IMO