Kodi zipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kodi zipi?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Amoeba, Aug 29, 2009.

 1. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  salaaam waku! bila kuisahau mizimu ya mababu inayowezesha uwanja huu
  kuendelea kkufanya kazi. naulizeni hiv, nikiagiza gari toka japani, ni kodi zipi na kwa percent ngapi ambaazo zitanipasa kulipa mpaka kukfikia kuliweka barabarani. pia kuna tetesi kuwa waalimu wanasamehewa baadhi ya kodi wakiagiza magari, mke wangu ni mwl. mwenye uhakika na hilo anipe details hapa kwa faida ya wote.
   
 2. d

  dullymo Senior Member

  #2
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 21, 2009
  Messages: 107
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  bro, kodi za magari inategemea na CC ya gari, mwaka wake wa first registration na vitu vingine. kwa gari ndogo ambayo haizidi miaka 10 from the first registration yenye CC 2000 au chini ya hapo kodi yake ni kama ifuatavyo. unachukua CIF price ya gari kisha unazidisha na import duty (20%) + VAT (25%) + 5% ambayo huwa ni registration ya gari. but iwapo gari yako itakuwa zaidi ya miaka kumi na ina zaidi ya CC2000 kodi yake itakuwa
  20% + 25% + 5% + excess duty (25%) + uchakavu 20%
  NB: kodi zetu huwa zinachange kila baada ya muda mfupi mfano kwa sasa nasikia vat ni 18% kutoka 25%.
  mabasi na gari za mizigo hazina excess duty wala kodi ya uchakavu.
  gd day
   
 3. Mama Subi

  Mama Subi Member

  #3
  Aug 29, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 88
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  Ni kweli VAT imebadilika ilikua 20% sasa ni 18%.
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Aug 30, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Hakuna utaratibu kamili ya kodi ya kuingiza bidhaa nchini. Unatakiwa uongee vizuri na afisa yeyote wa kodi ya forodha.
   
 5. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mama Subi!
  Usinichekeshe kodi hapa Tanzania sijui niite ni mdumange au mdundiko kwani sifahamu ngoma ya kwao Mustafa Mkullo.

  Mwaka jana VAT ilikuwa 20% . Wale wapumbavu wakaenda dodoma mwezi wa sita wakafanya marekebisho wakatudanganya wanapunguza ikawa 18%. lAKINI kinyemela kwenye bei ya umeme wakaongeza kodi 3% kwa ajili ya umeme vijijini ukijumlisha na ila ya EWURA 1% utaona kodi imeongezeka na kufikia 22% from 20% sasa kama Watanzania sio mataahira wanashangilia budget hiyo hovyo actually imekula kwetu wote. Stupid CCM hawana ubunifu
   
 6. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,473
  Likes Received: 1,428
  Trophy Points: 280
  ila wadau niliagiza gari kutoka japan kule nilinunua $1540 lakini ilivyofika hapa watu wa Custom wakaiambia haiwezekani ile gari iwe bei ile wakaniambia bei yao wanayoitambua ni $3500 iliniuma sana ila sikuwa na jinsi ikabidi nilipie tu, so ndugu amoeba be muangarifu
   
 7. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hiyo ilikuwa zamani sikuhizi kila kitu kipo wazi wanazo bei zote za magari ndani ya mtandao zamani watu walikuwa wana cheat bei lkn sikuhizi wanatambua mara moja kuwa bei siyo na kabla hawachukua uamuzi wa kuoongeza bei huwa wanawasiliana na gari lilikotoka kwanza,"lipa kwa manufaa ya mafisadi"
   
 8. d

  dullymo Senior Member

  #8
  Aug 30, 2009
  Joined: Aug 21, 2009
  Messages: 107
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mzee, next time ukiagiza gari ili kukwepa watu wa custom kuuplift bei, wakati unalodge documents zako ambatanisha na receipt yako ya malipo au km umenunua online ambatanisha na tt receipt ya bank pamoja na emails correspondnc wakati unanegotiate na huyo exporter.
   
 9. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #9
  Aug 31, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  siyo mizimu ya mababu inayofanya uwanja huu uendele kufanya kazi. rekebisha kauli yako
   
 10. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mawazo machafu ya wapenda rushwa ndo haya.
   
 11. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Rafiki,
  Sijaelewa vizuri kutokana na data zako hizi mkuu. Nijuavyo mimi VAT ilikuwa 20 % (now 18 %), Excise duty ilikuwa 10 % (NOT 25 % sijui kama mwaka huu imepanda kufikia 25 %) na import duty 20 % (uko sahihi hapa). Pia sijui kama registration ya gari ina percentage maalumu maana nijuavyo mimi hii ni fixed amount kutokana na ukubwa wa injini wa gari.
   
 12. Mathias

  Mathias Senior Member

  #12
  Aug 31, 2009
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wakubwa nashukuru kwa ufafanuzi japo sie aliyeuliza, ila nkuwa na tatizo la kujua mchanganuo huu wa kodi
  Inakuwaje kama gari likipitia bandari ya mombasa mpaka mpakani kwetu pale horohoro nafikiri sina uhakika panaitwaje! Kuna mtu mwenye uzoefu na ili? Kunatakiwa taratibu gani?
   
 13. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Tumia bandari ya Mombasa kama hutaki usumbufu na manyanyaso ya TRA
   
 14. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hapa ni kwamba utakuwa umekwepa kulipia port charges kwa TZ ila utakuwa umezilipa kwa Wakenya. Kodi zingine zinabaki kama kawaida (i.e VAT 18 %, Import duty 20 % na excise duty 10 %) baada ya gari lako kukanyaga ardhi ya TZ. Hizo nilizoweka nyekundu sijui kama nazo zimebadilika kwa mwaka huu (2009/2010) wa fedha. Kama wewe ni mtumishi wa umma basi soma attachment hii hapa kuhusu mwongozo wa msamaha wa kodi uliotolewa na TRA Tarehe 16 mwezi wa saba mwaka huu.
   

  Attached Files:

 15. Mathias

  Mathias Senior Member

  #15
  Sep 2, 2009
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkubwa RMashauri
  Nashukuru kwa ufafanuzi na mchanganuo
  Ni kweli gharama za bandari (port charges) zitaenda kwa wakenya, uzoefu nilioupata mara tatu sasa ni kwamba bandari yetu ya Dar inachukua zaidi ya wiki mbili gari kutoka na ata kama mtu una document zote na umeshafanya malipo halali, kila siku kuna story mpya! Mara server ipo low, mara long room hawajapokea malipo kutoka bank yani kila sehemu ni pressure na pindi gari linapotoka imetokea mara moja matairi yamebadilishwa, Nimejaribu kutumia mawakala watatu tofauti na kila mmoja ana story zake! Inapofika gari kutoka zile port charges pamoja na storage zinakuwa kubwa sana! Ndo maana nimeamua kujaribu mombasa, pale mpakani naambiwa hakuna ubabaishaji kama wa dar, swali langu ni kwamba kunatakiwa maandalizi yoyote ya makaratasi kutoka dar au kila kitu kinafanywa na jamaa wa mpakani? Asante mkubwa
   
Loading...