Kocha Juma Mgunda kung'ang'ania Simba SC ni kuendelea kujishushia heshima na kujidumaza akili yako

Yaani umeandika pumba Ina maana akiwa kocha mkuu Azam, singida una uhakika hawezi kupiga mpunga??

Mpaka awe mpaka koni pale msimbazi acha Mambo yako bhana .

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
We jamaa una akili za kijinga sasa aende Azam na Singida kwani hizo timu zilikwambia kuwa zimemuhitaji Mgunda na akakataa.
Watz uachage ujuaji ya kijinga.
 
Hakuna kocha ambaye hapendi kufanya kaz kwenye timu kubwa. Pia hela zinaruhusu kwanini apate shida wakati simba wanampa kile anchohitaji.#NALIA NGWENA said
 
Naam, mlio karibu na kocha juma mgunda naomba mumuonyeshe mawazo na fikra sahihi yaliyoandikwa na the great thinker NALIA NGWENA.

Ndiyoo ukweli mchungu lakini pia ni tiba kwa mtu mwelevu na mwenye kufikiria.
Nimeikumbuka coastal union ya mgunda ambayo yanga alikua hapati matokeo kirahisi na hata akipata lazima yanga afanye kazi kweli kweli.

Mpaka zikaibuka kelele za mashabiki nakudai kuwa coast ni simba B ipo ili kuikazia yanga isipate pointi tatu muhimu.

Kumbe haikua hivyo Bali ni tecninic mujarabu za mwamba mmoja aliyependa kuvaa msuli na siyo mwingine Bali ni kocha wa mpira pep gadiola mnene Al watani juma mgunda mzawa.

Huyu mwamba anauwezo mkubwa ni moja Kati ya makocha wazawa taifa linawahitaji katika kukuza mpira wetu huu

Kila nikikumbuka fainali ya kombe la azam, mgunda akiwa benchi na kikosi chake kikiikabili yanga nakutoa sare ya mabao matatu kwa kila timu mpaka kupigwa mikwaju ya penati na ndipo yanga anaibuka kidedea nakuchukua kombe.

Ilikua ni bonge la fainali juma mgunda alipambana na kocha nabi kimbinu mpaka mchezo unamalizika.

Hakika mwamba mgunda alitekeleza majukumu yake ipasavyo.
Kila nikikumbuka mbinu zake alizozitumia kuisogeza simba sc kimataifa baada ya simba kumfukuza kocha naona kabisa mgunda anasitahili kuwa na timu na siyo kuwa kocha msaidizi.

Kila nikiitazama azam, singida na ihefu naona kabisa mzawa mgunda anastahili kuwa kocha wa hizo timu na ataleta upinzani mkubwa katika timu kongwe za kariakoo.

Kwa uwezo alionao mgunda hastahili kuwa kocha msaidizi pale simba, hayo Mambo amuachie suleimani matola maana bado anajifunza na aendelee kugain experience kutoka kwa hao makocha wageni.

Inanisikitisha sana kumuona robertinho akipiga tumbo la mgunda kwa midadi kabisa baada yakuona mchezaji wake amekosa au amepata goli, kiukweli hii ni dharau kabisa.

Kila ninapo muona munda kwenye benchi la simba huwa napata majibu kuwa wachezaji wa kibongo na makoncha ndoto yao kubwa ni kucheza au kufundisha yanga na simba tu, na ndiyo maana kocha au mchezaji anafurahia kukaa benchi hata Kama akiwa hapati namba.

Nikiwa Kama mdau wa mpira NALIA NGWENA THE GREAT THINKER nakuambia juma mgunda nenda katafute timu kwani kung'ang'ania simba nikujishushia heshima maana hao makocha wa kigeni wanaokuja hapo hakuna kigeni usichokijua.



Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
sasa hapa umeandika nini hasa?
 
Back
Top Bottom