Kongamano la Siku Ya Uhuru UDSM Dec 9

matasha

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
378
400
UNIVERSITY OF DAR ES SALAAMAcademic Staff Assembly


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tunapenda kuwajulisha kuwa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) kwa ushirikiano na IPP Media wameandaa Kongamano tarehe 9 Desemba 2012 ndani ya Ukumbi wa Nkrumah kuanzia saa 8 mchana hadi saa 12 jioni. Mada kuu ya Kongamano ni, “Uhuru wetu na Mustakabali wa Taifa kwa Miaka 50 Ijayo”. Vipengele vya mjadala ni: a) Amani na Utulivu wa Taifa letu kwa Miaka 50 Ijayo;b) Elimu na Maendeleo ya Taifa kwa Miaka 50 Ijayo; c) Rasilimali zetu kwa Maendeleo ya Kiuchumi ya Taifa. Kongamano hilo litarushwa moja kwa moja na ITV, Radio One na Capital Radio. Wote mnakaribishwa kufuatilia mjadala huo. Wazungumzaji watakaongoza mjadala ni Bw. Maggid Mjengwa, Prof. Gaudence Mpangala, Dkt Martha Qorro, Dkt Kitila Mkumbo, Dkt Haji Semboja, na Mhandisi Joshwa Raya. Watakuwepo pia wazungumzaji waalikwa kama vile: Joseph Butiku, Dkt Aldin Mutembei, Julius Mtatiro, January Makamba, Usu Mallya na Esther Wassira. Wote mnakaribishwa Limetolewa na Uongozi wa UDASA
 
Safu iko powa nitakuwa live Luningani. Mbona Ulimwengu na Kubenea siku hizi kimya?
 
Hahaa imekaa njema sana nasubiria hu mtanange jumapili kwa hamu sana
 
Ahsante kwa kutujuza, nitaungana na wafuatiliaji wengine kujua kitakachoendelea.
 
Dah hii safi sana maana mijadala kama hii ya fikra huru ilikuwa ishapotea kitambo pale mlimani.
 
Sisi wengine tulio mbali na TV zetu tunaomba tupewe updates za kinachoendelea siku hiyo
 
Asante kwa taarifa. Ombi langu journalists watakaohudhuria wawe objective kuripoti yatakayojiri kwa mustakabali wa taifa, waweke ushabiki na itikadi pembeni. Editors nao wazipe habari hizo uzito unaostahili. Tanzania Kwanza.
 
Uhuru wa Nchi gani hiyo? ebu nyie wasomi mtwambie ukweli bwana hhhaa!




 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…