Kocha Antonio Conte aachana na Inter Milan

tc_edo

Senior Member
Apr 9, 2021
123
225
Haijatimia mwezi tokea Kocha Antonio Conte (51) achukue ubingwa wa Serie A. Huu ulikua msimu wake wa pili kuifundisha timu hiyo iliyo chukua ubingwa kwa mara ya kwanza tokea 2010. Kuwepo kwa tetesi za kutoelewana kati ya club na kocha kuhusu kuuzwa wachezaji na mishahara kupunguzwa ndio huenda vimepelekea kocha huyo kuondoka. Inter Milan itamlipa Antonio Conte takriban €7.

Klabu imetoa taarifa ikisema " FC Internazionale Milano tumefikia muafaka wa kuvunja mkataba na Antonie Conte kwa makubaliano kati ya pande zote mbili (mutual consent). Klabu inapenda kumshukuru Antonio Conte kwa kazi nzuri alioifanya hasa kuipatia klabu taji la kumi na tisa. Antonio Conte atabaki kwenye historia ya klabu yetu. "

Antonio Conte anaondoka akiwa ameshinda mechi 52, droo 17 na kupoteza 7 katika mechi 76 za seria A.

IMG_20210526_211248.jpg
 

usser

JF-Expert Member
Sep 25, 2015
13,256
2,000
Kinachotokea huko inter na kule ufaransa Kwa
Lile ambao nao n mabingwa havina tofaut

Kimsingi wanajarbu kujikunbusha Kama
Monaco walivofanya wakat walibeba
Ndoo ya ligi 1
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom