Kongamano la Katiba na Hoja ya Mnyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kongamano la Katiba na Hoja ya Mnyika

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Didia, Jan 16, 2011.

 1. Didia

  Didia JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 721
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  Katika kongamano lililoisha juzi UDSM mada kuu iligusa maeneo makuu matatu: Haja, Mchakato na Maudhui ya Katiba Mpya. Wajumbe wote walionekana kukubalina hususani na kipengele cha kwanza-Haja ambapo kila mtu alionesha kuwepo umuhimu wa kupata katiba mpya. Hivyo hapo hakuna mjadala zaidi.

  Katika kipengele cha pili kinachozungumzia mchakato yaani katiba ipatikane kupitia njia/utaratibu upi mpaka sasa kuna hoja tatu zinazokinzana. Napenda nizipe majina yafuatayo:

  1. Hoja ya Rais: Rais kuunda tume ikusanye maoni na kutoa ushauri ambao utashugulikiwa na vyombo vya kikatiba. Maoni ya wajumbe yalionesha kuwa kauli ya Rais haiko wazi na wengi wanaamini kuwa utaratibu wa tume ya Rais hautaleta matunda yenye kutarajiwa kama historia inavyoonesha.

  2. Hoja ya Mnyika: Kupeleka Hoja Binafsi Bungeni, yafanyike marekebisho ya katiba kuingiza ibara itakayo toa muongozo jinsi ya kutunga katiba mpya. Itungwe sheria inayo unda chombo cha kuratibu maoni ya wananchi......

  3. Hoja ya Shivji (tunaweza kuiita pia mtazamo wa Asasi za Kiraia): Tume ya Rais isimamie mchakato wa kukusanya maoni, iwe wazi, isiripoti kwa Rais bali kwa wananchi.
  Hoja iliyotolewa na Shivji ni kwamba Mnyika akipeleka hoja ya katiba bungeni matokeo yake huenda yasiwe mazuri ikizingatiwa wingi wa wabunge wa CCM. Mtazamo huu unaimanisha kuwa hoja ya katiba ikionekana kuwa himaya ya chama fulani patakuwepo mgawanyiko kati ya wananchi/wadau na huenda pasiwepo msukumo wa kutosha. Mapendezo yaliyotolewa ni kwamba nguvu sasa ihamie (i) kusukuma Rais aunde tume ambayo haita ripoti kwake, bali kwa wananchi. (ii) Katiba isiandikwe na Mwanasheria Mkuu bali wajumbe watakao teuliwa na bunge la mda (Constituency Assembly)


  Je, kuna haja ya Mh. Mnyika kuendeleza mchakato wa hoja binafsi? Nini itakuwa athari au faida za kupeleka hoja binafsi bungeni? Je kama unakubalina na hoja za Shivji ni mikakati gani tufanye kufanikisha hilo?


  • Kwakuwa swala lamaudhui (yaani tuwe na katiba ya namna gani ni pana sana, naomba mjadala ujikite zaidi kwenye mchakato i.e njia ipi itumike kupata katiba mpya)
  Ahsateni karibu kuchangia.
   
 2. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2011
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,212
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Kama Shivji anasema tume ikiundwa na bunge inaweza kuwa na mapungufu kutokana na ukweli kuwa CCM ndio wengi bungeni, mbona ikiundwa na Rais itakuwa imeundwa na mkuu wa CCM pekee? Hiyo hoja ni changa la macho.

  Isisahaulike vile vile kwamba katiba yetu ya sasa inasema Rais ni sehemu ya kwanza ya Bunge. Kwa hivyo, hoja ya Mnyika inashirikisha sehemu zote mbili za bunge. Anachotaka Shivji ni kuondoa sehemu ya pili ya bunge kwenye uundwaji wa tume.

  Shivji anapozungumzia tume kuripoti kwa wananchi, na sio kwa Rais au bunge ana maana gani? This is obscurantism. Kuripoti kwa wananchi ni kuripoti kwa wawakilishi wao, yaani bunge. Hata kama wabunge wengi ni wa CCM, kama wamechaguliwa na wananchi ni wawakilishi halali wa wananchi.

  Namsihi Mheshimiwa Mnyika aendelee na hoja yake, aipeleke bungeni. Ana mtazamo sahihi.
   
 3. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Msomi ni msomi tu hawezi kuangalia vitu kwa hisia, kwa fujo or political bias siku zote hutumia busara na 'commonsense', big up to Shivji. Binafsi nakubaliana nae kwa vitu vingi tu. Isipokuwa tume itakayo undwa kukagua katiba isiripoti kwa raisi wala wananchi iliripoti kwenye kamati ya bunge kama itaundwa na wao ndio wawe wakaguzi wa mwisho wa katiba, sasa tena kama upinzani hauta hakikisha wanapeleka wabunge wao wenye ujuvi wa sheria au usomi wa sayansi ya jamii wao ndio watakao kuwa hawajitendei haki wala hawatutendei haki wa Tanzania.

  Na sioni sababu ya kuandika li katiba lote upya au sijui kupoteza muda na asasi za jamii we all know, or somehow expect their demands will be in toe with their core beliefs. Katiba ya jamhuri aiko kumridhisha kila mtu bali hipo kuhakikisha usawa unatendeka as much as possible. Na kwenye katiba ya sasa kuna freedom of beliefs na uhuru wa mawazo no point ya watu wa dini tena kuwepo. Wao haki zao zipo kwenye katiba ya sasa, realistically hawa watu dini wawashe nyasi tu na ikiwezekena wafunge midomo yao mirefu watatupunguzia mengi na fujo zao sizizo na msingi bali fikra za uchoyo na kutaka kujipendelea.

  Na hamna sababu ya kwenda vijijini au kwenye miji kwenda kuwauliza wananchi wanataka nini haki zao zipo kwenye katiba tayari, kwanza watu hawa hawa ndio wanarudisha viongozi 'wezi' kupitia mfumo wa kura amna wanalo lijua asilimia kubwa, kwenda kuwauliza hawa watu ni pointless na ni kupoteza muda tu. Vilevile katiba yetu ina ambatana na human rights act (which has been adopted internationally) enough to fulfil peoples rights. Sasa sijui kwanini tupoteze muda kwenda kuuliza jamii nzima vitu ambavyo vinatoa basic rights zao vipo tayari kwenye katiba ya sasa, labda nisaidiwe kimawazo hapo.

  Matatizo makubwa ya msingi ni kwamba sheria Tanzania aifanyi kazi, teuzi zingine za raisi zina ruhusu upendeleo (kama NEC), ufujaji wa mali bila ya wahusika kusulubiwa (kwanini mahakama yetu ni dhaifu), wakurugenzi wa mashirika ya Umma wazembe (uchumi unakuwa dhaifu) na hawawajibishwi hata kama wame embezzle mali na assets design ya akina 'Katunda', amna uwazi wa asset kwa viongoozi wetu na biashara zao hili lina ruhusu watu kama kina akina RA na vigogo kujipa tenda na kununua shares kwenye makampuni yenye faida mapema (conflict of interest).

  In short the 'rule of law' hakuna na hapa ndio haki zetu zinapotea matokeo yake jamii kuvunjiwa heshima, polisi wauwaji hawafungwi wala kuwajibishwa imefikia hatua mpaka wamekuwa waporaji kama akina 'Zombe' na bado wapo mitaani, uchaguzi CCM wakiamua lao liwe linakuwa na atuna sauti ya kufanya lolote wala namna ya ku-challenge matokeo.

  Viongozi rushwa mtindo mmoja amna anaewajibishwa kwa kuliletea hasara taifa, watu wanajipa tenda za wizi na wizara zinapitisha tenda hovyo hovyo mwisho wa siku Tax payers wanatupiwa bills kibaya zaidi hawa mawaziri wana audacity ya kuja na kutupia mipira watu wengine huku wakitucheka. Sa sheria aifanyi kazi na inaleta udhaifu wa democracy na uchumi kwa ujumla.

  Lakini hii habari ya kusema katiba irudi kwa wananchi its just waste of time hivi vitu ni muhimu na ndio matatizo ya tanzania kuangalia upya kanuni na sheria zetu kikatiba na kurudisha nguvu za wananchi kupitia sheria. Na si kuangaika na watu wanaotaka katiba itakayo zua fujo tu huko mbeleni wadini, makabila, na personal issues hivo vitu vipo tayari kwenye katiba ya sasa na walale mbele tu hawa cha msingi baadhi ya haki zetu hizi pia azieshimiwi tunarudi pale no rule of law or land.

  Mwisho nimalizie katiba au kwenye kuangalia haya mambo kuna principles na mistari ya kuhakikisha usawa unapatikana vipi au unatungwa vipi a few of those lines are morality, land laws, good governance na mengine na si kila mtu kaenda shule kujifunza hayo ndio maana msomi kama 'Shivji' anaelezea umuhimu wa tume yenye experts kwanza.
   
 4. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #4
  Jan 17, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kwa maoni yangu ni kuwa Hoja ya Mnyika na Hoja ya Shivji, zote zinafanana, ila zinatofautiana tu pa kuanzia. Hoja ya Shivji ina mapungufu zaidi kwa kuwa pamoja na kubainisha tume itaundwa na raisi, lakini itakuwaje tume iripoti kwa wananchi? Tanzania ina zaidi ya watu milioni 20 (above 18), Je tume hiyo itaripoti kwao kivipi? Bila shaka ni kupitia kwa wawakilishi wao ambao ni wabunge, ambao wengi ni CCM, hivyo tunarudi pale pale. Kwa hiyo hoja za mnyika na Shivji, hazionyeshi ni kwa vipi tutaepuka wingi wa CCM katika uwakilishi.

  Binafsi naona hakuna mkato katika uundwaji wa katiba mpya. Lazima tupitie kwenye referendum (kura ya maoni)

  Kwa hiyo mi naona nitoe hoja yangu ambayo naiita Hoja ya mwendawazimu (nisieleweke vibaya, bali mi sijasoma sheria wala siijui katiba, hivyo ni kama mwendawazimu tu kwenye haya masuala)

  iv) Hoja ya mwendawazimu. Bunge la mda (Constituency Assembly) liundwe. Wananchi kupitia makundi mbalimbali ya kijamii (Taasisi za elimu, taasisi za dini, nyama vya siasa, mashirika yasiyo ya kiserikali, na serikali yenyewe) watoe maoni yao (kama waliyotoa CUF), ambayo yatajumuishwa, kujadiliwa na kuandikwa na bunge hilo la muda, kisha kutoka kwao tutapata katiba kielelezo, ambayo itapigiwa kura ya maoni (ambayo itaandaliwa na kusimamiwa na tume ya uchaguzi itakayoundwa na bunge hilo la muda). Kura itakuwa ni yes (kuikubali) au no (kuikataa), then majority watapewa ushindi.

  Bunge la muda liundwe na watu wasiziodi 13, ambao ni (mfano); mwakilishi mmoja mmoja kutoka katika kila chama chenye wabunge (6), mwakilishi mmoja mkristo, mwakilishi mmoja muislamu, mwakilishi mmoja kutoka NGOs, Mwakilishi mmoja kutoka serikalini, pengine na wengine watatu kadiri itakavyoonekana inafaa.

  Naomba kuwasilisha hoja...
   
 5. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180


  Ni mwanzo mzuri sisi tunaendelea kujifunza hapa tumepata elimu.karibuni wengine
   
 6. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Jambo langu la kwanza ni Hoja ya Mnyika;
  NAFIKIRI MNYIKA AENDELEE NA HOJA YAKE ILA KAMA ILIKUWA NI HOJA YA KUDAI KATIBA MPYA iBADILISHWE IWE HOJA YA KUDAI BUNGE LA KATIBA


  Jambo la pili ni mabadiliko gani tunayotaka

  NAAMINI TUNACHOKOSA SISI NI UTAWALA WA SHERIA TUU KWANI KILA KITU TAYARI KIPO NDANI YA KATIBA.
  Dicey alisema mambo muhimu katika katiba ambayo inatoa utawala wa sheria ni:
  1. Absence of arbitrary power;
  2. Equality before the law;
  3. The constitution is a result of the ordinary law of the land.
  The Rule of law is essentially the separation of powers between different organs of government

  TUNATAKA HAYA TUU MENGINE YATAKUJA AUTOMATICALL
   
 7. Didia

  Didia JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 721
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  Wakuu ahsante kwa uchambuzi wa kina na wenye mashiko. Nakubali kuwa Mnyika anapaswa kubadili hoja yake madai isiwe tena kudai katiba mpya maana tayari swala hilo lishajibiwa. Hoja sasa ijikite kwenye kudai mchakato
   
 8. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2011
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,423
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Kwa mara ya kwanza naomba nikiri kutofautiana na Prof Shivji! Sikuamini kama kauli ile ni ya kwake. Mwanamapinduzi anaogopa kuingia vitani kupigana, anataka kuchenga! Mnyika nenda na hoja Bungeni, kule ni vita vita tu! Nenda ukifahamu majority ya wabunge ambao ni CCM hawatapenda hoja yako. Mwanamapinduzi hapaswi kuogopa kupingwa. Pigana kiume, kwa nini udhani watapiga kura kichama katika jambo hili. Kuna kila dalili wapo walioshibishwa hoja ya kupinga, lakini wana-mapinduzi wapo pia. Tuanze nao.

  Prof Shivji, uliyenipandikiza mbegu ya uana-mapinduzi kuanzia ile mada yako ya kwanza ya Silent Class Struggle, usiogope! Kule bungeni tutashinda tu, hata kama CCM wataona ni kero hoja kuibuliwa na Mnyika. Mimi nahofia zaidi adui nisiyemfahamu. 'WANANCHI'! Hawa ni nani? Taasisis za Kiraia? Wale ambao wana agenda mmoja tu, kama ni kwamba mwanamke anaonewa basi, kwa kila kitu wataona mwanamke anaonewa, hata kama ni kuhudumiwa bia!? Au taasisi za kidini ambazo haziaminiani, kila moja anaona upande wake tu? Hujasikia taasisi za kiislamu wakaishabikia hii hoja, kwamba ni muda muafaka wa kuingiza sharia kwenye katiba? Na hujaona au kusikia maaskofu nao wamekaa kidete kupinga hii. Mada hii ni ya wakillishi tunaowafahamu....Mwache Bw Mdogo aende Bungeni.
   
 9. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,212
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Hoja ya Mnyika, ni kwamba Bunge liweke sheria itakayosimamia mchakato wa kupata katiba mpya. Bunge liamue aidha kuunda, kwa SHERIA, kamati ya kukusanya maoni, au liunde, kwa SHERIA, Baraza La Taifa La Katiba.

  Hoja ya Shivji ni kwamba Rais aunde tume ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya iweje. Hoja ya Mnyika inazingatia demokrasia, ya Shivji ni autocratic. Si sahihi kusema zinatofautiana mahali pa kuanzia tu.

  Kwa kifupi, hoja ya Mnyika ni wawakilishi wa wananchi waamue mchakato wa kupata katiba mpya uweje, wakati hoja ya Shivji ni Rais ndiye aamue huo mchakato uweje. Kuna tofauti kubwa.

  Maoni ya Shivji kwamba bungeni CCM ndio wengi kwa hivyo afadhali tume ya Rais ni mtiririko mbaya wa mawazo kwani Rais ni kiongozi wa CCM.
   
 10. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hayo maeneo ya rangi nyekundu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  Bila mwongozo wa kisheria kuupa mustakabali huu wa kitaifa nguvu ya kisheria, itabaki ni suala la hisani, au utashi wa mtu binafsi, jambo ambalo ni hatari kuliko yote!!!!!!!!!!!
  Mheshimiwa Mnyika endelea na azma yako kufikisha hoja hii bungeni ili tupate national commitment ya kisheria, na pia kuwapa wananchi nafasi ya kupima integrity ya wabunge kuhusu suala hili ambalo ni la uhai wa kitaifa kwa vizazi vijavyo, ambalo hatuhitaji kuhusisha vested interests za vyama ama makundi katika jamii. Bila nguvu ya sheria kulinda mchakato huu, kuna makundi yatateka nyara mchakato sas hivi , jambo ambalo kuna hatari ya kuzua mgogoro mkubwa sana wa kitaifa!!!!!!!!!!!!!!
  Kama suala la vyama vingi lilivyokuja-njia hiyo hiyo italeta katiba mpya-pressure kubwa kutoka ndani na nje!!!!!!!!!!
  Mimi nawaomba wabunge walipe suala hili top priority katika agenda yao ili kunusuru taifa hili!!!!!!!!! Kuna hisia za kweli kwamba jambo hili litaishia kuvutana vutana hadi mwaka 2015 unafika katiba mpya inayotamaniwa haijapatikana!!!!!!!!!!!! Hivi kumbe ndiyo maana Kenya walifuata njia ya kuchinjana kama kuchinja kuku au mbuzi-ni kwa sababu ya uvutano uliochukua miaka mingi.!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Hapa Tanzania ziko dalili za wazi,ukisoma between the lines, mijadala inayoendelea, kwamba watu usiowatarajia waki-advocate njia huria za kupata katiba mpya!!!!!!!!!!!!! Katiba Mpya inayotamaniwa na wananchi wa taifa hili ni kama kuleta risasi za moto kuwapiga na kuwaua wenye nchi hii!!!!!!!!!!!!!!! Hivyo siamini kama itakuwa rahisi na mtelemko kama invyoelekea kuaminiwa na supporters wa mchakato huria!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 11. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Kikwete hawezi kuteua wajumbe watakao wakilisha umma, the man is so biased. Ukiangalia mlolongo wa uteuzi wa kamati zake zikiwemo taasisi za serikali, kama NEC , TAKUKURU, na tume nyingine mbalimbali, historia inaonesha usanii mtupu.

  LEO HII AIBUKE NA KUTAJA MAJINA AMBAYO HAYATA-SIDE UPANDE WOWOTE? HAPA KUTAKUWEPO CHANGA LA MACHO kama vile nilivo sema mwanzo historia ya kikwete kuteua ndugu, jamaa na marafiki ndio iliyo igharimu nchi na kutufikisha hapa tulipo.

  So Mnyika pambana nchi iko kwenye RIP
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Jan 20, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  ..mnakumbuka tume ya afrika mashariki?

  ..wa-Tanzania walitoa maoni yao kupinga suala hilo.

  ..Tume ikachakachua maoni yao ni kupelekea bungeni mswada uliowaburuza wa-Tanzania kwenye eac.

  ..Raisi akiteua Tume maana yake anaipangia hadidu za rejea na matokeo na ripoti ya tume yanakwenda kwa Raisi.

  ..baada ya hapo Raisi,Mwanasheria Mkuu,na baraza la mawaziri, wanaamua ni lipi ndani ya ripoti ya Tume lipelekwe bungeni kuundiwa sheria.

  ..nadhani kinachotakiwa ni mchakato wa wazi zaidi.

  ..pia suala la kura ya maoni kuhusu muungano ni jambo la msingi kwa wakati huu.
   
Loading...