Kongole Ditopile kwa ujenzi wa ofisi ya CCM tawi la Mwasonga

Apr 9, 2022
66
32
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Mwasonga, wamempongeza Katibu wa Jumuiya ya wazazi wa Tawi hilo Ashura Athumani Ditopile, kwa juhudi zake za kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.

Mbali na kumpongeza kwa juhudi zake za kumsapoti Rais, pia wamemshukuru kwa kitendo cha kuwatafutia muwekezaji ambaye amewawezesha kupata kiwanja na ujenzi wa ofisi unaendelea kitu ambacho kwa miaka 30, Tawi hilo halijawahi kuwa na ofisi licha ya kuwa Tawi mama lililozalisha matawi zaidi ya sita.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari Katibu wa CCM Tawi la Mwasonga, Ndugu Mtulika Luheka kwa niaba ya wanachama wenzake amemshukuru Bi. Ashura Ditopile kwa jambo kubwa alilolifanya katika Tawi hilo.

"Ndugu yetu mwanachama mwenzetu, katibu wa Jumuiya ya Wazazi Tawi la Mwasonga, aliyoyafanya ni makubwa amewezesha tumeweza kupata mfadhili ambaye ametununulia kiwanja, na tayari tumekabiziwa hati ya Kiwanja cha Chama, toka muda mrefu sisi wanachama wa Tawi la Mwasonga takribani miaka 30, hatuna eneo la Chama ukizingatia Tawi letu ni Tawi mama limezalisha matawi karibia sita lakini sisi hatukuwa na eneo la chama", alisema Luheka.

Eidha Luheka amemshukuru Ditopile kwa upendo mkubwa kwa kuwawezesha pia kuwaletea mdhamini ambaye kama unavyooona ujenzi wa Ofisi unaendelea.

" Mpaka hapo tu Mimi kwa niaba ya wanachama wenzangu, nampongeza na ninamshukuru sana, lakini kwa nini nasema haya, tunajifunza mambo mengi sana kupitia Ditopile, kuna watu wengi wenye uwezo lakini hawana moyo wa namna hii", alisema Luheka.

Kwa upande wake Katibu wa umoja wa Wazazi Tawi la Mwasonga, Ashura Ditopile ambaye ni Mwekezaji Kata ya Kisalawe tu, amemshukuru Mungu kwa juhudi binafsi za kumtafuta Mfadhili na kujenga ofisi ya chama katika Tawi la Mwasonga , ambao ujenzi wake unaendelea.

"Nimefanya jitihada hizi ili nimsapoti na kumuunga mkono Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan", alisema Ditopile.

Ameeleza kuwa katika kile ambacho yeye anakipambania katika kujenga Nchi yetu, yeye atahakikisha anamuunga mkono Rais kwa kila jambo.

" Nipo tayari kutumika kwa kila jambo ambalo yeye analitaka, akiitaji kututumia tupo tayari, tutajitahidi kufanya vile yeye anataka na tutahakikisha 2025, tunamuweka tena madarakani kwa kumsimamisha kidedea tena kwa kula nyingi", alisema Ditopile.
 
Back
Top Bottom