Mbalamwezi1
JF-Expert Member
- Dec 20, 2013
- 2,073
- 2,024
KONGWA NA URAIS WA MSUMBIJI
[URL='http://www.habarileo.co.tz/images/Non-Frequent/handaki-kongwa.jpg']
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana akijiandaa kuingia ndani ya handaki alilotumia kujificha Samora Machel.
[/URL]
AMINI usiamini, huo ndio ukweli, mtu anayetaka kugombea au kuwania urais nchini Msumbiji, lazima afike Kongwa kuomba baraka za kupata ushindi katika kinyang’anyiro hicho.
Utamaduni huo, umekuwa ukifanyika kila wakati kwa viongozi wa Msumbiji kufika mahali hapo, umbali wa kilometa 2.5 kutoka Kongwa mjini. Makao makuu ya wilaya yaliyopo umbali wa kilometa 85 kutoka mjini Dodoma, ni mahali ambapo wapigania uhuru wa nchi mbalimbali za kusini mwa Afrika, waliishi kwa muda mrefu wakipanga mikakati ya namna ya kuzikomboa nchi zao.
Kwa nini wagombea hao kupitia chama cha ukombozi cha Frelimo, walifika hapo?
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kongwa, ambaye pia ni diwani wa eneo hilo, White Zuberi anamwelezea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana sababu yake. “Wanafika hapa kupiga magoti na kuomba baraka za ushindi kwa wapigania uhuru waliotangulia mbele ya haki waliolala mauti mahali hapo.” Marais wa Msumbiji ukiacha Samora Machel (1933–1986) aliyeishi hapo na baadaye kwenda kuipigania Msumbiji, wengine wote wamekuwa wakifika kuomba baraka za wenzao waliolala mauti kutokana na shida mbalimbali kabla ya kwenda kupigania uhuru nchini kwao.
Marais Joaquim Chissano, Armando Guebuza na wa sasa, Filipe Nyusi, kwa nyakati tofauti kabla ya kuingia kwenye kinyang’anyiro, wamekuwa wakifika mahali hapo na kupiga magoti makaburini na kurudi kwao kugombea na wanashinda. Wanafika hapo na kusafisha makaburi, kuangalia majina ya waliotangulia na kuomba dua au sala zao na kurudi nchini kwao na kushinda uchaguzi katika nchi yao.
Kitendo hicho cha kufika Kongwa, kinatambulisha wazi kuwa, ushindi wa kiongozi wa chama cha Frelimo, unatokana na imani kwamba amepata baraka za wapigania uhuru waliomwaga damu kabla yao wakati wakiiandaa nchi kuwaondoa wakoloni Wareno. Mkuu wa Mkoa, Rugimbana baada ya kupokea maelezo hayo na kuona jengo lililotumika kama kituo cha reli, anaingia kwenye handaki kuona mahali ambapo alikuwa akijificha Machel.
Rugimbana anapita uwanda tambarare, kibarabara kidogo kwenda mahali lilipo handaki alilokuwa akijificha kiongozi huyo. Hakuishia nje ya handaki, Rugimbana akaingia ndani kuona namna lilivyokuwa limejengwa kwa umahiri. Ni refu kama meta tano hivi, ndani yake kuna giza kiasi, lakini mwanga kutoka nje unasaidia kuakisi, lakini ni pana kiasi cha mtu mmoja kupita bila tabu.
Kima chake ni kirefu kiasi cha mkuu wa mkoa kutoinamisha shingo, limejengwa kwa saruji imara na kuna ngazi za kuingilia na kutokea upande wa pili. Handaki hilo limebomoka kidogo kwenye mlango wa kuingia na kutokea, lakini bado linatanabaisha kwamba muasisi wa chama cha Frelimo, Machel alitumia kwa ajili ya kujificha. Handaki hilo lipo umbali wa meta 500 kutoka nyumba aliyokuwa akiishi, bado linaonekana vizuri ukiwa karibu, ukiwa mbali unaweza kudhani ni kichuguu kidogo.
Mkuu wa Mkoa pia akatembelea nyumba ambazo inasemekana awali zilijengwa kwa udongo na kuezekwa kwa makuti, zilibadilishwa na kuwa za tofali na bati, ndizo zilizoifanya shule ya Sekondari Kongwa kuanzishwa kwa urahisi. Nyumba hizo zimeendelea kutunzwa kutokana na kuwapo kwa Shule ya Sekondari Kongwe inayotumia majengo yote ya wapigania uhuru, isipokuwa moja ndilo imejenga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kongwa, Zuberi anasema, kuwapo kwa majengo hayo kulisaidia kuifanya shule hiyo ianze kwa urahisi kwani mengine yanatumika kama madarasa na mengine ni nyumba za walimu. Pamoja na Msumbiji ambayo ilipata uhuru Juni 25, 1975, nchi nyingine ambazo zilitumia majengo hayo kwa ajili ya kupigania uhuru wa nchi zao ni Namibia.
Wapigania uhuru wake, nao walikuwapo hapo kwa miaka mingi, wakijiandaa kuikomboa nchi yao kutoka kwenye makucha ya makaburu, hivyo Sam Nujomba na chama chake cha Swapo, walianzia harakati zao katika eneo hilo. Nchi nyingine, Zimbabwe inayoongozwa na Robert Mugabe, pia wapigania uhuru wake walikuwapo hapo Kongwa wakijiandaa kukomboa nchi zao na zikapata ukombozi.
Wapigania uhuru hao, walikaa kambini kwa siku tano na siku za mwisho wa wiki, Jumamosi na Jumapili waliruhusiwa kutoka na kwenda mjini Kongwa na kujichanganya na wenyeji. Si ajabu ukifika sasa Kongwa, ukakutana na watoto wenye damu mchanganyiko ya watu wa Msumbiji, Namibia na Zimbabwe na nchi nyingine na wenyeji, kutokana na ukweli kwamba wapigania uhuru hao walijichanganya na wenyeji.
Zuberi anasema, Kongwa ni kama ngome ya kupanga uhuru kusini mwa Afrika na ndipo mahali walipopanga mbinu za kuwaondoa na kujinasua kwenye makucha ya wakoloni nchini mwao. Kutokana na nchi nyingi kutumia Tanzania kama kituo cha ukombozi Kusini mwa Afrika, imeshiriki katika ukombozi kwa mchango wa hali na mali, ikiwamo hiyo ya kutoa makazi ya wapigania uhuru hao.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kongwa, Mussa Abdi, anasema alibahatika kucheza mpira wa miguu na Samora wakati wa uhai wake, alipokuwa akisoma shule ya kati, Kongwe mwaka 1963. Abdi anamwelezea Samora kwamba alikuwa mchezaji mzuri wa mpira wa miguu, kiasi cha kumfanya asimtoke katika kumbukumbu zake za uchezaji mpira. Wapigania uhuru hao, wameacha kumbukumbu nyingi, kutokana na ukweli kwamba walipewa mapokezi mazuri, hasa baada ya Waziri Mkuu wa wakati huo, Rashidi Kawawa kufika Kongwa na kuwaomba wawapokee wapigania uhuru kwani ni binadamu wenzetu.
Awali mwaka 1940, Kongwa ilikuwa kituo cha reli kilichojengwa rasmi kwa ajili ya kusafirisha karanga, zao ambalo lilianzishwa na wakoloni katika eneo hayo. Kati ya mwaka 1963 na 1977, Kongwa ndipo palitumika na wapigania uhuru wa nchi zilizoko kusini mwa Afrika kwa ajili ya kujiandaa kuzikomboa nchi zao. Lakini, kati ya mwaka 1982- 1993, eneo hilo lilitumiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama Chuo cha Mafunzo ya Usalama wa Kijeshi.
Eneo hilo lina ukubwa wa ekari 951, japo sasa maeneo ya pembezoni yamevamiwa na watu wanaofanya shughuli zao. Hasa eneo la ekari 79, ambazo zilitumika na watu waliokuwa wakiendesha mradi wa kumwagilia, ndilo limechukuliwa na wananchi na wanafanya shughuli zao. Mkuu wa Mkoa ameagiza halmashauri kuhakikisha wanabainisha mipaka, ili eneo hilo walipoishi wapigania uhuru lijulikane na libaki kama lilivyotengwa.
CHANZO: HABARI LEO