KOMBORA KIOTANI-45

FANANI MTENZI

Senior Member
Joined
Jul 4, 2017
Posts
106
Reaction score
95
KOMBORA KIOTANI-45

BONIFACE BIRAGE


“Ni heshma kubwa kukuona mheshimiwa rais Serambovu.Umefanya kazi nzuri.Kutana na THE BIG BOYS.”alitamka mmoja wao.

Serambovu aliwatizama ulimi ukawa mzito kwa upande wake.

“Kuna machache lazima utakuwa huyajui.Tumeamua kujitokeza kabla hujatoa hotuba.Sisi ni kundi maalum tunashiriki biashara kubwa dunian za uuzaji mafuta.Tuna mpango wa kusambaza mafuta duniani kote kwa takribani miaka 50 hijayo.Taifa lanu lina mtaji huu.Ndo maana tumewekeza fedha nyingi sana.Unachotakiwa kufanya nikuishikilia serikali yako vilivyo nchi yenu inatakiwa iwe kwenye kamtikisiko wa kisiasa ili wazawa wasiwe na muda kuangalia rasilimali.Nakuhakikishia kuna mengi tutayatekeleza nchini mwako ila uwe makini sana.Tutakupa back up ya kutosha.Kuna kipindi kigumu utapitia lakini tutakusaidia kuwatambua wasumbufu na kuwanyamazisha.”alisema bwana Yule akiwa kavalia mawani ya macho.

“Tulitengeneza visa vyote kwa kushiriikiana nanyi mliweza kufanikisha ghasia nchi haikupoa na sasa tumefanikiwa tena kumuondoa Kilua.Hii ni zamu yako.Pesa usiiwaze ipo ya kutosha kwaajili yako.Utaendesha nchi kawaida ila tu maslahi yetu uyachunge kwa kutukingia kifua.”aliongeza mwingine.

“Naweza kuyajua majina yenu?”
“Sisi ni big boys team.Hata kufanikiwa kuiona sura yetu ni bahati kubwa sana kwako.Unasimama mbele ya timu mahiri sana ya wafanyabiashara.”mwingine alitamka.

“Lakini mabwana mtanihakikishia vipi usalama wangu?”

“Tuna vikosi vya kutosha.Pesa ipo tunachoangalia ni mwanya wa sisi kupata hayo mafuta.”

Serambovu alihisi ujasiri ukimwingia,”Mlifanikisha haya mapinduzi?”
“Sema tulifanikisha wote maana una husika.Sura yako ndo itakuwa inaulizwa sana.Kuna viapo utatakiwa kula katika muungano huu pamoja nasi.Kumbuka unapoingia hakuna kutoka.”alisema Yule bwana.Kisha akawageukia waliokuwepo kuwapa ishara watoke.Wameingia hadi ikulu kumaanisha walikuwa na uwezo wa kuingia nakutoka.Sasa ilibaki jambo moja tu kumsimika Serambovu kuwa rais mpya wa taifa hilo.

Walipishwa halafu wakaingia wengine wawili wakiwa na mkoba.Waliuweka kwenye meza.Kisha wakamsogelea Serambovu.Mmoja alimpa ishara ya kumpa mkono.Serambovu alitii nakumpa mkono.

“Mpango wetu no kundi chache kuwaongoza wengi na wewe utasimikwa leo kuwaongoza wenzako.Kiapo hiki ni cha damu.Binadamu wote tuna asili ya kuamini kitu kwa kula yamini.Kiapo unachokula leo kitakuwa imani yako ingawa utahitajika kufanya mambo mazito lakini na hakika kwa kiapo hiki utakuwa jasiri sana na utaweza kutusaidia sisi.”alisema moja ya watu wale.Serambovu alitikisa kchwa.Yule aliyemshika mkono alichomoa kisu anakumkata kwenye ncha ya kidole kidogo kisha akashika kidole kile nakukata kuanzia kwenye ukucha.Aakata chote nakuelekezwa asipige kelele.Damu zilipokuwa zinavuja walizikinga kwenye kikombe Fulani hivi.Kilionekana kikombe cha miaka mingi chenye rangi ya dhahabu.

“Damu yako imetiririka katika kikombe hiki ishara yaw ewe kujiunga nasi.Kidole chako hakipo chote kumaanisha sehemu ya mwili wako ipo nasi.Sisi wote tulikatwa.Inatakiwa uyavumilie maumivu hayo yatapoa.Kila utakapoona kidole chake kimekatwa utakumbuka kiapo hiki.Sasa utasoma maneno haya kwenye karatasi kimoyomoyo.”

Serambovu alikuwa akiugulia maumivu huku akiwatukana watu wale kimoyomoyo akiwatukania mama zao.Alisoma maneno yale kimoyomoyo nakula yamini akawa amejifumba rasmi katika kifungo cha The big boys.Sasa alikuwa mshirika tayari aliyeiweka nchi yake rehani.Kumbe kule kutikiswa kote akajua mpango ulikuwa rasilimali za taifa hasa hayo mafuta.Alijua katika bara lake kuna utajiri mkubwa lakini watu wamekuwa wakiteseka sana katika kuudhibitisha utajiri huo.Sasa kibarua kilikuwa kikubwa kwake.

“Hatimaye umekuwa mmoja wetu.Karibu katika timu.Hakikisha huwataji wenzako hovyo.Usifanye makosa na kila uamuzi lazima upitie kwetu.”walimwambia.Serambovu aliitikia kwa kutikisa kichwa maumivu yalikuwa makali.Alipewa kitambaa kufunika kidonda chake.

“Pumzika kidogo usije ukaenda kusoma hotuba ya kutangaza Kilua kafa huku una maumivu.Nenda pale ukiwa soba.”walimwambia.

“Kontena mshechukua?”
“Ndiyo.Vijana wetu kwa sasa wanatafuta wafuasi wa Kilua nakuwanyamazisha ni hatua ngumu lakini tutafanikiwa.Baada ya muda utasikia watu wamepotea hovyo na wengine wamekutwa wamekufa.”alisema mwingine.

Serambovu alihisia maumvi kisha akabeba karatasi ya hotuba nakutoka ofisini kwa rais Kilua.Walinzi walimpokeaa.Wale watu wane waliondoka pamoja naye.Serambovu alitoka hadi kwenye ukumbi wa ikulu.Waandishi wa habari walikuwepo.Akatoa karatsi yake nakuanza kulihutubia taifa lake.Kiota ilikuwa mikononi mwake sasa kibarua ni kuwajuza wananchi.

***

Kulikuwa na maandamano makubwa taifa zima baada ya Serambovu kujitwalia madaraka akidai rais Kilua amefariki dunia kwenye ajali.Ajali ya raisi Kilua kuna ambao walirekodi kisadfa na tayari video kadhaa zilikuwa zimesambaa kila pembe kutaka kujua nini kimeeendelea.Ilikuwaje Serambovu ajiamulie kuwa rais?Vikosi vya usalama vilikuwa kila kona kutuliza maandamano hayo.Watu waliuawa ilimradi kuusimika utawala mpya wa Serambovu ambao hadi muda huo haukuwa na uhalali kisheria kama kweli atawale au la!Kibarua kilikuwa kigumu sana.Alijaribu kuwatuliza lakini hali ikawa tete.Simu mbalimbali zilipigwa ikulu zikitaka kujua yu wapi rais Kilua.Mwili wake upo wapi?Serambovu alijitahidi kutoa muongozo lakini hali ikawa tete.Maandamano yalisheheni kila kona.

Wafanyakazi wa sekta mbalimbali waligoma kufanya shughuli zozote hadi pale watakapojua hatma ya rais Kilua.Kulikuwa na taarifa ya mume wa rais Kilua kumuua mtu aliyeitwa Twalipo muda mfupi baada ya taarifa ile ikafuatia taarifa ya Kilua kupatwa na ajali akiwa kwenye msafara wake.Mgongano wa matukio hayo ulikosa majibu kabisa kwamba ni kitu gani kimefanyika.



TAMATI
MSIMU WA KWANZA
USIKOSE MSIMU WA PILI
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 49
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…