Sinoni
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 6,188
- 10,666
Kiongozi wa Korea ya Kaskazini amesema kuwa, nchi yake haitatumia silaha za nyuklia lakini endapo itashambuliwa, basi itatumia silaha hizo kwa ajili ya kujilinda.
Kim Jong-un kiongozi kijana wa Korea Kaskazini amesema hayo mbele ya wajumbe wa kamati kuu ya chama tawala mjini Pyongyang na kusisitiza kwamba, jeshi la nchi hiyo litatumia silaha hizo za nyuklia kulinda uhuru wa taifa hilo pindi utakapokabiliwa na tishio.
Aidha Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini amesema kuwa, nchi yake itaanza kufanya mazungumzo na mataifa yaliyokuwa mahasimu wao hapo awali.
Vyombo vya habari vya taifa hilo vimemnukuu kiongozi huyo akiambia baraza Kuu la chama kinachotawala nchini humo kwamba, kunapaswa kuwepo mashauriano zaidi na Korea Kusini ili kuimarisha uelewano na kuaminiana.
Kim Jong-un aliitaja Marekani kuwa ni jambazi mkubwa duniani na kwamba, kuashiria maneva ya kijeshi yasio na mfano nchini humo na kusema kuwa, maneva hayo yanafanyika kwa lengo la kukabiliana na serikali ya kijambazi ya Marekani na mwitifaki wake yaani Korea Kusini.
Mara kadhaa serikali ya Korea Kaskazini imetisha kushambulia Marekani na Korea Kusini kwa mabomu ya kinyukilia