BilioneaPATIGOO
JF-Expert Member
- Jun 23, 2012
- 12,320
- 11,345
Huoni hata mkorogo umekataa.Kumbe jamaa ni wa enzi za mwalimu !!!!! 1956 si wa leo.
Hahah katulia mkuu muangalie vizuri mzee mzima kazimikaMbona kale kadem kaimbaji anakokadinya kamepigwa pasi?
Naona itamalizwa juu kwa juu mana hamna kinachoendeleaIle kesi yake ya Kenya ilifikia wapi
Jina lake halisi anaitwa Antoine Christophe Agbepa Mumba alizaliwa 13 July 1956),anajulikana zaidi kama Koffi Olomide, ni mkongo ambae anaimba mziki aina ya soukous, pia ni dansa mzuri, mtayarishaji mziki na composer.
Ana ngoma za dhahabu zilizotingisha sana katika career yake ya mziki. Ni muanzilishaji wa kundi la Quartier Latin International orchestra ambalo lilikua na wasanii mahiri kama Fally Ipupa na Ferré Gola.
Mimi namuitaga mzee wa mizigo [emoji23][emoji23][emoji23]...sijui mizigo yake kwenye video zake hua anawatoa wapi mana wanakuaga mizigo haswa halafu hua anawabambia haswa (sijui kama wanatokaga salama) [emoji2][emoji23][emoji23] kama video ya Etoile d'etat kwa sasa anaimba na kale kadada kana saut nzuri kinoma kanaitwa nani tukumbushane hapo chini....nasikia kua ni mtu wake kwa sasa, demu alimkomalia akamwambia kua asimchezee chezee tu amtumie kama wanawake wengine naona jamaa akamywea so anagonga kistaarabu (tetesi) .
Koffi hajachuja na hana mpango wa kuchuja nakumbuka tokea nasoma primary jamaa yuko kwenye gemu hadi sasa...ngoma yake ya LOI tulishindanishwa na watoto wengine kipind hicho kama kumi tuicheze ngoma ya LOI kama wanavocheza hahah nkashika nafas ya pili nakumbuka nilipewa zawadi ya keki [emoji23][emoji23][emoji23].
Ila kuna member mmoja humu nahis amekaa zaire sana au anaujua mziki wa zaire na wanamuziki wake, alitoaga thread nafikiri ya wanamuziki wa kongo na mambo yao ya black magic wanayotumia, kofi naye alimsema "u-black magic wake".
Anyway mwenye chochote aweze kuongezea kwa huyu mfalme wa mizigo [emoji23][emoji23][emoji23]...unakumbuka nini enzi hizo unapomsikia koffi olomide. Kuna kipindi nikiwa mdogo nilisoma gazeti moja liliandikwa hivi katika kichwa cha habari "USIMUONESHE MKEO KOFFI OLOMIDE" [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
View attachment 427355
View attachment 427356
Hebu ENDELEA .....Uchambuzi mzuri wa kumuhusu ' Large Degaire ' Koffi Olomide na hongera sana kwa hilo Mkuu ila tambua ya kuwa hata kama ana uwezo gani ila katika fani yoyote ile kama huna ' nidhamu ' ni kazi bure. Koffi Olomide anasumbuliwa mno na ' ulimbukeni ' hasa baada ya kuwa ni Mtoto aliyekulia katika familia ya kimasikini na kuishi kimasikini vile vile mpaka alivyopata Pesa ndipo akaanza ' kubadilika ' na ndiyo maana hata afanyeje huwa ' hafurukuti ' kwa lolote au chochote kutoka kwa Vijana waliokulia katika ' utajiri ' akina Jean Bedele Tshituka Mpiana na Ngiama Makanda Werrason ambao wao ' mziki ' hawafanyii ' dhiki ' au ' shida ' hasa ukizingatia wote Baba zao walikuwa ni ' Mabalozi ' wa nchi kubwa za Ulaya enzi za Rais Mobutu Seseseko Kuku Wa Zabanga ' Le Grand Leadear '. Na anachokifanya sasa Koffi Olomide ni kuiba tu Wanamuziki wa akina Wenge Musica BCBG na Wenge Musica Maison Mere lakini kinachomuumiza na kumshangaza ni kwamba kila ' akinyakuwa ' Wanamuziki ' mahiri ' huko akina JB Mpiana na Werrason wanaingia ' chimbo ' na kuibua vijana wapya kabisa ambao huja kuwa ' moto wa kuotea mbali ' na ' tishio ' pia.
Mfano Koffi Olomide alimnyakuwa ' Drummer ' maarufu sana wa Wenge Musica BCBG ya JB Mpiana aitwae Titina Alcapone ' Le Grand Prete ' ila muda mfupi tu JB Mpiana akaibua ' fundi ' wa kuzikaanga ' chips ' ama ' drums ' aitwae Seguen Mignon a.k.a Maniata ambaye kwa kweli amemfunika vibaya mno Titina na sasa ' kapotea '.
Hakuishia tu hapo bali Koffi Olomide akaendelea na ' upuuzi ' wake ambapo safari hii akaenda katika bendi ya Werrason ya Wenge Musica Maison Mere na ' kumnyakua ' kwa ' jeuri ' Rapa au Fundi wa ' kughani ' wenyewe Wakongo huwaita ' atalakus ' na Wafaransa huwaita ' animateurs ' aitwae Rwinga Keps au kwa jina ' maarufu ' la muziki alijulikana sana kama ' Brigade Sabateur ' ambapo baada tu ya kumchukua Werrason hakuchelewa na mara moja akaenda kukiibua ' kifaa ' kimoja ' matata ' katika ' kurapu ' aliyekuwa akiitwa Celeo Mozami Muviu au kwa jina maarufu anaitwa ' Stramme ' ambaye alikuja kumfunika vibaya sana Brigade na hadi sasa kapotea.
Hata hivyo kwa faida yako Mkuu Koffi Olomide ni mzuri tu wa kuimba miziki hii ya ' Video ' ila wenye ' shughuli ' yao hasa katika ' live ' perfomances Congo nzima hakuna anayewafunika Wenge Musica BCBG ya JB Mpiana na Wenge Musica Maison Mere ya Werrason na ndiyo maaana hata Kampuni kubwa kabisa ya ' Kilevi ' kinachopendwa Congo nzima kiitwacho ' PRIMUS ' imeingia ' mkataba ' nao mnono lakini kwa Koffi Olomide ' wamesitisha ' baada ya kuona kuwa hana ' mashabiki ' wengi anapokuwa anapiga katika concerts zake sehemu mbalimbali duniani.
muda mwingine inatokea tu anawadinya hata wembamba ila ye ni mzee wa Mizigo kama Sheikh KipozeoMbona kale kadem kaimbaji anakokadinya kamepigwa pasi?
Uchambuzi mzuri wa kumuhusu ' Large Degaire ' Koffi Olomide na hongera sana kwa hilo Mkuu ila tambua ya kuwa hata kama ana uwezo gani ila katika fani yoyote ile kama huna ' nidhamu ' ni kazi bure. Koffi Olomide anasumbuliwa mno na ' ulimbukeni ' hasa baada ya kuwa ni Mtoto aliyekulia katika familia ya kimasikini na kuishi kimasikini vile vile mpaka alivyopata Pesa ndipo akaanza ' kubadilika ' na ndiyo maana hata afanyeje huwa ' hafurukuti ' kwa lolote au chochote kutoka kwa Vijana waliokulia katika ' utajiri ' akina Jean Bedele Tshituka Mpiana na Ngiama Makanda Werrason ambao wao ' mziki ' hawafanyii ' dhiki ' au ' shida ' hasa ukizingatia wote Baba zao walikuwa ni ' Mabalozi ' wa nchi kubwa za Ulaya enzi za Rais Mobutu Seseseko Kuku Wa Zabanga ' Le Grand Leadear '. Na anachokifanya sasa Koffi Olomide ni kuiba tu Wanamuziki wa akina Wenge Musica BCBG na Wenge Musica Maison Mere lakini kinachomuumiza na kumshangaza ni kwamba kila ' akinyakuwa ' Wanamuziki ' mahiri ' huko akina JB Mpiana na Werrason wanaingia ' chimbo ' na kuibua vijana wapya kabisa ambao huja kuwa ' moto wa kuotea mbali ' na ' tishio ' pia.