Korea kaskazini wadukua mfumo wa GPS wa korea kusini

thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,827
4,757
Maofisa wa korea kusini wamedai kuwa korea kaskazini wamedukua mfumo wa GPS maeneo ya mpakani na kudai kuathiri ndege 110 pamoja na meli na pia inawezesha kusababisha simu za mkononi kutofanya kazi ipasavyo.

Msemaji wa wizara ya South Unification ministry jeong joon-hee ameliita tukio ni la uchokozi.

Msuguano umekuwa mkubwa baina ya korea mbili tangu jaribio la nne la nyuklia lililofanywa na korea kaskazini.

Vitendo vya Udukuzi wa mfumo wa GPS wa korea kusini vimeripotiwa kuanza mwezi uliopita maeneo tofauti tofauti mpakani mwa nchi hizo mbili, lakini alhamisi Korea kaskazini walifanya mashambulizi makubwa na kusababisha jamming ya mfumo wa GPS signals, hii ni kwa mujibu wa bwana Yonhap akinukuu taarifa kutoka kwa maafisa wakuu wa serikali.

Walinzi ya Pwani ya korea kusini wameripoti kwamba karibu meri za uvuvi 70 zililazimika kurudi nchi kavu baada ya kutokea matatizo katika mfumo wa GPS, AFP imesema. hakukuwa na ripoti kutokea kwa matatizo kwa safari za ndege.

Shirika la habari korea kusini limedai kwamba Udukuzi wa mfumo wa GPS umekuwa ukifanywa tangu mwaka 2010 na korea kaskazini. korea kaskazini imedai kwamba taarifa ni za uongo na upotoshaji.

Uchambuzi kutoka mwandishi wa bbc.
Serikali ya korea kusini imesema ndege 58 na meli 52 zimeathiriwa kutoka na kudukuliwa kwa mfumo wa GPS na kusababisha kutofanya kazi vizuri japokuwa madhira yaliyotokea hayakuwa makubwa.

Miaka minne iliyopita GPS ilishambuliwa na safari za ndege 300 ziligunduwa tatizo katika GPS.

Raia mmoja wa korea kusini ameambia bbc kwamba alishangaa kuona ramani yake kuonyesha yupo mbali sana na eneo halisi lilipo.

North Korea 'jamming GPS signals' near South border - BBC News
 
Hao jamaa n watata...pamoja na china kuanza kuwachoka ila bado mkwara wanaendeleza....
 
halafu tunaambiwa N.Korea wana IQ ndogo ukweli hawa jamaa wapo vizuri sana
 
Pamoja na vikwazo lukuki walivyowekewa NK lakini bado speed ya maendeleo yao ni Kali sana! Kama wasingekuwa na vikwazo hawa jamaa ni habari nyingine kabisa!
 
yaa niliipenda waliwapa hasara kubwa sony kwa hasira wakairelease bure, ila U.S.A waliwazimia Internet nchi nzima cyber war ngum sana kupata mshindi manake hakuna system iko 100% secure
Walifanya nn kurudishiwa internet???,
Au ilirudi tu yenyewe!!
 
kushindwa kwa marekani kuishambulia korea kaskazini ni kutokana na madhara makubwa yatakayotokea korea kusini kwa kipindi kifupi sana pale vita itakapoanza. kuna uwezekano kutokea kwa vifo vya raia wa korea kusini 2400 kwa saa idadi inayoweza kufikia 64,000 kwa siku.
Idadi kubwa ya vifo vya raia ndiyo inayosababisha marekani kusita kuingia vitani na korea kaskazini
 
kushindwa kwa marekani kuishambulia korea kaskazini ni kutokana na madhara makubwa yatakayotokea korea kusini kwa kipindi kifupi sana pale vita itakapoanza. kuna uwezekano kutokea kwa vifo vya raia wa korea kusini 2400 kwa saa idadi inayoweza kufikia 64,000 kwa siku.
Idadi kubwa ya vifo vya raia ndiyo inayosababisha marekani kusita kuingia vitani na korea kaskazini
Hiyo siyo sababu hata kidogo.
Walipokuwa wanapanga kuishambulia NK hawakujua hilo?
 
wana hicho kikosi chao kinadili na Cyber wars kinaitwa Unit 121 au Bureau 121 ni hatari sana hawa jamaa wana akili za ajabu kama alliens

wana ujuzi wa juu sana wa masuala ya computer afu wapo kwa makadirio kama 1700 tu ktk kikosi hiki ila shughuli yao ndo hatare

nawasilisha
Tz nasi tunacho kitengo kama hiki au hatuna?
Nalog off
 
Back
Top Bottom