Kombe la Mataifa Afrika kitendawili

Kombe la Mataifa Afrika kitendawili

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,158
Reaction score
64,499
140829095452_african_cup_of_nations_2015_304x171_caf_nocredit.jpg

Morocco ni mwandaaji wa Michuano ya Kombe la mataifa Afrika 2015

Serikali ya ufalme wa Morocco itakutana na maafisa wa shirikisho la soka barani Afrika,CAF kwa ajili ya kufanya uamuzi kuhusu kuahirisha fainali za kombe la mataifa ya Afrika au la kwa sababu ya mlipuko wa ugonjwa wa ebola katika nchi za Afrika magharibi.


Morocco imesema haiko tayari kuandaa mashindano hayo kwa hofu ya kusambaa kwa ugonjwa huo.


CAF inataka michuano hiyo ifanyike kama ilivyopangwa ifikapo mwezi Januari na Februari mwakani.


Hata hivyo imeomba nchi nyingine saba kama wataridhia kuwa waandaaji mbadala,lakini mpaka sasa hakuna hata nchi moja iliyojibu ombi hilo.
Morocco ilipendekeza michuano iahirishwe mpaka mwezi Juni mwakani.Mia

Chanzo:BBC
 
Kwa upande wangu naona Morocco wako sahihi,huu ugonjwa ni tishio na ukizingatia unakusanya mataifa mbalimbali upo uwezekano mkubwa wa maambukizo kuenea.
 
140829095452_african_cup_of_nations_2015_304x171_caf_nocredit.jpg

Morocco ni mwandaaji wa Michuano ya Kombe la mataifa Afrika 2015

Serikali ya ufalme wa Morocco itakutana na maafisa wa shirikisho la soka barani Afrika,CAF kwa ajili ya kufanya uamuzi kuhusu kuahirisha fainali za kombe la mataifa ya Afrika au la kwa sababu ya mlipuko wa ugonjwa wa ebola katika nchi za Afrika magharibi.


Morocco imesema haiko tayari kuandaa mashindano hayo kwa hofu ya kusambaa kwa ugonjwa huo.


CAF inataka michuano hiyo ifanyike kama ilivyopangwa ifikapo mwezi Januari na Februari mwakani.


Hata hivyo imeomba nchi nyingine saba kama wataridhia kuwa waandaaji mbadala,lakini mpaka sasa hakuna hata nchi moja iliyojibu ombi hilo.
Morocco ilipendekeza michuano iahirishwe mpaka mwezi Juni mwakani.Mia

Chanzo:BBC
Wapi MH. JAMAL MALINZI achangamkie fulsa hiyo!!!!!!!
 
Back
Top Bottom