Kodi Vurugizi zinapunguza mapato

Kodi Vurugizi zinapunguza mapato

Augustine Moshi

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2006
Posts
2,556
Reaction score
1,394
Hizi ni kodi ambazo zinavuruga au zinahujumu uchumi. Kwa mtazamo usio wa kina zinaweza kuonekana kama kodi za kuchangia mapato ya serikali lakini ukichunguza vizuri utaona kwamba zinapunguza sana economic activity na mwishowe hupunguza kiasi kitakachokusanywa.

Nitoe mfano hai. Nimekwenda sehemu ya utalii, Chala Hotel, nikiwa na mke na watoto watatu. Karibu na eneo la hoteli kuna kizuizi (gate) cha Idara ya Wanyamapori kwa ajili ya kukusanya kodi. Walidai kodi ya shilingi laki moja na sabini na tisa elfu (sh 179,000) kwa ajili ya siku nne ambazo nilipanga kupumzika pale hotelini.

Walidai nilipe sh 10,000 kwa ajili ya gari kwa kila siku, sh 5,000 kwa kila mtu kwa siku kama kodi ya kitanda, na sh 2,000 kwa siku kwa kila mtu kama kodi ya hifadhi.

Hawana risiti za TRA lakini wana risiti za zamani za serikali ambazo walinipa na kuandika ni malipo ya "general wildlife activities and conservation". The irony of this is that there are no wildlife activities in the area and the only conservation work around there is that which done by the hotel.

To add insult to injury this Wildlife office did not have an invoice to give to me when they demanded the second and last installment of my payme to them as I was leaving. They forced me to pay, without being invoiced, otherwise I could not leave. They are probably armed, so I paid.

I shall of course never visit the place again. I know others who have adopted a similar resolution. You kill rather than promote internal tourism when your charges are unreasonable, and unjustifiable.

Ukiiua biashara za hoteli unaua ajira za watu wengi. Hatukuacha mteja yeyote hotelini tulipoondoka. Kodi zitakusanywaje kama biashara zinafungwa?

There is absolute stupidity in some places. You maximize your taxes by charging reasonable amounts to a lot of people and not by charging a few people huge amounts.

In the case of Chala Hotel, there is no need for a Wildlife gate there. There is no service that is provided by the Wildlife Department to those who visit the place. It seems to me that the gate is there only to kill the hotel, and that is sad.
 
Ndio serikali tunayoambiwa inachapa kazi.

Utasikia wananchi kuweni wazalendo tembeleeni hifadhi za taifa gharama ni nafuu sana

Kwa maoni yangu, serikali ya awamu hii inafanya kazi vizuri lakini kuna watendaji wengine kama hao wa Idara ya Wanyamapori ambao wana mawazo mgando. Itabidi tumbua tumbua iwafikie.
 
Kwa maoni yangu, serikali ya awamu hii inafanya kazi vizuri lakini kuna watendaji wengine kama hao wa Idara ya Wanyamapori ambao wana mawazo mgando. Itabidi tumbua tumbua iwafikie.
Hizo kodi serikali inajua na imebariki
 
Kwa mtaji huu utalii wa ndani utakuwa ni ndoto. Tunalaumiwa kwa kutokwenda kutalii katika mbuga zetu hapa Tanzania. Lakini iwapo kuna kodi za aina hii, basi ni wachache miongoni mwetu ambao wanaweza kufanya hivyo. Matokeo yake tuwaachie watalii wa nje waendelee kufanya huo utalii japo na wao hulalamikia utitiri huu wa kodi.
 
As long as mnapigia chapuo taifa kubanwa !!.

Naserikal itaendelea kutafuta njia za kuwabana .
 
Tatizo sio kodi. Dunia nzima inahitaji tozo za kodi, iweze kujiendesha, watanzania wengi na waafrica wengi hatuna desturi ya kutoka au kutembelea sehemu za utaliii na tukitembelea tunataka tupate msamaha wa tozo. Hata uko South Africa watalii ni jamii za wazungu tuuu. Waafrika wengi bado tupo kwenye mawazo ya kutafuta Pesa na kuzaliana lakini sio kutembelea
 
Unawezaje kutenganisha SERIKALI na WATENDAJI ..? SERIKALI NI NANI? AU ndo Serikali ya mtu mmoja?

Traffic Officer akikuomba rushwa utasema ni serikali imekuomba rushwa? Kuna tofauti kati ya serikali na watendaji. Mtendaji kama huyu mzembe aliyeamua kuweka tozo ya wanyamapori mahali ambapo hakuna mtu anakwenda kuangalia wanyama ni jipu tu serikalini. Ni la kutumbua ili serikali isipate usaha.
 
Tatizo sio kodi. Dunia nzima inahitaji tozo za kodi, iweze kujiendesha, watanzania wengi na waafrica wengi hatuna desturi ya kutoka au kutembelea sehemu za utaliii na tukitembelea tunataka tupate msamaha wa tozo. Hata uko South Africa watalii ni jamii za wazungu tuuu. Waafrika wengi bado tupo kwenye mawazo ya kutafuta Pesa na kuzaliana lakini sio kutembelea

Nakubali tatizo sio kodi. Ni tozo zembe zinazoharibu fursa za kukusanya kodi. I would be happy to pay for"general wildlife activities" around Lake Chala Hotel if they existed. They don't.
 
Mimi ndio maana siendi kodi nyingi sana bora niingie porini nikaangalie mnyama ninaemtaka wanyama wamejaa kibao porini hakuna ulazima wa kwenda huko
 
Nilipanga kuchukua family twende Mikumi, umenitisha wacha twende tu Coco beach
 
Traffic Officer akikuomba rushwa utasema ni serikali imekuomba rushwa? Kuna tofauti kati ya serikali na watendaji. Mtendaji kama huyu mzembe aliyeamua kuweka tozo ya wanyamapori mahali ambapo hakuna mtu anakwenda kuangalia wanyama ni jipu tu serikalini. Ni la kutumbua ili serikali isipate usaha.
Serikali ni nani?
 
Nakubali tatizo sio kodi. Ni tozo zembe zinazoharibu fursa za kukusanya kodi. I would be happy to pay for"general wildlife activities" around Lake Chala Hotel if they existed. They don't.
Umeongea vizuri kila kitu kiko poa...mkuu Mimi nawashangaa watanzania wa JF kushobokea nyuzi za kijinga kwa nguvu nyingi tofauti na nyuzi za maana kama huu Uzi! Sio fare kabisa kwa Uzi huu kuwa na kurasa mbili licha ya muda mrefu tangu uanzishwe!!!
 
Back
Top Bottom