TANZIA Kocha Sven-Goran Eriksson amefariki Dunia

Ingekuwa bongo tayari mahema na viti nyumbani kwa marehemu, huku michango na wapigaji humo humo. Wenzetu wanaomba privacy, wasipigiwe wala kutumiwa jumbe, ukitaka tuma huko kwa website.....

Dunia mbili tofauti!!
Na daftari kuubwa pamoja na picha ya marehemu nyumba kwa nyumba vs mtaa kwa mtaa
Umaskini mkuu wangu unaleta yote haya
 
May his soul rest in eternal peace.

Naona baba yake bado yupo hai.

I wonder atakuwa ana umri gani.
 
Apumzike kwa amani, namkumbuka wakati wake akiwa mkufunzi wa timu ya taifa ya England
Watoto wa 2000 hawawezi kumjua

Nskumbuka mwaka 2002 world cup ilifanyikia huko Asia mechi zote tulikuwa tunaangalia saa mbili asubuhi kama sikosei kupitia antena ndefu aina ya SONET tv Panasonic

Mechi ilikuwa ni kati ya ENGLAND Vs BRAZIL robo fainali golikipa Siemens, namba saba Beckham na tisa Owen bila kumsahau mpiga mashuti Paul scholes

Gaucho alikuwa na Red card hakucheza, Ronaldo akawaangamiza England

Kocha alikuwa Erickson
 
Golikipa alikuwa Seamen sio Siemens
 

Sio kweli, Gaucho alipewa kadi kwenye hiyo mechi dakika ya 58 baada ya kumtungua Seamen. England ililala 2-1 Michuano hiyo iliandaliwa na Japan na Korea Kusini
 
Sio kweli, Gaucho alipewa kadi kwenye hiyo mechi dakika ya 58 baada ya kumtungua Seamen. England ililala 2-1 Michuano hiyo iliandaliwa na Japan na Korea Kusini
Mkuu ni miaka 22 sasa imepita nimekosea kidogo sana ila kumbu kumbu zangu zipo sawa

Brazil walivaa jezi ya blue na bukta nyeupe
 
Rip
 
Apumzike kwa amani.

Ingekuwa bongo ingekuwa fursa ya wasanii na wanasiasa kwenda kuuza sura kwa kupiga picha.

Ingekuwa fursa kubwa zaidi kwa Msechu kuachia track.
Halafu huyo jamaa jana nimemuona jamhuri stadium dodoma aseeh ule unene hapana.

Anyway rest easy coach
 
Kuna rafiki yangu shabiki Mkubwa wa England Toka kitambo,

Hii Taarifaa imemsikitisha,

Japo yeye alikuwa anamuona kuwa ni Avarege coach, kwamba kikosi kile Cha akina lampad, Gerald , Beckham, & nk kilimzidi uwezo .

REQUIESCAT in peace, Goran Ericksson.

If you want to know who Iam, The Answer is Ashe's & Burnt Embers.


(N.f. .f. n.s . n. c)

I was not. I was, Iam not. I care not.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…