ahsanteni wote kwa ushauri wenu. Tatiizo hili sasa nimeishatatua.
ahsanteni wote kwa ushauri wenu. Tatiizo hili sasa nimeishatatua.
umelitatuaje, please tupe yaliyojiri.
Sister wangu alikuwa mmoja wa watu niliomueleza baada ya kuona sipati ushauri mzuri na wa maana hapa. Well kafoka foka lakini unajua tena wanawake wakiwaka unakuwa kimya, Anyway alivyomaliza akanambia nimtumie yeye namba na hiyo laki 3 alafu yeye ataongea naye. Nkafanya hivo, sasa leo nimeongea na yule bibie kasema sis kamtumia laki 5 na kamuelekeza akapange na ajibane vipi wakati anatafuta kazi. Keshajulishwa atakavyomaliza hiyo hela ahakikishe kapata kazi.
Ila mi sishangai Mwisho wa mwezi huu ndugu zangu so watu tumekinga si unajua tena ukifika.
Kiufupi Siji kutongoza mdada mwenye Kichanga tena. Mwezi huu budget yangu imevurugika mbaya mpaka sijui ka ntaumaliza bila kukopa.
Ok, This is how it was. Nlienda Mbeya kikazi kwa muda wa kama wiki 3 hivi tokea 29th May mpaka 21st June. Muajiri alinilipia Hotel na chakula pale hoteli nlikuwa nikila ninachotaka na ku sign tu. Kabla hata wiki haijaisha nligundua kuwa nahitaji Companion wa kike to get me through the weeks. Nkapiga simu naumwa next day na kwenda kuzurura Town. Katika pitapita zangu mkononi nikiwa na T-shirt 3 kali za mtumba nlizokuwa nimenunua siku hiyo nkamuona binti bomba sana kwa mbali. All was fine mpaka nlivomsogelea nkaona kabeba mtoto mchanga mgongoni, Nkajipa moyo sio wake na kumuingia. Nlimuanza kwa kumshauri amfunike vizuri mtoto kwani hali ilikuwa baridi na upepo mkali. Nlimsifu mtoto alivyo mzuri huku nikiuliza jina la mtoto na kudai kafanana na mama yake. Nia yangu ilikuwa ni kuhakiki mtoto ka ni wake. Alikana na kudai kachukua sura ya baba yake. Anyway Story zilianzia hapo na nliendelea kuongea naye huku tukitembea kwa pamoja. Tulipanda basi moja ingawa nilikuwa siendi anakoenda, aliposhuka nami nkashuka na kupewa namba kwa sharti nsipige usiku.
Siku iliyofuata Nliripoti kazini na lunchtime nkampigia. Tuliongea kwa kama saa nzima. Alinieleza kazalishwa na mume wa mtu (Mkristo) so hawezi kuolewa naye. Aliendelea kueleza jamaa anahudumia kila kitu kampangishia chumba na anampa elfu 5 per day yaani 150,000 per month pia mtoto akiumwa na hela ndogo kama vocha e.t.c. Tulizoeana kwa kipindi kifupi nkamualika hoteli aje tubadilishane mawazo kama friends na kumtumia tax mida ya jioni akaja. Tukaongea tu ile siku bali jumaamosi ya wiki ile nlishinda hotelini akaja na kuanzia siku ile tukawa wapenzi. Kama kawaida ya mwanaume mimi uongo mwingi nlimmwagia na ahadi kibao fix. Mapenzi yalinoga mpaka akaacha kulala kwake na kuhamia pale hotelini kwangu. Alikuwa ananyonyesha mtoto so nilikuwa najilia tu peku.
Matatizo yalianza pale Baba wa yule mtoto alipoambiwa na wapambe kuwa nyumba ndogo yake hailali tena nyumbani. Alikuwa na funguo za ghetto la yule demu so akaenda kubeba kila kilicho mle ndani alichomnunulia yule demu. Mwenye nyumba akakabidhiwa chumba apangishe na kurudisha kodi iliyobaki. Tulienda wote kwake nikayashuhudia haya. Baada ya mimi kuona hivo, siku ninayoondoka (21st June) nilimuamishia mrembo wangu guest ya bei rahisi na kumlipia siku 10. Nkamuachia na 50 ya kula siku 10. Nkasepa na kurudi Dar.
Sasa hapa Kichwa kinaniuma nisaidieni wana JF nifanyeje? Ukichehe wangu umefanya nimejitwisha Limzigo likubwa na mbaya zaidi yule mwanamke kwao waislamu hivyo kuzaa na mkristo na kukubali kuwekwa nyumba ndogo walishamtenga na hili alinambia mwanzo kabisa. So kurudi kwao hawezi maana huwa wanamfukuza tu. Hapa kichwa kinaniuma mawazo hayaishi. Mtoto sio wangu so SIWEZI hudumia milele na kodi ya guest na hela ya kula yule mwanamke vinaisha in 4 days time. Alisharudi kwa baba wa yule mtoto kamkataa na sasa anasema yule mtoto sio wake maana demu malaya. Mpenzi mwenyewe hana ushauri wa maana analia tu siku nizima hata tukiongea kwenye simu kilio tuuu. Nafikiria sijui nimzimie simu au? Please, PLEASE, PLEASE, PLEASEEEEEEEEE Nishaurini Najitoaje humuuuuuuuuuu.
Rudia kuangalia maneno yako hapo kwenye rangi. Unampenda binti huyu na unamthamini ndio maana unakosa raha. Sasa jitahidi kadri ya uwezo wako umsaidie. Nakuomba sana umsitelekeze. Kila la heri.
Hahaha unanifurahisha ndugu yangu. Hapa keshaingia kwenye blacklist siku nyingi yaani namba yangu haitopatikana kwake. Sitaki hata kumsikia sio kumuona tu. Kwenye maisha haitakiwi uchukue matatizo ya mwenzio umpokee. Mwenyewe nimejizoelea wanawake wa Dar akishaona unamkatia simu anatuma vi msg viwili vi 3 alafu anakushiti. Ila huyu alikuwa anaagua kilio utadhani kafiwa. Nimekula hasara kubwa hapa hela yangu inaniuma sanaaaaaaaaaaaaaaaa. Imenibidi nigombanie daladala kuja kazini leo. Na maisha haya mwezi huu mzima kuja kazini na kurudi. Natamani niombe hela yangu irudi. Mateso matupu. Alafu yeye ukiangalia hajateseka hata kidogo katoka guest kaenda kuishi na kitita cha hela.
Finaly jana nlipata courage ya kumwambia ahadi zote za kumuoa ama kumleta dar zilikuwa ni za uongo. Na sasa kimpango wake, akaomba nimtafutie kazi hata ya u house girl tu. So mwenye kuhitaji mschana wa kazi mwenye kichanga cha miezi mi 5 ani pm.
Thanks Jestina for your observation.
Hata wewe ukiangalia mazingira ya huyo binti, kuzalishwa na mtu ambaye hana matarajio yoyote naye, kutengwa na familia yake, kisha sasa amekataliwa na huyo bwana aliyekuwa anamuweka mjini, hapo kunahitajika moyo wa ubinadamu japo kiasi kidogo.
Wakati mwingine tukubali kubeba majukumu yanayotokana na tamaa zetu za kimwili ama uongo wetu.
btw, ombi lako bado ninalitafakari.:thinking::thinking: