Kolabo ya Lil Wayne & Chris Brown featured by MB Dogg hivi ni kweli jamani?

TEKNOLOJIA

JF-Expert Member
Jan 6, 2014
4,305
2,562
Leo hii ndani ya XXL ya Clouds FM msanii MB Dogg amethibitisha kwamba mpango wa kuwashirikisha wanamuziki mashuhuri kutoka Marekani Lil Wayne na Chris Brown ktk wimbo wake upo na wanatarajia kufanya kolabo mwezi June mwaka huu.

Mh siamini niliyoyasikia au labda jamaa ana_joke flani hivi. Yaani aipate hii nafasi adimu ambayo hata P-SQUARE na umaarufu wao wote wameshindwa kuipata?

Mmmh haya bhana!

==========

Update:
Uongozi wa MB Dog wadai kumtafutia kolabo na Chris Brown

Meneja wa Q Chief na MB Dog, QS J Mhonda amemuongeza Chris Brown kuwa miongoni mwa wasanii kutoka Marekani watakaofanya kolabo na MB Dog baada ya miezi michache iliyopita kumtangaza Lil Wayne.

MB-Dog.jpg


Akizungumza na 255 katika kipindi cha XXL cha Clouds FM, Mhonda alisema anashukuru Mungu mpaka sasa mazungumzo yanaenda poa.

“Tumepiga hatua na tunatarajia labda kwenye mwezi wa sita kolabo itafanyika ni vitu tu vya kukamilisha hasa hasa taratibu zao,” alisema.

“Tumefikiria tusimchukue tu Lil Wayne tunafanya mpango tumpate na Chris Brown ili iwe vyema. Kwahiyo mpaka sasa hivi tupo kwenye mazungumzo mwezi wa sita kuangalia waje au tufanye mpango MB Dog aende au kuwaleta Lil Wayne na Chris Tanzania ili wafanye show halafu wafanye kolabo, kwahiyo kati ya hivyo tutaangalia nini kati ya hivyo tunaweza kukifanya,” aliongeza.

Hadi sasa Mhonda ameshatumia kiasi kikubwa cha fedha kuwarudisha MB Dog na Q Chief.

Chanzo: Bongo5
 
Vijana acheni kuvuta asubuhi asubuhi bila ya kupata chai kwanza. Nilimsikia mwingine juzi anasema alisoma na Obama South Africa. Chonde chonde, bangi ni dawa sio kiburudisho.
 
mh,ngumu kumeza ila tusimalize maneno wadau,tuvuteni subra huwenda anamaanisha kabisa anachokisema,you never know ametumia njia gani mpaka kufikia uko!it is just a matter of time,in shaa allah!
 
Leo hii ndani ya XXL ya Clouds FM msanii MB Dogg amethibitisha kwamba mpango wa kuwashirikisha wanamuziki mashuhuri kutoka Marekani Lil Wayne na Chris Brown ktk wimbo wake upo na wanatarajia kufanya kolabo mwezi June mwaka huu.Mh siamini niliyoyasikia au labda jamaa ana_joke flani hivi.Yaani aipate hii nafasi adimu ambayo hata P-SQUARE na umaarufu wao wote wameshindwa kuipata?Mmmh haya bhana!!!??

Nothing impossible under the sun,,,,let's wait
 
uongooo yani mb doggi akipiga tu kolabo hata na Davido nakunya hadi kenya, tena ndo apige collabo na chris brown aki ya nani NEVEEER, Samahanini lakini
 
Leo hii ndani ya XXL ya Clouds FM msanii MB Dogg amethibitisha kwamba mpango wa kuwashirikisha wanamuziki mashuhuri kutoka Marekani Lil Wayne na Chris Brown ktk wimbo wake upo na wanatarajia kufanya kolabo mwezi June mwaka huu.

Mh siamini niliyoyasikia au labda jamaa ana_joke flani hivi.Yaani aipate hii nafasi adimu ambayo hata P-SQUARE na umaarufu wao wote wameshindwa kuipata?

Mmmh haya bhana!

aaaah! kuna vitu ambavyo ukiambiwa kama ulikuwa unaangalia TV unazima halafu unakwenda kulala, ndiyo kama hii.
Sina uhakika Lilwayne na Chriss kama watakubali kufanya Collabo.
 
Kwani ili uwashirikishe ufanyeje maana wote mnasema haiwezekani bila kutuambia kwanini haiwezekani na ili iwezekane unafanyaje ??????????? ( tuongee kwa hoja sio kama walevi wa mataputapu ndio mantiki ya uwepo wa JF)
 
Back
Top Bottom