Komboa fikra zako uokoe wakati wako

Komboa fikra zako uokoe wakati wako

uvugizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,351
Reaction score
1,100
Watu wenye chuki tamaa, masengenyo , uongo , magomvi , wanaolia kuwa maisha yamebana niligundua ni Mashuhuri sana wa kupoteza muda na bila kujua wanaupotezaje huo Muda

Unaweza kukuta kijana ana mipango lakini kila mwaka ana update mipango yake tu kwa kutiwa moyo na maneno ya inspiration ni Mengi kuliko vitendo , yaani anapenda kusikia halafu anahisi kama amefanya bila kuchukua hatua.
mfano, hujawahi kuona mtu anasema nikipata million kadhaa nitakuwa tajiri , lakini ukimuangalia kama umejifunza zile akili 3 za mwanadamu , huchelei kusema hizo ni ndoto za mchana , maana umaskini na utajiri haupo katika hela ni kichwani.

Hapo mwanzo Mungu aliumba Muda kwanza kabla ya kitu chochote. Ukitaka utajiri anza na Muda , tumia muda wako vizuri kabla muda haujakutumia , kama wastaafu wengi wanayopitia ni kwamba hawakutumia muda wao vizuri katika mipango yao kabla ya kustaafu, walitumia kwenye kile walichokistaafia na ndiyo maana wengi huwa nawashauri warudi katika fani zao kwa style yao kwa ajili yao,(sustenance).

Shetani alitumia muda mchache sana kuharibu maisha ya Adam na Eva pale bustanini

Tatizo watu wengi wanatumia muda vibaya hasa sehemu ambayo sio sahihi .

Kupoteza muda ni kung'ang'ania na kufanya jambo ambalo sio lako na ukatumia muda na nguvu zako zote katika sehemu hiyo . kumbe wewe ni mzuri wa kuongea kwa nini usiende kujifunza public speaking /inspirational speaker , ukawa hata MC wa masherehe ukapiga hela.

Shetani huteka fikra za mtu na anajua kitu gani Mungu aliweka kwako ,tangu kuzaliwa kwako , hivyo anakufanya upoteze Muda 24/7.

Komboa fikra zako ili uweze kukomboa wakati wako.
 
Mkuu unakunywa kinywaji gan... Ongeza hapo bill yangu..

Umeongea vyema sana matendo ni zero kabisa.
 
Back
Top Bottom