Kibunango
Platinum Member
- Aug 29, 2006
- 8,468
- 2,349
- Thread starter
- #21
ZFA: Karume Boys itakuwa ya kudumu
Haji Mtumwa, Zanzibar
CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA) kimesema hakitoivunja tena timu ya taifa ya vijana ëU-17í Karume Boys kama ilivyokusudiwa na badala yake kuimarisha ili kuwa kikosi imara.
Akizungumza na wanahabari, rais wa chama hicho Ali Fereji Tamimu, wakati wautambulisho kocha mpya wa timu ya taifa Abdelfatah El Masqsood kutoka nchini Misri kuchukua nafasi ya kocha Badr El Din Haddad, aliyemaliza muda wake.
Rais Fereji alisema lengo la chama hicho ni kuitunza timu ya vijana kwa muda mrefu.
Hivi sasa hatuna nia tena ya kuivunja timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, na badala yake tutaiimarisha ili kuwa kikosi bora zaidi,î alisema.
Tamimu alifafanua kuwa hatua hiyo imekuja baada ya kuonyesha kiwango cha kuvutia zaidi kwenye michuano ya vijana ya Chalenji iliyomalizika hivi karibuni nchi Sudan.
Alisema timu hiyo imethibisha ubora kwa kufika hatua ya robo fainali, ishara moja wapo ya kuwa kikosi ni imara na kinahitaji kupewa misingi tu.
ìKufika hatua ya robo fainali ni jambo la kujivunia kwa vijana wetu na soka ya visiwani hapa kwa ujumla kikubwa kinachohitajika hivi sasa ni kuboreshwa zaidi,î alisema.
Timu hiyo hivi sasa ipo chini ya kocha wake Hamad Moroco ilirejea nchini hapa hivi karibu kutokea nchini Sudan katika mashindano ya Chalenj, lakini ilitolewa katika hatua ya robo fainali na timu ya Eritrea kwa kuchapwa mabao 2-0.