Kodi ya Asilimia 10: Kwa kila Tshs 1,000 ya kwenye Miamala, tshs 280 ni za TRA kuanzia Julai mosi

*UFAFANUZI!*

_Watu wengi wamestuka sana kusikia kuwa kuanzia tarehe 01 Julai 2016, kila utakapotoa fedha kwenye ATM au huduma za fedha kwa mitandao ya simu, TRA itachukua asilimia 10 ya pesa hizo_.

_Ukweli ni kuwa kodi hiyo ya 10% kwenye muamala wa simu au kutoa pesa kwenye ATM itakatwa kwenye gharama ya kutolea au kutumia na wala siyo kwenye pesa zako_.

_Mwanamtandao Gabriel Mwang'onda amefafanua kuwa 'kwa mfano ukitoa sh milioni moja gharama ya kutolea ni sh 7500, basi serikali wanakata 10% kutoka katika hiyo sh 7500 (sh 750) na siyo kwenye sh milioni moja_'.

_Ngoja tuwafafanulie hapa ili watu wasije kukimbia na mabegi kutoa hela zao kwenye mabenki_.

Mtatiro J.

==========
kwani hiyo garama ya kutoa inakatwa kwenye hela za nani?watafute vyanzo vya mapato sio kodi rahisi
 
Mkuu sasa nimeelewa vizuri, nilikuwa nimeanza kuichukia sana Serikali ya mzee wa majipu sasa umenituliza roho yangu
 
*UFAFANUZI!*

_Watu wengi wamestuka sana kusikia kuwa kuanzia tarehe 01 Julai 2016, kila utakapotoa fedha kwenye ATM au huduma za fedha kwa mitandao ya simu, TRA itachukua asilimia 10 ya pesa hizo_.

_Ukweli ni kuwa kodi hiyo ya 10% kwenye muamala wa simu au kutoa pesa kwenye ATM itakatwa kwenye gharama ya kutolea au kutumia na wala siyo kwenye pesa zako_.

_Mwanamtandao Gabriel Mwang'onda amefafanua kuwa 'kwa mfano ukitoa sh milioni moja gharama ya kutolea ni sh 7500, basi serikali wanakata 10% kutoka katika hiyo sh 7500 (sh 750) na siyo kwenye sh milioni moja_'.

_Ngoja tuwafafanulie hapa ili watu wasije kukimbia na mabegi kutoa hela zao kwenye mabenki_.

Mtatiro J.

==========
Mtatiro hii umeielewa?

- To introduce VAT on fee based financial services (interest on loans not included)
 
Zito angesema ukweli na si kupotosha umma wakati hiyo 10 % inakatwa kampuni kwenye ile tozo ya kutolea pesa
 
Hapo inakuwaje kwa Benki kama Barclays ambao wamejipambanua kutokutoza ada kwenye miamala ya ATM, inamaana hata mitandao ya simu wakiamua kutokutoza ada miamala yao nao hawatadaiwa?
 
'Tumeipenda wenyewe...tumeichagua wenyewe...wacha waisome namba eeeh...waisome namba...CCM mbele kwa mbeleeee'×4. Ninauhakika ukimwimbia Mwana CCM wimbo huu leo atakutupia jicho hiloooo!
 
Unachofurahia ni nini sasa hapo ? Maana kama mfanyakazi ashakatwa kodi kwenye Mshahara halafu bado ukotoe kwenye ATM ukatwe tena r u serious? Hii kama ni kweli itarudhisha Enzi za ujima za watu kukaa na hela ndani badala ya kuweka benki ziingia kwenye mzunguko kwa watu kukopa maana benki hazina hela zinazungusha za waweka akiba watu wasipoweka akiba ni msiba kwa benki haitakuwa na hela ya kukopesha na ujue serikali ishakimbiza zake BOT. Tutakua tunaenda mbele au tunarudi kwenye enzi za ujima?
Patamu hapo! Mishahara sasa irejeshwe madirishani tu.
 
Sasa uoni kuwa mabanki na makampuni ya simu yataongeza gharama za service charge.
Hili ndio tunalopigia kelele, Makampuni ya simu yalishajiwekea viwango vyao yaani faida zao, sasa serikali ikianza kukata maana yake faida zao zitashuka watakuwa Chini ya makusanyo yao ya kawaida,
Kitachofuata hapo ni kupandisha gharama kwa watumiaji wa mwisho, ngoja tusubiri tuone
 
Kodi imeongezeka kwa asilimia hiyo iwe kwa makampuni au walaji ni kuwa gharama za kutuma fedha zitaongezeka tuu..ufafanuzi wa nini wakati gharama zimeongezeka wanavyoongeza kodi ya soda au bia kwa makampuni na wao si wanaongeza bei...
 
image.jpeg
 
UFAFANUZI!

Watu wengi wamestuka sana kusikia kuwa kuanzia tarehe 01 Julai 2016, kila utakapotoa fedha kwenye ATM au huduma za fedha kwa mitandao ya simu, TRA itachukua asilimia 10 ya pesa hizo.

Ukweli ni kuwa kodi hiyo ya 10% kwenye muamala wa simu au kutoa pesa kwenye ATM itakatwa kwenye gharama ya kutolea au kutumia na wala siyo kwenye pesa zako.

Mwanamtandao Gabriel Mwang'onda amefafanua kuwa 'kwa mfano ukitoa sh milioni moja gharama ya kutolea ni sh 7500, basi serikali wanakata 10% kutoka katika hiyo sh 7500 (sh 750) na siyo kwenye sh milioni moja'.

Ngoja tuwafafanulie hapa ili watu wasije kukimbia na mabegi kutoa hela zao kwenye mabenki.

Mtatiro J.
Mitandao ikikatwa si watafidia hasara hiyo kwa kupandisha gharama za huduma, hivyo atakayebeba mzigo huo ni mtoaji wa mwisho.
 
Sas ndo huone kwamba bajeti hii itatukandamiza wananchi wa hali ya chin, kodi bank imepanda kinachotokea makato kwa mwananch atakae tumia ATM bila shaka nayo inapanda.
 
Back
Top Bottom